Rais Magufuli amempongeza mbunge wa Singida Mashariki (CCM), Miraji Mtaturu akisema jimbo hilo lilikuwa limetelekezwa na Tundu Lissu.
Akizungumza leo Jumatatu Septemba 16, 2019 katika hafla ya uzinduzi wa rada za kuongoza ndege katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Rais Magufuli amewapongeza wajumbe wa kamati ya Bunge ya Miundombinu pamoja na mbunge huyo wa Singida Mashariki, aliyemtaka akawatetee wananchi bila kujali vyama.
“Nimefurahi kumuona hapa kwenye Kamati ya Miundombinu mbunge wa CUF , lakini pia na mheshimiwa Mtaturu wa lililokuwa jimbo lililokuwa limetelekezwa na Tundu Lissu.
"Saa nyengine majimbo yanakosa uwakilishi...Kama ulivyoagiza mheshimiwa Spika (Job Ndugai) kwamba tushughulikie tatizo la maji katika jimbo lile…kama tulivyoshughulikia jimbo la Dar es Salaam…ninakuahidi kwamba serikali yangu itashughulikia, ili yale yaliyokuwa yamechelewa yaanze kufika haraka haraka," amesema Magufuli.

Mtaturu amechaguliwa hivi karibuni kuwa mbunge wa Singida Mashariki kuchukua nafasi ya Lissu ambaye Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai alitangaza kuwa amepoteza sifa za kuwa mwakilishi wa wananchi wa jimbo hilo.
Loading...
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi
==>>... << BOFYA HAPA Kui Install>>
Mgid
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )