Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Tuesday, September 17, 2019

Rais Magufuli azuia ukusaji Ushuru machinjio ya Vingunguti.....Atoa Maagizo MAZITO Kwa Uongozi wa Mkoa wa Dar, Ilala na NHC

adv1
 Rais John Magufuli ameuagiza uongozi wa Hamashauri ya Ilala kutochangisha fedha katika machinjio ya Vingunguti hadi pale watakapokamilisha ujenzi wa machinjio ya kisasa.

Rais Magufuli amesema hayo, alipofanya ziara ya kushtukiza na kuwataka viongozi wa Halmashauri hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na watendaji wengine kuangalia namna ya kukamilisha kazi hiyo ili kuwaondolea adha wafanyabiashara wa maeneo hayo.

Amesema, kuanzia sasa mkurugenzi wa Halmashauri na watendaji wengine ni marufuku kukusanya ushuru wa aina yoyote sambamba na kuwataka kufanyia kazi maagizo yake usiku na mchana.

Uamuzi huo umepokelewa kwa shangwe na wafanyabiashara wa eneo hilo la machinjioni ambalo linadaiwa kukusanya takribani milioni 100 kwa mwezi baada ya kupita akitokea kwenye uzinduzi wa Rada na kiwanda cha mabomba ya plastiki kilichopo maeneo ya Vingunguti jijini Dar es Salaam
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )