Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Friday, December 27, 2019

Watu 15 wafariki na wengine 35 kujeruhiwa baada ya ndege ya Bek Air iliyobeba watu 98 kuanguka

adv1
Takriban watu 15 wamefariki baada ya ndege iliokuwa ikiwabeba abiria 98 na wafanyakazi kuanguka nchini Kazakhstan , kulingana na maafisa wa uwanja wa ndege wa nchi hiyo.

Wanasema kwamba ndege hiyo ya Bek Air ilianguka muda mfupi baada ya kupaa katika uwanja wa Almaty mapema siku ya Ijumaa.

Takriban watu 35 , ikiwemo watoto wanane walipelekwa hospitali. Ndege hiyo ni ya aina ya FlightZ92100.

Ndege hiyo ilikuwa ikielekea katika mji mkuu wa Kazakhstan wa Nursultan kutoka mji mkubwa wa Almaty.

Inadaiwa kwamba kwamba ndege hiyo ilipoteza mawasiliano mwendo wa saa moja na dakika 22 , kabla ya kugonga kizuizi kimoja na kuangukia nyumba ya ghorofa mbili.

Ndege hiyo haikuwaka moto baada ya kuanguka. Tume maaluma itabuniwa ili kubaini chanzo cha kuanguka kwa ndege hiyo.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )