Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Sunday, September 1, 2019

Rais Magufuli Amualika Rais Yoweri Museveni katika Kongamano La Wafanyabiashara Tanzania Na Uganda

adv1
Rais Magufuli amemualika Rais Museveni wa Uganda katika ufunguzi wa mkutano mkubwa wa Wafanyabiashara kati ya Uganda na Tanzania  ambao utawashirikisha wafanyabiashara zaidi ya 1000 ambao watapata nafasi ya kujadili namna ya kuongeza biashara mpya baina ya nchi hizi Mbili.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa wakati akizungumza na waandishi wa habari alipokuwa akihamasisha  wafanyabiashara wa Tanzania kujitokeza Kwa wingi kushiriki katika kongamano hilo linalotaraji kufanyika Septemba 6,2019 katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Bashungwa amesema kongamano hilo litafunguliwa na Rais Yoweri Museven wa Uganda, litahudhuriwa pia  na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli

Aidha Waziri Bashungwa ametoa wito kwa wafanyabiashara wa mikoa ya kanda ya ziwa ambao wengi wao ndio wamekuwa wakifanya biashara Moja kwa Moja na nchi za jirani hili waweze kupata mtandao mpya wa kibiashara.

Ametaja na kusema muungano wa kimtandao baina ya Tanzania na Uganda utafungua njia mpya ya Biashara hadi Sudan ya kusini ambao wamekuwa wakifanya biashara na Uganda kila uchwao.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )