Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Wednesday, December 18, 2019

Bajeti ya Jeshi la Marekani Mwaka Ujao 2020 ni Balaa...Tazama hapa

adv1
Marekani ni nchi yenye bajeti kubwa zaidi ya kijeshi duniani, yakiwa ni matokeo ya sera yake ya kuwa na nguvu kubwa zaidi  za kijeshi katika uga wa kimataifa. 


Washington huongeza kila mwaka bajeti yake hiyo; na kwa kufanya hivyo kupiga hatua zaidi za kupanua na kuimarisha nguvu zake za kijeshi.

Katika muendelezo wa sera hiyo, Baraza la Seneti la Marekani, siku ya Jumatatu ya tarehe 16 Desemba lilipitisha kwa kura 76 za ‘ndiyo’ dhidi ya kura sita tu za ‘hapana’ bajeti ya dola bilioni 738 kwa ajili ya wizara ya ulinzi ya nchi hiyo, Pentagon kwa mwaka ujao wa 2020.


 Kufuatia kupitishwa bajeti hiyo na Seneti, mswada huo ulitazamiwa kuidhinishwa rasmi na kuwa sheria jana Jumanne, baada ya kusainiwa na rais wa nchi hiyo Donald Trump.

 Wiki iliyopita, Baraza la Wawakilishi la Marekani, ambalo linahodhiwa na chama cha Democrat liliupasisha kwa kura 377 zilizounga mkono dhidi ya 48 zilizopinga, mswada wa bajeti ya ulinzi ya nchi hiyo kwa mwaka 2020, unaojulikana kama Sheria ya Utoaji Mamlaka ya Ulinzi wa Taifa, kwa kimombo National Defense Authorization Act (NDAA) ambayo ndiyo iliyoainisha sera na bajeti ya ulinzi ya Marekani kwa mwaka wa fedha wa 2020.

 Trump na wajumbe waandamizi wa chama chake cha Republican katika mabaraza hayo mawili yanayounda Kongresi ya Marekani yanakuchukulia kupitishwa kwa bajeti hiyo ya ulinzi kwa mwaka 2020 kuwa ni ushindi mkubwa kwao kutokana na kuzingatiwa na kuambatishwa matakwa yao katika bajeti hiyo.

 Mswada wa bajeti ya ulinzi kwa mwaka 2020 unajumuisha pamoja na mambo mengine asilimia 3.1 ya nyongeza ya mishahara kwa ajili ya askari na uanzishaji wa kikosi cha anga za mbali, kikiwa ni kipaumbele cha Trump kwa ajili ya kuwa na uwezo wa juu zaidi kijeshi.

Kuna mambo kadhaa ambayo yameongezwa katika mswada wa bajeti ya ulinzi ya Marekani katika mwaka 2020, kikiwemo kipengele kinachohusu vikwazo vya lazima dhidi ya bomba la usafirishaji mafuta na gesi ya Russia kuelekea Ulaya, hususan bomba la usafirishaji gesi kuelekea Ujerumani, lijulikanalo kama Nord Stream-2 pamoja na marufuku iliyowekwa kwa jeshi la Marekani kuwa na ushirikiano wa kijeshi na wa moja kwa moja na Russia. 


Katika mswada huo, wabunge wa Marekani wamejumuisha pia vifungu kadhaa vinavyohusu kuiwekea vikwazo Uturuki kwa sababu ya kununua kwa Russia mfumo wa ulinzi wa anga wa S-400 na vile vile kupiga marufuku kuipatia nchi hiyo ndege za kivita aina ya F-35.

Katika mswada huo kuna vifungu pia vinavyohusu vikwazo dhidi ya Rais Bashar al-Assad wa Syria pamoja na shakhsia au taasisi zote zinazoshirikiana na nchi hiyo. 


Mpango wa Trump wa kuanzishwa kikosi cha anga za mbali kwa bajeti ya dola bilioni 71.5 nao pia umejumuishwa kwenye mswada huo wa bajeti ya ulinzi. 

Kwa mujibu wa duru mbili kutoka chama cha Demokrati katika Kongresi ya Marekani, bajeti ya ulinzi ya nchi hiyo, imeambatisha pia kifungu kuhusu sharti zitalopewa nchi kadhaa ikiwemo Saudi Arabia, ambazo zinataka zijengewe vinu ya atomiki na Marekani. 

Kwa mujibu wa gazeti la Washington Times, hati rasmi ya “Sheria ya Utoaji Mamlaka ya Ulinzi wa Taifa imempa mamlaka Trump ya kuratibu sera kuhusiana na Iran na Saudia na pia kuhusu namna ya kudhamini bajeti ya ujenzi wa ukuta wa uzio katika mpaka wa pamoja wa Marekani na Mexico.

Kwa kuzingatia kuwa mswada wa bajeti ya ulinzi ni miongoni mwa sheria muhimu za bunge la Marekani zinazopitishwa kila mwaka, kuna viambatisho vingi vinavyoongezwa ndani ya mswada huo katika nyuga tofauti za kisiasa, kiusalama, kiuchumi n.k. 


Mswada huo huwa unagusia pia masuala muhimu ya kijeshi kama ununuzi, ukarabati na ufanyaji za kisasa silaha mbali mbali pamoja na kuainisha viwango vya mishahara ya wanajeshi. 

Lakini mbali na masuala hayo, katika mswada wa bajeti ya ulinzi ya Marekani ya mwaka 2020 kuna viambatisho kadhaa vilivyoongezwa na kupitishwa kwa kuzingatia malengo, matakwa na vile vile changamoto muhimu katika uga wa kimataifa ili kuweza kufikia malengo yaliyokusudiwa pamoja na kukabiliana na changamoto hizo tarajiwa.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )