Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Tuesday, October 1, 2019

Atiwa Mbaroni na TAKUKURU Kwa kwa kuisababishia Serikali hasara ya milioni 15

adv1
Kamanda wa TAKUKURU mkoa wa Dodoma, Sosthenes Kibwengo, amesema wanamshikilia Emmanuel Mziwanda ambaye alikuwa Afisa afya mkuu na mratibu wa mradi wa Belgian Fund for Food Security BFFS Halmashauri ya wilaya ya Bahi kwa tuhuma za kusababishia hasara ya shilingi milioni 15.

Kibwengo akizungumza leo Jumanne Oktoba Mosi, 2019 amesema mtuhumiwa huyo aliyekamatwa akiwa msibani alikuwa akitafutwa na taasisi hiyo tangu Julai,  2017 akikabiliwa na mashtaka ya kughushi nyaraka na kumdanganya mwajiri wake.

Amesema kitendo hicho kimeisababishia Serikali hasara ya Sh15 milioni na kwamba baada ya uchunguzi kukamilika  na mkurugenzi wa mashtaka (DPP) kutoa kibali cha kumfikisha mahakamani, mtuhumiwa alitoweka kusikojulikana.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )