Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, October 17, 2019

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan Kufungua Maonyesho Ya Pili Ya Viwanda Mkoani Pwani

adv1
NA MWAMVUA MWINYI,PWANI
MAKAMU wa Rais wa Jamhur ya Muungano wa Tanzania ,Samia Suluhu Hassan anatarajia kufungua maonyesho ya viwanda ambayo yanafanyika kwa mara ya pili mkoani Pwani, octoba 17  mwaka huu.
 
Katika maonyesho hayo ,wenye viwanda 206 wamejitokeza kushiriki .
 
Maonyesho hayo yataambatana na kongamano la uwekezaji litakalofanyika octoba 19 na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Wazir Mkuu Kassim Majaliwa.
 
Akizungumza na waandishi wa habari  kuhusu suala hilo, mkuu wa mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo alisema, waratibu wa maonyesho hayo watakuwa ni wabobezi wa masuala ya maonyesho kama hayo kampuni ya magazeti ya serikali (TSN) pamoja na mamlaka ya maendeleo ya viwanda (TANTRADE) .
 
Alieleza, malengo ya matukio hayo ni kuonyesha kwamba mkoa wa Pwani ,umedhamiria kuwa ukanda wa viwanda,wenye viwanda kupata masoko ya uhakika,kupanua wigo wa soko la ndani ya mkoa kufikia kimataifa na ,kuvutia wawekezaji wapya.
 
Aidha Ndikilo alifafanua lengo la kongamano hilo ,kuwa ni kuonyesha fursa za uwekezaji zilizopo mkoani humo kupitia sekta mbalimbali ikiwemo utalii,uchumi,kijamii,kilimo,uvuvi na viwanda.
 
“Kufanyika kwa kongamano hili italeta picha halisi ya fursa zote zilizopo mkoani Pwani,na kuonyesha namna mkoa ulivyopiga hatua katika sekta ya viwanda,uwekezaji na fursa za miradi mikubwa ikiwemo mradi mkubwa wa ujenzi wa uzalishaji umeme megawatts 2,100 STIGO ,huko Rufiji”alibainisha Ndikilo.
 
Hata hivyo,mkuu huyo wa mkoa alisema wenye viwanda maonyesho ya mwaka jana walikuwa 166 mwaka huu wanatarajia  wameongezeka 206.
 
Nae Januarius Maganga wa TSN alisema ,wanakwenda kuratibu maonyesho hayo ikiwa ni maonyesho ya kumi .
 
Maonyesho hayo pia yatafungwa octoba 23 mwaka huu na Wazir Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )