Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Friday, September 20, 2019

Serikali yaagiza Halmashauri zote za mkoa wa Shinynaga kujenga maeneo ya Maegesho ya malori ya mizigo kabla ya octoba 25 mwaka huu.

adv1
NA SALVATORY NTANDU
Wakurugenzi wa Halmashauri za mkoa wa Shinyanga wametakiwa kujenga maaeneo ya maegesho ya malori ya mizigo na mafuta ambayo yemekuwa yakiengeshwa katika maeneo yasiyorasimi(makazi ya watu) hali ambayo inaweza kuhatarisha usalama wa wananchi kabla ya octoba  25 mwaka huu

Kauli hiyo imetolewa jana na Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack kwenye kikao cha robo ya pili ya bodi ya barabara mkoa wa shinyanga, na kusema kuwa kumekuwa na tabia ya uegeshaji holela wa malori ya  katika makazi ya watu huku mengine yakiwa na kemikali hatari kama vile gesi na mafuta.

Amesema serikali haiwezi kukubali hali hiyo huku wenye mamlaka ya kusimamia na kupanga maeneo ya miji na wilaya wakiwa hawatimizi wajibu wao na kuendelea kuruhusu uegeshaji holela wa malori hayo ambao ni hatari kwa maisha  kwa uslama wa wananchi wa mkoa huo.

Amefafanua kuwa utengaji wa maeneo ya malori ya mizingo kwenye halmashauri za mkoa wa shinyanga kutaongeza mapato  kutokana na malori hayo na pia itawawezesha wamiliki wa malori hao kutoibiwa vifaa vyao vya magari katika vituo hivyo kwani  katika maeneo hayo kutakuwa na ulinzi wa kutosha.

Michael Matomora ni mkurugenzi wa Halamshauri ya Ushetu na Godfrey Mwangulumbi Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga wamesema katika bajeti ya mwaka 2018/19 hawakutenga bajeti kwaajili ya kutenga maeneo hayo lakini kwa mwaka huu wa fedha watahakikisha agizo hilo linatekelezwa harasa.

Naye Kaimu Meneja wa TANROAD mkoa wa Shinyanga Mhandisi, Mibara Ndilimbi amesema kwa sasa Wakala  huo unaendelea kujenga eneo la maengesho la Kagonjwa Isaka ili kuhakikisha tatizo hilo linapatiwa ufumbuzi sambamba na kuboresha eneo la Maegesho la Mjini Kahama.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )