Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Friday, September 20, 2019

Trump kupokea ushauri wa kijeshi juu ya kuiadhibu Iran

adv1
Wizara ya ulinzi ya Marekani, Pentagon inatarajiwa hii leo kumkabidhi rais wa nchi hiyo Donald Trump, mikakati kadhaa ya kijeshi anayoweza kuitumia kujibu mashambulizi dhidi ya miundombinu ya mafuta ya Saudi Arabia, ambayo utawala wa Trump unaituhumu Iran kuyafanya. Iran imekanusha tuhuma  hizo. 

Maafisa wa kijeshi watakutana na Rais Trump katika Ikulu ya White House, na kumpa orodha ya vituo vinavyoweza kulengwa ndani ya Iran, na wakati huo huo kumtahadharisha kiongozi huyo kuwa mashambulizi dhidi ya Iran yanaweza kusababisha vita kamili. 

Afisa ambaye hakupenda jina lake litajwe amesema huo ni mkutano wa kwanza unaoweza kuchukua uamuzi juu ya namna ya kulipiza kisasi kwa mashambulizi dhidi ya mmoja wa washirika muhimu wa Marekani, Saudi Arabia. 

Hata hivyo, uamuzi wowote wa kujibu mashambulizi hayo, utategemea ushahidi utakaotolewa kuthibitisha kwamba ndege zisizo na rubani pamoja na makombora vilivyoipiga miundombiu ya mafuta zilitokea Iran.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )