Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, December 19, 2019

Mbowe Achaguliwa Tena Kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa.....Tundu Lissu Kuwa Makamu Wake

adv1
Mgombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amechaguliwa tena katika nafasi hiyo baada ya kupata kura 886 sawa na 93.5% dhidi ya mpinzani wake Cecil Mwambe aliyepata kura 59 sawa na 6.2%. Mbowe atatumikia nafasi hiyo kwa kipindi cha miaka mitano. 

Matokeo hayo yametangazwa leo Alhamisi Desemba 19, 2019 saa 11 alfajiri na msimamizi wa uchaguzi, Sylvester Masinde, akibainisha kuwa kura tatu ziliharibika.

Uchaguzi huo umefanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.


Baada ya Masinde kumtangaza Mbowe kuwa mshindi, idadi kubwa ya wajumbe wa mkutano mkuu  walinyanyuka kwenye viti  na kumfuata mbunge huyo wa Hai kwa ajili ya kumpongeza.


Wagombea wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Chama Taifa (Bara) walikuwa wagombea  wawili,Tundu Lissu na Sophia Mwakagenda, Lissu amepata kura 930 sawa na 98.8% huku Mwakagenda (aliyetangaza kujitoa akiwa ukumbini) akipata kura 11 sawa na 1.2%.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )