Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, October 24, 2019

Waziri Kamwelwe aagiza kukamatwa kwa anayeendesha mtandao wa ATCL Aviation TV kwa kutangaza UONGO kuwa ndege nyingine mpya Inakuja

adv1
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano nchini Tanzania, Isack Kamwelwe ameagiza anayeendesha mtandao wa ATCL Aviation TV kukamatwa kwa kutangaza kuwa ndege nyingine mpya aina ya Dreamliner inakuja nchini wakati si kweli.

Kamwelwe ameeleza hayo leo Oktoba 24, 2019  jijini Dar es Salaam katika kongamano la Tehama lililowakutanisha wadau mbalimbali wa sekta hiyo kujadili mchango wake kwa maendeleo ya uchumi wa viwanda.

Amesema kila jambo lina mamlaka zake za kutangaza na kama ni suala la ndege, wizara yake ndio ina dhamana ya kutangaza.

Amesema ameliuliza Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) wakamueleza kuwa hawakifahamu chombo hicho, nao pia wanashangaa.

"Nimeagiza atafutwe nimemwambia na Waziri wa Mambo ya Ndani (Kangi Lugola) kuangalia sheria ya kumshtaki. Kama hakuna sheria tutamsumbua tu mpaka wenzake wamuonee huruma," amesema Kamwelwe.

Amesema imefikia hatua vyombo vya habari vinatangaza kifo cha mtu, kusisitiza kuwa Taifa  lina maadili yake na hali hiyo haitaachwa iendelee.

"Kuna utaratibu wa kutangaza jambo, kama ni kifo familia ndiyo watatangaza. Kama mimi naumwa, wewe inakuhusu nini kama sijakwambia?" amehoji waziri Kamwelwe.

Amesema siku chache zilizopita, ndege ya ATCL ilizuiwa nchini Afrika Kusini kwa sababu baadhi ya Watanzania kutoa taarifa za uongo mitandaoni.

Credit: Mwananchi
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )