Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Monday, September 23, 2019

Wabunge wa Kiarabu Israel Waapa Kumng'oa Madarakani Benjamin Netanyahu

adv1
Wabunge wa vyama vya kisiasa vya Kiarabu katika bunge la Israel hapo jana wamemuunga mkono mkuu wa zamani wa jeshi Benny Gantz anaegombea wadhifa wa waziri mkuu, na kumuongezea uwezekano wa kumshinda kiongozi aliye madarakani Benjamin Netanyahu

Hatua hiyo ya kihistoria ni ishara ya dharau kwa Netanyahau ambaye anatuhumiwa kuchochea chuki dhidi ya Waarabu wakati ya kampeni yake ya kugombea tena uwaziri mkuu. 

Ni mara ya kwanza katika kipindi cha miongo mitatu kwa vyama vya Kiarabu kumuunga mkono mgombea wa wadhifa wa waziri mkuu.

 Kwa sasa ni juu ya Rais wa Israeli Reuven Rivlin kuamua ni mgombea yupi wakupewa nafasi ya kuunda serikali ya mseto na kuongoza kama waziri mkuu. 

Gantz na Netanyahu wote wawili wamekosa wingi wa viti katika bunge la viti 120. Lakini kuungwa mkono na vyama vya Kiarabu, huenda kukamsaidia Gantz.

Aymen Odeh, kiongozi wa mungano wa makundi ya waarabu , amemuambia  Rais Rivlin kwamba kipaumbele cha muungano wao ni kumzuia   Netanyahu kuongoza kwa muhula mwingine. 

Amesema hawamuidhinishi Bwana Gantz na sera zake, lakini wanafanya juhudi za kujaribu kumzuwa Benjamin Netanyahu kupata muhula mwingine madarakani, na vilevile kutuma ujumbe wa wazi kwamba hali ya baadae ya Israeli lazima ijumuishe ushirikishwaji sawa na kamili wa raia wake wa kipalestina.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )