Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Sunday, December 15, 2019

Watu 37 Walazwa baada ya kula chakula chenye sumu msibani

adv1
Watu 37 wamelazwa katika hospital ya rufani jijini Dodoma baada ya kusadikiwa wamekula chakula chenye sumu katika msiba uliotokea eneo la mtumba lililoko nje kidogo ya jiji hili.

Akizungumza hospitalini hapo Meya wa jiji la Dodoma Profesa Davis Mwamfupe amesema anashukuru jitihada za madaktari wa hospital hiyo waliofanikiwa kuokoa maisha ya watu hao ambao wanahara na kutapika kutokana na kula chakula kinachisadikiwa kuwa na sumu.

Naye Mkuu wa wilaya ya Dodoma Patrobasi Katambi amesema wanasubiri taarifa ya vipimo vya unga na maharagwe yaliyotumika kupikia kwenye msiba huo.

Amewashukru madaktari wa Hospitali hiyo kutokana na jitihada za huduma ya kwanza iliotolewa kuhakikisha wagonjwa hao wote wamepata Huduma.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )