Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Saturday, December 7, 2019

Milioni 11 Zatumika Kulipia kadi za bima ya afya iliyoboreshwa (CHF) Kwa Wazee Kahama

adv1
SALVATORY NTANDU
Wazee 2271 katika Halamshauri ya Mji wa Kahama mkoani Shinyanga wamepatiwa kadi za bima ya afya iliyoboreshwa (CHF) ambazo zitawasaidia kupata matibabu bure kwa mwaka mzima na kuondokana kwenda kwa waganga wa kienyeji kutafuta tiba.

Wazee wasiojiweza waliosajiliwa na baraza la wazee la Halmashauri ya mji wa Kahama mkoani Shinyanga ni 6247 na waliopatiwa kadi za CHF ni 2271.

Hayo yalibinishwa jana Mwenyekiti wa Baraza la  wazee wa Halmshauri ya Mji kahama, Willfred Bilago wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini kahama  alisema  hapo awali wazee walikuwa wanahangaika kupata matibabu kutokana na kukosa kadi za CHF iliyoboreshwa.

 “Wazee tulikuwa tunaona ni bora kwenda kwa waganga wa kienyeji kutafuta tiba mbadala kuliko kwenda katika hospitali ambapo tulikuwa hatuthamini na wengi wetu walipoteza maisha kutokana huduma hizo zisizokuwa za kitaalamu”alisema Bilago.

Alisema kadi  za CHF zimesaidia wazee wasiojiweza kupata huduma za matibabu ambapo kwa unafuu na haraka kwani katika hospitali ya Halmashauri ya Mji wa kahama kunadirisha la kuhudumia wazee na madaktari maalum kwaajili wao.

 “Tunawaomba wadau,wafanyabiashara,viongozi wadini kusaidia upatikanaji wa kadi za CHF kwa wazee wasiokuwa na waangalizi ili waweze kupata matibabu bure kwani suala hili tukiiachia serikali pekee kwani nasi tunawajibu wa kuwatuza wazee wetu” alisema Bilago.

Nae Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Kahama Abel Shija alisema kuwapatia kadi za CHF wazee katika halmashauri hiyo ni takwa la kisheria hivyo hawana budi kulitekeleza agizo hilo.

kwa mujibu wa sera ya taifa ya  wazee  ya mwaka 2003 inazielekeza halmashauri kuhakikisha haki za wazee waliofikia miaka 60 zinalindwa pamoja na kuwapatia huduma bure za matibabu.

Mwisho.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )