Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, January 2, 2020

'Al-Shabaab' yateka basi na kuua abiria Watatu Kenya

adv1
Watu watatu wameuawa huku wengine kadhaa wakijeruhiwa baada ya watu wenye silaha wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa kundi la kigaidi la al-Shabaab kuteka nyara basi la abiria katika kaunti ya Lamu, pwani ya Kenya.

Irungu Macharia, Kamishna wa Kaunti ya Lamu amethibitisha kutokea shambulizi hilo na kubainisha kuwa, basi hilo la abiria lilikuwa linatokea mjini Mombasa likielekea Lamu kabla ya shambulizi hilo.

Inaarifiwa kuwa, watuhumiwa wa kundi la al-Shabaab wamefanya shambulizi hilo la kushtukiza katika eneo la Nyongoro lililoko karibu na wilaya ya Witu, kaunti ya Lamu.

Mapema mwezi uliopita, watu 10 waliuawa katika shambulizi jngine dhidi ya basi la abiria lililofanywa na genge la kigaidi la  al-Shabaab katika kaunti ya Wajir, kaskazini mashariki mwa Kenya mpakani na Somalia.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )