Showing posts with label habari za kitaifa. Show all posts
Showing posts with label habari za kitaifa. Show all posts

Tuesday, May 22, 2012

Huko Kenya nadhani wamebakiza tu kila nyumba kuwa na chama - UHURU azindua chake


Kenya's Deputy Prime Minister, Uhuru Kenyatta has formally ditched the party of independence KANU, by launching The National Alliance (TNA) party thereby ending weeks of anxiety on his preferred political vehicle, ahead of the forthcoming country's presidential contest.

This is certainly a tumultuous entry to the expanding scene of political parties in Kenya and many other African countries experiencing "expansion of political freedom, freedom of expression and a struggle for real democracy".

At a the official launch marked with glitz, glamour via latest technology including live satellite relays under the watchful gaze of the giant monument of his father on Sunday afternoon at the Kenyatta International Conference Center, Uhuru said, time has come for Kenyans to vote for leaders from political parties that are issue based, with ideologies that will transform the country. Uhuru also urged the youth to take over leadership roles in the country in the coming general election.

He said the new party will strive to conduct the country's politics differently, with people empowerment at the heart of his presidential bid.

The Gatundu South lawmaker promised an accountable Government that will provide a platform for the youth, who make up the bulk of the Country's population to, amongst other things, derive a livelihood from their talents.

The Deputy Prime Minister sidestepped the woes he faces before the International Criminal Court, but called for de-tribalised politics and a peaceful Electoral process as the Kenyan electorate goes to the polls, in the first General Election, under The New Constitution.

Francis Gachuri witnessed the launch, dubbed the 'i believe experience' and has the details in the video embedded below.
Uhuru Kenyatta officially unveiled a party that he will use in his quest to be president of republic of Kenya. The national alliance abbreviated, as TNA will be Kenyatta's party to state house.

HABARI KAMILI..>>>

Zitto in The Netherlands on agenda: Oil and Gas

Zitto Maxime the Netherlands
Zitto Kabwe with Maxime Verhagen - Deputy Prime Minister, Minister of Economic Affairs, Agriculture and Innovation
A delegation of members of the Parliament from Tanzania arrived in The Netherlands on Monday, for a 4-days study tour.

The tour which begins Monday 21st May 2012 until the 24th will see the Honorable MPs Zitto Kabwe, hon. Nasir, hon. Sarah Msafiri and David Kafulila and Ms. Pallangyo meeting representatives of the Netherlands Ministries of Foreign Affairs and that of Economic Affairs, Agriculture & Innovation (EL&I). The meeting will provide opportunities to discuss issues such as government policies on careful and transparent exploration/exploitation of natural resources and on management of the ensuing income, and Dutch experience in the field (Dutch disease and its prevention and cure).

They delegates will tour the port of Rotterdam to be followed by presentation of BAM international on LNG.

The MPs will also have a meeting with the Vice Prime Minister and Minister of Economic Affairs, Agriculture And Innovation, Mr. Verhagen.

The MPs will also have an opportunity for site and company visits.

They will meet the Netherlands enterprises that have expertise in  fields which are of immediate relevance to oil and gas exploration and accompanying service delivery.

Also in plan is to visit the Shell company for an introduction to upstream exploration and production and  off-shore exploration and development before adjoining for discussions on global energy dynamics as well as partnerships between countries and International Oil Companies.

They will  tour on the largest terminal in Europe and Vopak company at Europort terminal. Vopak is a provider of conditioned storage facilities and transshipment solutions for bulk liquids (oil and LNG). It operates in 31 countries worldwide at 84 terminals along the world’s major shipping lanes.

Another visit is to the Port of Rotterdam / Havenbedrijf Rotterdam (Port of Rotterdam Authority).

Rotterdam is the largest port with industrial complex of Europe of major, global importance both in field of transfer of containers as well as of (liquid and dry) bulk (crude oil, chemicals, coal, ore etc). The Port of Rotterdam Authority manages, operates and develops the port and industrial area. It invests in the development of the existing port area, new port sites (Maasvlakte 2), public infrastructure and the handling of shipping.

The MPs expect to gain first hand knowledge and experience from The Netherlands that may be beneficial to Tanzania.
Zitto Kafulila in the Netherlands
HABARI KAMILI..>>>

Monday, May 21, 2012

RAIS KIKWETE AFANYA UTEUZI WA MAJAJI WA MAHAKAMA YA RUFANI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewateua Majaji wawili wa Mahakama Kuu ya Tanzania kuwa Majaji wa Mahakama ya Rufani.

Walioteuliwa ni Jaji Semistodes S. Kaijage na Jaji Kipenka M. Musa na kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo, Jumatatu, Mei 21, 2012 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue, uteuzi wao ulianza tokea Machi 15, mwaka huu, 2012.

Kabla ya kuteuliwa kwake kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani, Jaji Kaijage (57) alikuwa Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam tangu Mei 17, 2007. Aliteuliwa kuwa Jaji Mahakama Kuu Novemba 28, mwaka 2000.

Naye Jaji Musa (57) alikuwa Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu Kanda ya Tanga kabla ya kuteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani.

Pia amewahi kuwa Wakili wa Serikali, Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba. Aliteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu Septemba 13, 2004.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
21 Mei, 2012
HABARI KAMILI..>>>

TAIFA STARS NA MALAWI KUKIPUTA JUMAMOSI DAR


KIKOSI cha timu ya Taifa ya Malawi, kinawasili nchini Ijumaa kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya timu ya Taifa, Taifa Stars, utakaofanyika Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Angetile Osiah, alisema kuwa wameshapata taarifa ya ujuo wa wageni wao hao.

Alisema licha ya kujua siku ya kuja lakini bado hawajataja idadi ya watakaokuja licha ya TFF kuwapa idadi ya watu 27 ambao watakuwa chini yao.

"Tumewaambia wakija 27 ni idadi ambayo itakuwa chini yetu kama watazidi wengine watakuwa chini ya Chama cha Mpira wa Miguu Malawi"alisema Osiah.Stars iliyopo kambini chini ya kocha Kim Poulsen inacheza mechi kwa ajili ya kujipima nguvu kabla ya kwenda kuivaa timu ya Taifa ya Ivory Coast ugenini Juni 2, jijini Abidjan.

 Mechi hiyo ya  mchujo wa kuwania tiketi ya fainali za Kombe la Dunia za mwaka 2014 kwa kanda ya Afrika dhidi ya Ivory Coast . wachezaji ambao wapo kambini kujiandaa na mchezo huo makipa; Juma Kaseja (Simba), Mwadini Ally (Azam) na Deogratius Munishi (Mtibwa Sugar).
Mabeki: Nassor Masoud Cholo (Simba), Aggrey Morris (Azam), Amir Maftah (Simba), Erasto Nyoni (Azam), Kelvin Yondani (Simba), Waziri Salum (Azam), Shomari Kapombe (Simba) na Juma Nyoso (Simba).

Viungo ni Mwinyi Kazimoto (Simba), Salum Abubakar (Azam), Nurdin Bakari (Yanga), Jonas Mkude (Simba), Shabani Nditi (Mtibwa Sugar), Edward Christopher (Simba- U20), Mrisho Ngasa (Azam) na Frank Domayo (JKT Ruvu- U20).Washambuliaji ni Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo), Ramadhan Singano (Simba-U20), Simon Msuva (Moro United- U20), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DR Congo), Haruna Moshi (Simba) na John Bocco (Azam).
HABARI KAMILI..>>>

JUHUDI ZA UNDER THE SAME SUN KATIKA KUWASAIDIA WATU WENYE ULEMAVU WA NGOZI NA UONO HAFIFU KANDA YA ZIWA

Mwanzilishi wa Shirika la mapambano dhidi ya ukatili kwa watu wenye ulemavu wa ngozi (Under The Same Sun) Peter Ash akiwa amembeba mmoja kati ya watoto 23 waliofanya vizuri kwenye masomo na kutunukiwa medali katika shule ya Lake View jijini Mwanza.

Shirika hilo linalotoa udhamini wa elimu kwa watoto wapatao 64, kati ya hao 23 wamefanya vyema kwenye mitihani shule mbalimbali za msingi jijini Mwanza, huku watoto 17 wakishika nafasi ya 1,2,na 3 hali hiyo ikichangiwa na kuwawezesha watoto hao vifaa maalum vya kuweza kuona na kusoma bila shida (miwani na lensi maalum).

Watoto ndani ya chumba cha kuzawadiwa medali.

Aidha Shirikahilo limetoa semina kwa walimu wa shule zinazowalea watoto wenye ulemavu wa ngozi na uono hafifu za Lake View na Jeris zote za jijini Mwanza, elimu ya jinsi ya kuwatunza, kuwalea pamoja na kuwahudumia. 

Under The Same sun pia ilishiriki kugawa kofia na mafuta maalum ya ngozi kwaajili ya kujikinga na mionzi mikali ya jua pamoja na kuwapima macho na kuwafanyia utafiti watoto wenye uono hafifu. 

Mafuta maalum yaliyogawiwa kwa watoto hao ikiwa ni sehemu ya mapambano dhidi ya maradhi ya kansa ya ngozi.

Mtoto Maisha Msobi mwanafunzi wa 'prep one' akiniandikia jina lake huku mapacha wawili Matias na Yohana, macho wakiyaelekeza kwenye kamera yako.

Wakipata flash ya pamoja kutoka kushoto ni Heri Abel, Matias, Yohana na Maisha Msobi

Madam Jackline Raymond anasema 'Tuwatunze watoto wasicheze kwenye mionzi ya jua kali tofauti na jua la asubuhi ambalo ni muhimu kwani lina vitamini muhimu kwa ngozi" Vilevile mwalimu huyu ametoa wito kwa serikali kulibeba suala hili mgongoni kama ilivyoweza kulibeba suala la malaria na gonjwa la ukimwi katika mapambano.

"Naishukuru jamii ya watanzania inayoonekana kubadilika kwa kasi kifikra zamani sisi hatukupewa nafasi katika jamii zilizotuzunguka, tulitengwa kielimu hata pale tulipoonekana kufanya vizuri nafasi hatukupewa, lakini sasa jamii inashituka na kutupa majukumu"

Rais wa Under The Same Sun Peter Ash, kwa mara ya kwanza alitambulisha kwa watoto mchezo wa magongo (Hockey game) ambapo pamoja na kuwafundisha jinsi ya uchezaji pia alikabidhi vifaa vya uchezaji mchezo huo.

Fun ....Oh yeah....!!!!

Mchezo ukiwa umekolea bin kunoga, pale kati namwona rais wa Under The Same Sun (Peter Ash) na  mkurugenzi wa shirika hilo nchini dada Vick Mketema, wakijumuika mchezoni....
HABARI KAMILI..>>>

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira Dk. Terezya Huvisa Akutana na Balozi wa Brazil Nchini Tanzania

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira Dk. Terezya Huvisa. Akizungumza na Balozi wa Brazil, Nchini Tanzania, Comoro na Seychelles Bw. Francisco Carlos Joares Luz. Mazungumzo hayo yalihusu maandalizi ya Mkutano wa Kimataifa wa Rio +20. yalifanyika Mtaa wa Luthuli, Dar es Salaam.Picha na Ali Meja.
HABARI KAMILI..>>>

MAMA ASHA BILAL MGENI RASMI MAADHIMISHO YA MIAKA MIWILI YA TAASISI YA TUSHIKAMANE PAMOJA FOUNDATION

Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, akimkabidhi zawadi ya ua mmoja wa wanachama wa Taasisi ya Tushikamane Pamoja Foundation’, Joha Simba, wakati wa hafla ya maadhimisho ya kusherehekea kutimiza miaka miwili ya Taasisi hiyo, iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Diambond Jubilee, jana Me i 20, 2012. 
Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, akimkabidhi zawadi ya ua mwananmitindo maarufu, Mustafa Hassanali, wakati wa hafla ya maadhimisho ya kusherehekea kutimiza miaka miwili ya Taasisi ya Tushikamane Pamoja Foundation, iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Diambond Jubilee, jana Mei 20, 2012.
Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, akisoma hotuba yake wakati wa hafla ya maadhimisho ya kusherehekea kutimiza miaka miwili ya Taasisi ya Tushikamane Pamoja Foundation, iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Diambond Jubilee, jana Mei 20, 2012.
Mke wa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mama Margareth Samue Sitta, akipita jukwaani na vazi la asili kwa mikogo, wakati wa hafla ya maadhimisho ya kusherehekea kutimiza miaka miwili ya Taasisi ya Tushikamane Pamoja Foundation, iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Diambond Jubilee, jana Mei 20, 2012.
Mchezaji wa mpira wa Kikapu, Hasheem Thabeet, akipita jukwaani na vazi la asili kwa mikogo, wakati wa hafla ya maadhimisho ya kusherehekea kutimiza miaka miwili ya Taasisi ya Tushikamane Pamoja Foundation, iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Diambond Jubilee, jana Mei 20, 2012.
MBunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Shy-Rose Bhanji, akipita jukwaani na vazi la Harusi kwa mikogo, wakati wa hafla ya maadhimisho ya kusherehekea kutimiza miaka miwili ya Taasisi ya Tushikamane Pamoja Foundation, iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Diambond Jubilee, jana Mei 20, 2012.
Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Mwanamitindo,Flaviana Matata
HABARI KAMILI..>>>

KAJALA ADAAI TALAKA MAHAKAMANI


STAA wa filamu za Kibongo, Kajala Masanja amewaacha midomo wazi marafiki zake waliomtembelea katika Gereza la Segerea, Dar es Salaam hivi karibuni baada ya kufunguka kuwa, anataka talaka yake kutoka kwa mumewe Faraji Agustino.

Chanzo cha kuaminikakilichokuwa miongoni mwa mashosti zake waliofika gerezani kumtembelea mwishoni mwa wiki iliyopita kilitonya kuwa, wakiwa hapo Kajala alidai akifanikiwa kushinda kesi inayomkabili hatahitaji tena kurudi kwa mumewe huyo ambaye wameshitakiwa pamoja.

“Mwenyewe alieleza kuwa, ndoa ndiyo iliyomfikisha hapo alipo kiasi kwamba anajuta kuolewa, akasema bora apewe talaka yake.

“Tulijaribu kumsihi asiwe na mawazo hayo kwa kuwa kila kinachotokea ni mipango ya Mungu lakini alionekana kushupalia hilo la talaka akidai isingekuwa kuolewa na mwanaume huyo, sasa hivi angekuwa anakula bata mtaani,” alidai mtoa habari huyo. 

Kilieleza kuwa, siku hiyo Kajala aliwatoa watu machozi baada ya kueleza kuwa, ndoa yake imemuingiza kwenye matatizo ambayo yamemfanya ashindwe kwenda kushuhudia mazishi ya Kanumba, msanii aliyemfanya asimame kwenye filamu.

Kajala na mumewe wanaendelea kusota kwenye Gereza la Segerea wakikabiliwa na kesi ya kutakatisha fedha haramu.

SOURCE: GP
HABARI KAMILI..>>>

MIMBA YA LULU MICHAEL YATOKA

 
ULE ujauzito wa miezi mitatu wa mwigizaji nyota wa sinema Bongo ambaye kwa sasa yuko nyuma ya nondo za Gereza la Segerea, Dar es Salaam kwa kesi ya kifo cha Steven Kanumba, Elizabeth Michael 'Lulu' umedaiwa kuchoropoka
 
Kwa mujibu wa chanzo cha uhakika ambacho ni makini, sababu kubwa ya mimba hiyo kutoka ni kutunga nje ya mfuko wa uzazi hali ambayo ingemletea matatizo Lulu.

“Nikwambie kitu, unajua wengi wanaamini Lulu ana mimba na hivi karibuini iliandikwa imefikisha miezi mitatu, ilikuwa sahihi, lakini ukweli ni kwamba kwa sasa imetoka.

“Sababu kubwa ni kwamba afya yake ilidorora, ukiachia ule ugonjwa wa U.T.I alioripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari kwamba anao, lakini kingine ni kuwa iligundulika ujazuito wake ulitunga nje ya mfuko wa uzazi ikawa haina jinsi, ikabidi kutolewa na kusafishwa,” kilisema chanzo hicho bila kuainisha tukio hilo lilitokea lini.

Kikiendelea kuzungumza kwa umakini mkubwa, chanzo chetu kilidai kuwa eti ujauzito huo ni wa tatu kuchoropoka kwa msanii huyo.

“Unajua huu unakuwa ujauzito wa tatu kwa Lulu kutoka. Kwa kweli kama si hivyo angekuwa na mtoto,” kilisema chanzo bila kuweka wazi nyingine mbili zilitoka kwa matatizo gani. 

“Kuna wakati Lulu alikwenda China, aliporudi alikuwa na ujauzito, lakini nao ulitoka, inaonekana ana matatizo kidogo kwenye upande wa kizazi,” kilidai chanzo hicho.

Kikaendelea: “Baada ya hapo, haukupita muda mrefu, akanasa nyingine ya mwanamuziki mmoja wa Bongo Fleva, pia hiyo nayo ikaja kutoka ya tatu ni hii ya Kanumba.”

SOURCE: Global Publisher
HABARI KAMILI..>>>

PENZI LA DIAMOND NA JOKATE LAINGIA DOSARI BAADA YA DIAMOND KUNASWA AKIWA NA AUNT EZEKIEL


KITENDO cha hivi karibuni cha mwanamuziki Naseeb Abdul ‘Diamond’ kunaswa hotelini na staa wa filamu za Kitanzania, Aunt Ezekiel, kumetibua mambo na sasa inadaiwa uhusiano wa kimapenzi wa kidume huyo na mwanamitindo Jokate Mwegelo umeingia mdudu mbaya.

Chanzo cha kuaminika kimedai kuwa tangu kuzagaa kwa habari za Aunt na Diamond kubambwa katika Hoteli ya Kebby’s iliyopo Mwenge, Dar wakila ‘good time’, Jokate anadaiwa kumaindi na kumnunia mwanamuziki huyo kiwango.

“Kwa kifupi Diamond na Jokate kimeshanuka. Jokate tangu asikie tetesi hizo kisha kusoma kwenye gazeti, hapokei simu za mpenzi wake huyo. Diamond atakuwa na kazi ya kumbembeleza ili kumrudisha kwenye hali ya kawaida,” kilidai chanzo hicho.

Katika kutafuta mzani wa habari hiyo, waandishi wetu  walifanya jitihada za kuwatafuta wahusika na Diamond alipopatikana alifunguka nusunusu:

“Aaah!Hakuna kitu kama hicho bwana (anacheka), mbona mambo yako sawa tu, ila sasa hivi simu yangu inasumbua, nitafute baadaye nitakupa ukweli.”

Hata hivyo, alipotafutwa baadaye aliendelea kuchenga kutoa ufafanuzi juu ya suala hilo, mazingira yaliyoashiria kuna kitu ambacho hakupenda jamii ikijue kwa sasa.

Baada ya Diamond kuchenga kuzungumzia uhusiano wake ulivyo kwa sasa, Jokate kwa upande wake alionesha kuwa na kitu moyoni na mahojiano kati yake na mwandishi wetu yalikuwa hivi;

Mwandishi: Mambo Jokate?
Jokate: Safi za siku?
Mwandishi: Ni nzuri tu, vipi hali yako zaidi?
Jokate: Mimi niko poa. 

Mwandishi: Kuna habari tumezinasa kuwa sasa hivi huongei na mpenzi wako Diamond kisa kunaswa na Aunt, ni kweli?
Jokate: Hahaaa… duh.. bwanaa! Mimi sitaki.
Mwandishi: Hutaki nini sasa?

Jokate: Sitaki tu udaku.
Mwandishi: Siyo udaku ila nimekuuliza swali, unatakiwa ujibu, unaongeleaje sakata hilo kwa jumla?
Jokate: Sawa tu! 

Mwandishi: Sawa nini au unamaniisha sawa umemnunia Diamond na Aunt?

Jokate: Mimi sitaki kuongelea hilo kwa sasa, naingia kanisani.
Mwandishi: Kabla hujaingia kanisani naomba unipe majibu ya kuridhisha.

Jokate: Bwana nitafute baadaye, sasa hivi naingia kanisani… Mara simu ikakatika na alipopigiwa tena hakupokea.

Baada ya dakika 20, mwanadada huyo anayefanya freshi kwenye mambo ya umodo alituma ujumbe mfupi ‘sms’ kwenye simu ya mwandishi ukisomeka; “Diamond ni mtu mzima mwenye akili zake, ana maamuzi yake. So please (Tafadhali sana) naomba msinitoe mtanikwaza kiukweli na sipendi kukwazika, naomba uheshimu hilo.”

Hivi karibuni Diamond aliamua kufunguka kuwa na uhusiano na Jokate lakini juzikati zikaibuka habari za mwanamuziki huyo kunaswa na Aunt hotelini, mazingira yaliyosababisha kuchafuka kwa hali ya hewa kati yao.

source: GP
HABARI KAMILI..>>>

MIAKA 16 YA KUMBUKUMBU YA WALIOKUFA KATIKA AJALI YA MELI YA MV. BUKOBA


Hili ni eneo la makaburi ya baadhi ya watu waliofariki katika ajali ya meli ya MV Bukoba iliyozama Mei 21, 1996 ambayo ni miaka 16 iliyopita katika Ziwa Victoria ikitokea mkoani Kagera kuelekea Mwanza. Inakadiriwa kuwa watu zaidi ya 800 walipoteza maisha katika ajali hiyo.
HABARI KAMILI..>>>

Mjadala wa Mabadiliko ya Tabia nchi Afrika Unaendelea Mjimni Donn Ujerumani

 Bw. Theodore Silinge Kulia Afisa misitu mkuu kutoka wizara ya nishati na madini, na Evelyn mkokoi  Afisa habari ofisi ya makamu wa rais,wakifuatilia majadiliano ya mjadala wa mabadiliko ya Tabia nchi katika kundi la nchi za Afrika kwenye mkutano wa mabadiliko ya Tabia nchi unaoendelea mjini Bonn Ujerumani.Picha na Evelyn Mkokoi-Afisa Habari Ofisi ya Makamu wa Rais
HABARI KAMILI..>>>

LETICIA NYERERE KUSHITAKI WALIOMKASHIFU


MBUNGE wa Viti Maalum, Leticia Nyerere (CHADEMA), ametishia kuwashitaki watu waliotoa taarifa katika vyombo vya habari, zikidai kuwa alikuwa amekamatwa na polisi kuhusiana na makosa aliyotenda nchini Marekani. 

Katika taarifa yake jana kwa vyombo vya habari, Leticia alieleza kusikitishwa kwake na taarifa hizo, akidai kuwa zimemdhalilisha na kumkashifu mbele ya jamii inayomheshimu na kumthamini, na hivyo atachukua hatua za kusafisha jina lake. 

Alisema tuhuma hizo zilizosambazwa katika moja ya mitandao hapa nchini na kunukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari, Mei 14, mwaka huu, zilikuwa za kutungwa, na zilizolenga kumchafua mbele ya Watanzania waishio Marekani na hapa nchini. 

Mbunge huyo alisema tayari ametoa taarifa kwa mamlaka za kisheria nchini Marekani, na tayari uchunguzi utaanza kuwanasa wale wote waliohusika kusambaza uzushi huo. 

Mei 14, mwaka huu, mtu aliyejitambulisha kama Amos Cherehani, akidai kuwa Katibu wa CHADEMA, tawi la Marekani, alisambaza taarifa za kukamatwa kwa mbunge huyo jijini Washington DC, kwa tuhuma za kutenda makosa mawili ya jinai, likiwemo la kujipatia kadi ya kijani (Green Card) kwa njia ya udanganyifu. 

Aidha, Cherehani ambaye alikuwa akiwaomba Watanzania kumchangia mbunge huyo fedha za kukabiliana na kesi hiyo, alisema anatuhumiwa kufanya kosa la kuvunja masharti ya dhamana, kwa kutofika mahakamani hapo Februari 10, mwaka huu, katika kile kilichosemwa ni kesi ya kutapeli dola 15,000 toka kwa mtu aliyetajwa kama dada Cooper. 

Hata hivyo, taarifa hizo zilikanushwa vikali na Leticia mwenyewe, na baadhi ya viongozi waandamizi wa CHADEMA, ambao walimtaka atoe maelezo ya kujisafisha kwa Watanzania. 

Wakati huo huo, mbunge huyo, amesema kuwa, uzinduzi wa tawi la CHADEMA katika mji wa Maryland nchini Marekani, utafanyika Mei 27. 

Chanzo: Tanzania Daima
HABARI KAMILI..>>>

FAINALI ZA KOMBE ZA MAGIC SITE IRINGA

ZAWADI YA KOMBE
KAPTENI WA TIMU YA MASHINE TATU AKIPOKEA KOMBE LA MSHINDI WA KWANZA
KAPTENI WA TIMU YA VIZIWI AKIPOKEA ZAWADI
KAPTENI WA TIMU YA ZIZI LA NGO'MBE AKIPOKEA KOMBE LA MSHINDI WA PILI
MDHAMINI WA MASHINDANO YA MKWAWA MAGIC SITE NGD STEVEN NYANDONGO
HABARI KAMILI..>>>

MCHUNGAJI WA KANISA LA BAPTISTI DODOMA AFUKUZWA KWA UZINZI


MCHUNGAJI wa Kanisa la Baptisti la Makole katika Manispaa ya Dodoma, John Mwangafike ambaye pia ni Katibu wa Kanisa hilo Tanzania, amefukuzwa katika kazi hiyo ya kumtumikia Mungu kutokana na kile kilichoelezwa kuwa ni kukiuka kwake kwa makusudi maadili ya kichungaji. 

Barua hiyo ambayo ilitiwa saini na Katibu wa Kanisa hilo, Daniel Njonde na Mzee Kiongozi wa Kanisa hilo Simon Marivey Pia ilimtaka Mchungaji huyo kukabidhi mali zote za Kanisa kufikia jana saa nne asubuhi.  “Aidha Kanisa katika kikao cha Jumuiya ndogo ya Dodoma ya Aprili 15, mwaka huu, iliridhia wewe kufukuzwa katika huduma ya kichungaji hapa Kanisa la Kibatisti Makole,” ilisema sehemu ya barua hiyo.

Awali, habari kutoka ndani ya Kanisa hilo zinasema kuwa, Askofu na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kanisa la Baptisti mkoani hapa, Emmanuel Mwakandulu alisaini barua ya waumini na wazee wa Kanisa hilo, waliotaka Mchungaji huyo asimamishwe kwa tuhuma za kuzaa na waumini, akiwemo msichana wake wa kazi na mwanamke mmoja ambaye ni mke wa mtu ambaye licha ya kuwa na mtoto moja naye, sasa ni mjamzito.

Kusimamishwa kwa mchungaji huyo kuliridhiwa na washirika 47 na wazee wa Kanisa hilo. Kulingana na tuhuma za mchungaji huyo, waumini na viongozi walitaka mchungaji huyo aondolewe kwenye huduma baada ya kukaidi kujiuzulu alipotakiwa kufanya hivyo. Hatua ya kumtimua kiongozi huyo imefanyika kulingana na Imani ya Kibaptisti na Katiba ya Kanisa hilo kifungu Na. 24(9), 27(C) na (F) (10) vinavyozungumzia ukosefu wa maadili.

Aidha, anatajwa kuzaa watoto watatu na mfanyakazi wa ndani ambaye hata hivyo jina lake linahifadhiwa na kuzaa mtoto mmoja mmoja na waumini wake wawili. Inaelezwa katika kikao hicho na wajumbe waliofika kwake, alikanusha kuwa na watoto nje ya ndoa, akisema wanaomwita baba ni `watoto wa kiroho’.

Aidha, inaelezwa Mchungaji huyo alikiri kusafirisha kwa jina la Kanisa chakula kwenda Malawi, akisema waumini wa Kanisa hilo nchini humo wako katika njaa, ingawa hakikuwafikia.
HABARI KAMILI..>>>

MWENYEKITI WA YANGA NDUGU LYOD NCHUNGA ATIMULIWA

Mwenyekiti wa Kamati ya Wazee wa Klabu ya Yanga, Ibrahim Akilimali akitangaza kumfuta Uenyekiti wa timu hiyo, Lyod Nchunga, baada ya kutimiza kolamu  ya wanachama mia tano na hamsini na sita na wajumbe nane kujiuzuru rasmi
wakati wa mkutano wa wanachamauliofanyika kwenye klabu hiyo, Mtaa wa Jangwani naTwiga jijini Dar es Salaam.

Wanachama wa Yanga wakishangilia tamko la kumg'oa Mwenyekiti wa Klabu hiyo Lyod Nchunga
 Mashabiki wa Yanga ambao si wanachama, wakifuatilia mkutano wakiwa mbali

 Mmoja wa wanachama wa Yanga, anayeitwa Nyachia akionyesha kadi yake wakati wa kujisajili kuingia kwenye mkutano huo.  Fuatilia katika Blogu hii baadaye tunapandisha Video ya sehemu ya mkutano huo.
Tofauti na vikao vingine vya Yanga ambavyo hufanyika katika ukumbi wa  jengo la Klabu hiyo
HABARI KAMILI..>>>

HARUNA MOSHI ASHIRIKI MAZISHI YA SWAHIBA WAKE MAFISANGO

Haruna Moshi Boban  wa pili kutoka kushoto na Mussa Hassan Mgosi wa kwanza kushoto wakizungumza na wenyeji wao wakati wa mazishi ya aliyekuwa mchezji wa timu ya Simba marehemu Patrick Mutesa Mafisango leo  huko Lemba, Kinshasa DRC Congo Fullshangwe imeshuhudia tukio hilo na itakuwa ikikumuvuzishia kadiri matukio yatakavyokuwa yakiingia..
Waombolezaji wamejitokeza kwa wingi sana katika mazishi ya Mafisango huko Lemba nje kidogo ya jiji la Kinshasa.
Waombolezaji wakiwa katika mstari tayari kwa kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Patrick Mafisango.
HABARI KAMILI..>>>