Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Friday, December 13, 2019

Maalim Seif "Awaponza" Makamanda Wawili wa Jeshi la Polisi.....Naibu Waziri Masauni Aagiza Waondolewe

adv1
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni amemuelekeza Inspekta Jenerali wa Polisi Nchini, Simon Sirro kuwaondoa Makamanda wa Polisi wa Mikoa Miwili ya Kusini Pemba   na Kaskazini Pemba kwa kushindwa kutekeleza Mradi wa Ujenzi wa Nyumba 16 za Makazi ya Polisi uliozinduliwa mwishoni mwa mwaka 2018 na Makamu wa Rais,Samia Suluhu Hassan pamoja na kuacha mikutano ya siasa ya Chama cha ACT Wazalendo  kuendelea Kisiwani Pemba  hali ambayo  kukaidi agizo la Kiongozi Mkuu wa Nchi..

Masauni ametoa agizo hilo jana Alhamisi Desemba 12, 2019 katika mkutano wake na waandishi wa habari mjini Unguja.

Amesema kwa muda mrefu kisiwa cha Pemba kimekuwa na matukio yasioridhisha jambo linaloashiria kuwa wameshindwa kazi.

Makamanda hao ni Hassan Nassir Ally wa Mkoa wa Kusini Pemba na  Sheikhan Mohamed Sheikhan wa Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Akitoa mfano wa matukio hayo, Masauni amesema Maalim Seif anafanya mikutano kila kona huku ikijulikana kuwa imezuiwa.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )