Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Sunday, July 3, 2022

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo July 3

Read More

Friday, July 1, 2022

Kesi Waliyoifungua Akina Halima Mdee Kutolewa Uamuzi Julai 6


Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imepanga kutoa uamuzi wa maombi ya Mbunge wa viti maalum wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Halima Mdee na wenzake 18 kuomba kibali cha mahakama kufanya mapitio ya kimahakama kupinga kuvuliwa uanachama wa chama hicho.

Halima Mdee na wenzake wamewasilisha ombi hilo wakiwa na hoja tano za kisheria ikiwemo, kufungua maombi hayo ndani ya muda wa kisheria na kuonesha maslahi yao mapana kwa Chadema na kama Wabunge wametafuta haki zao ndani ya chama hicho hadi ngazi ya juu.

Akiwasilisha hoja hizo, mmoja wa mawakili wa wabunge hao Ipilinga Panya amedai waliopeleka kuwa waliopeleka maombi wote kumi na sita wanamaslahi katika jambo hilo kwani wamekuwa waathirika wa maamuzi ya Bodi ya Wadhamini ya chama hicho kupitia uamuzi wa Baraza kuu la CHADEMA lililofanyika Mei11 mwaka huu na kufukuzwa uanachama.

Pia amedai kuwa waliopeleka maombi wote ni Wabunge wa viti maalum wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania walioteuliwa na Bodi ya Chama hicho mwaka 2020/2025 hivyo maamuzi ya kuwafukuza uanachama bila kufuata utaratibu wa kuwasikiliza kunagusa maslahi yao binafsi kama wanachama wa chama cha siasa na wabunge wa Bunge la Tanzania.

Wakili mwingine wa wabunge hao EBSON KILATU amedai kitendo cha baraza hilo kuwafukuza uanachama hawakuzingatia haki wakati wa utoaji maamuzi hayo.

Akijibu hoja hizo kwa niaba ya Baraza la Wadhamini la CHADEMA Wakili Peter Kibatala amedai hawapingi hoja ya wabunge hao kuwa na maslahi mapana ila kigezo cha mgogoro huo kuwepo Ushahidi mahakamani ili ichunguze huo Ushahidi wao na mahakama ijiridhishe na kutoa uamuzi.

Amedai mahakama hiyo haiwezi kuwapa nafuu ianazoomba walioleta maombi kwa sababu wamewasilisha maombi hayo nje ya muda.

Kesi hiyo imeahirishwa mpaka Julai 6 mwaka huu itakapotolewa uamuzi.

Read More

Uwekaji Vigingi Pori La Loliondo Hautoathiri Maendeleo Ya Wananchi-Majaliwa


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema zoezi la uwekaji wa vigingi katika eneo la kilometa za mraba 1,500 la Pori Tengefu la Poloreti-Loliondo ambalo limekamilika kwa asilimia 100 halitoathiri maendeleo ya wakazi waishio kwenye eneo la vijiji 14 vinavyopakana na eneo hilo.

Hata hivyo, Mheshimiwa Majaliwa amesisitiza kwamba hakutakuwepo na kijiji chochote kitakachofutwa na hakuna miundombinu itakayoondolewa kwa kuwa ndani ya eneo la kilometa za mraba 1,500 hakuna miundombinu yoyote.

Ameyasema hayo jana(Alhamisi, Juni 30, 2022) wakati akitoa Hoja ya Kuahirisha Mkutano wa Saba wa Bunge la 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bungeni jijini Dodoma. Amesema    Serikali imesimamia kwa umakini mkubwa zoezi la uwekaji vigingi kwenye hilo ambalo ni muhimu kwa ikolojia ya Hifadhi ya Serengeti na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro.

Mheshimiwa Masema Serikali imeendelea kushirikiana na wananchi wa Loliondo katika kuboresha malisho ya mifugo, uchimbaji wa visima vya maji, ujenzi wa majosho pamoja na miundombinu ya kunyweshea mifugo kwenye eneo la kilometa za mraba 2,500. 

“Pia, ninaielekeza Wizara ya Maliasili na Utalii kushirikiana na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi pamoja na wadau wengine kuhakikisha kuwa Sheria ya Ardhi ya vijiji namba 5 ya mwaka 1999 inatumika ipasavyo kutenga na kuweka mipaka ya vijiji.”

Amesema  Serikali kwa kuzingatia matakwa ya wananchi hasa maeneo ya malisho kwenye vijiji 14 vilivyopo karibu na Pori Tengefu la Poloreti itaweka utaratibu utakaopangwa kwa pamoja baada ya kukamilisha zoezi la utambuzi wa mifugo kwenye vijiji husika.

Mheshimiwa Majaliwa amesema katika kuhakikisha uwepo wa matumizi endelevu ya Pori Tengefu la Poloreti, Serikali ilielekeza eneo la kilometa za mraba 1,500 lihifadhiwe na eneo lililobaki la kilometa za mrada 2,500 wananchi waendelee kulitumia kwa shughuli nyingine.

Akizungumzia kuhusu zoezi la wakazi wa Ngorongoro kuhama kwa hiari katika eneo kwa ajili ya kupisha uhifadhi endelevu, Waziri Mkuu amesema kumekuwa na mafanikio makubwa katika kusimamia utekelezaji wa zoezi hilo hadi kufikia tarehe 09 Juni 2022, jumla ya kaya 293 zenye watu 1,497 zimejiandikisha. “Serikali imeendelea kuhamasisha na kuandikisha zile kaya ambazo zipo tayari kuhama kwa hiari.”

“Upendo huo uliooneshwa na Mheshimiwa Samia, Rais wetu hauna budi kupongezwa na kila mwenye kuitakia mema nchi hii. Hata hivyo, utaratibu huu ni maalum kwa Ngorongoro pekee. Leo tarehe 30 Juni, 2022 kaya nyingine 25 zenye jumla ya watu 115 zinatarajiwa kusafiri kwa hiari kuelekea Msomera na kuendelea na maisha yao kama kawaida.” 

Wakati huo huo, Waziri Mkuu ameiagiza Wizara ya Maliasili na Utalii isianze zoezi upandishwaji hadhi wa maeneo ya mapori tengefu kuwa mapori ya akiba hilo hadi wananchi watoe maoni yao kwa maslahi ya pande zote.

“Niwahakikishie wananchi wa maeneo husika kwamba utaratibu wa kupandisha hadhi maeneo ya mapori hayo kuwa mapori ya akiba utasubiri mapitio ya pamoja kati ya Serikali na wananchi. Tathmini hiyo na ushirikishwaji wa wananchi husaidia Serikali kufanya maamuzi ya iwapo kuendelea na utaratibu wa kupandisha hadhi au la Hivyo, Wizara isianze zoezi hilo hadi wananchi watoe maoni yao kwa maslahi ya pande zote.”

Amesema rasilimali za wanyamapori ni muhimu kwa maendeleo ya nchi, hususan katika kukuza utalii na hivyo kuongeza pato la Taifa. “Kwa msingi huo, mpango wa Serikali kupandisha hadhi baadhi ya mapori tengefu kuwa mapori ya akiba ni katika kuimarisha ulinzi wa rasilimali zilizopo katika mapori hayo kwa uhifadhi endelevu.” 

Hata hivyo,  Waziri Mkuu amesema utaratibu wa kutangazwa kwa eneo  lolote kuwa Pori la Akiba hufanywa na Mheshimiwa Rais kwa kufuata taratibu zilizowekwa kisheria ikiwemo kufanya tathmini ya kina ya umuhimu wa eneo husika katika uhifadhi na ushirikishwaji wa wananchi kupitia Mamlaka za Serikali za Mitaa za maeneo husika.


Read More

Jenerali Venance Mabeyo Ateuliwa Mwenyekiti Wa Bodi Ya Ngorongoro (Ncaa)

Read More

Utendaji Wa Wakurugenzi Na Wakuu Wa Idara Kupimwa-Majaliwa


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali inakusudia kupima utendaji wa Wakurugenzi na Wakuu wa Idara kwa kutumia viashiria muhimu hususan usimamizi wa mapato na makusanyo ya ndani pamoja na upelekaji wa fedha kwenye miradi ya maendeleo.

Amesema watendaji hao pia watapimwa  kwa namna wanavyosimamia mikopo ya asilimia 10 ikiwa ni pamoja na marejesho, usimamizi wa miradi ya maendeleo na uzuiaji na utekelezaji wa hoja za ukaguzi zinazoibuliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

Ameyasema hayo jana (Alhamisi, Juni 30, 2022) wakati akitoa Hoja ya Kuahirisha Mkutano wa Saba wa Bunge la 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bungeni jijini Dodoma. Amesema hatua hiyo ni katika kuhakikisha dhamira nzuri ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan inayojiakisi kwenye Mpango na Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2022/2023 inafikiwa.

Mheshimiwa Majaliwa amesema Serikali imejipanga vema kuendelea kusimamia suala la uwajibikaji katika utumishi wa umma kwa kuweka mikakati mbalimbali. “Mikakati ipo katika kuimarisha uwajibikaji hususan kwenye Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ni pamoja na kupima utendaji wa utendaji wa Wakurugenzi na Wakuu wa Idara.”

Amesema mkakati mwingine ni kongeza bajeti ya matumizi mengineyo katika Ofisi za Wakuu wa Mikoa na Wilaya kutoka shilingi bilioni 57.44 hadi shilingi bilioni 79.09 ili kuwezesha utekelezaji wa majukumu ya ofisi hizo.

“Sambamba na ongezeko hilo la Bajeti katika mwaka 2022/2023, Serikali pia, imehuisha muundo wa Sekretarieti za Mikoa kwa kuboresha iliyokuwa Sehemu ya Usimamizi wa Serikali za Mitaa na kuwa Sehemu ya Menejimenti, Ufuatiliaji na Ukaguzi ili kuimarisha ufuatiliaji wa mapato, matumizi na utekelezaji wa miradi katika Mamlaka za Serikali za Mitaa.”

Amesema Serikali itaendelea kuwajengea uwezo Madiwani, Mafisa Tarafa na Watendaji wa Kata kupitia Programu ya Uimarishaji Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa lengo la kuongeza uelewa wa majukumu yao kisheria, kuimarisha mahusiano yao na viongozi wa kisiasa na kusimamia ipasavyo miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwenye maeneo yao pamoja na ukusanyaji wa mapato.

Waziri Mkuu amesema Serikali inaendelea kujenga mifumo na miundo wezeshi katika eneo la ufuatiliaji na tathmini ili kuboresha utendaji kazi unaojali matokeo. “Eneo hili linahitaji uwepo wa mifumo na miundo imara ambayo itawezesha kujenga msingi thabiti wa usimamizi wa utendaji kazi wa Serikali.”

Amesema hatua hizo zinajumuisha kupitia upya miundo na majukumu ya Wizara, Idara zinazojitegemea, Wakala za Serikali, Mashirika ya Umma, Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa katika eneo la ufuatiliaji na tathmini ili kuziimarisha pamoja na kujenga uwezo wa watumishi katika eneo hilo.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amesema Serikali imeanza maandalizi ya Sera ya Ufuatiliaji na Tathmini kwa kuzihusisha taasisi simamizi zinazohusika na ufuatiliaji na tathmini ili kuchambua maeneo wanayosimamia na kuhakikisha maeneo yote muhimu yanajumuishwa ikiwemo usimamizi wa mipango ya maendeleo na utendaji wa Serikali kwa ujumla. 

“Sambamba na hatua hizo, tayari, Serikali imekamilisha Mfumo wa Kitaifa wa Usimamizi wa Miradi ya Maendeleo ambao utaanza kutumika Julai, 2022. Mfumo huo, pamoja na mambo mengine utasaidia Serikali kuimarisha ufuatiliaji na tathmini katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo na hivyo kuongeza tija na thamani ya matumizi ya fedha za umma kwenye miradi husika.”

Vilevile, Waziri Mkuu amesema Serikali imehuisha Muundo na Mgawanyo wa Majukumu wa  Ofisi ya Waziri Mkuu hususan kwa upande wa Sera, Uratibu na Bunge ili kuimarisha jukumu la ufuatiliaji na tathmini. “Lengo ni kuhakikisha taarifa za ufuatiliaji na tathmini kutoka katika wizara na taasisi za Serikali zinafanyiwa uchambuzi wa kina pamoja na kutoa mrejesho kuhusu utendaji wa Serikali.”

Waziri Mkuu ametoa wito kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kushirikiana na Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Ofisi ya Waziri Mkuu na Wizara ya Fedha na Mipango kufanyia kazi changamoto ya uhaba wa wataalamu wa ufuatiliaji na tathmini; kazi za tathmini kufanyika kwa ufanisi na uwepo wa mifumo mingi ya ukusanyaji wa taarifa yenye kuathiri ubora wa takwimu.

Amesema Serikali itaendelea kufanya tathmini ya ujuzi unaohitajika, kufanya tathmini ya mifumo ya ufuatiliaji na tathmini iliyopo kwenye taasisi za Serikali, kuandaa Kanzi-Data ya Watumishi wenye utaalamu wa masuala ya ufuatiliaji na tathmini, kuongeza matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kwenye ufuatiliaji na tathmini na kuimarisha vitengo vya ufuatiliaji na tathmini ili kujenga mfumo jumuishi wa ufuatiliaji na tathmini ambao utawezesha kufuatilia, kuchambua na kupata taarifa halisi na kwa wakati za utendaji wa Serikali.

Read More

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo July 1

Read More

Thursday, June 30, 2022

Rais Samia Afanya Uteuzi wa Mkuu Mpya wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania (CDF)

Rais Samia Suluhu Hassan amempandisha cheo Meja Jenerali Jacob John Mkunda kuwa Jenerali na amem
teua kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (Chief

lass="separator" style="clear: both;">
of Defence Forces – CDF).

Kabla ya Uteuzi huo alikuwa Mkuu wa Tawi la Operesheni na Mafunzo katika Makao Makuu ya Jeshi (Chief of Operations and Training).

Rais Samia pia amempandisha Cheo Meja Jenerali Salum Haji Othman kuwa Luteni Jenerali na amemteua kuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (Chief of Staff – C of S).

Kabla ya uteuzi huo Meja Jenerali Othman alikuwa Kamishna wa Utafiti na Maendeleo Jeshini (Commissioner for Research and Military Development) katika Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.

Kabla ya uteuzi huo Meja Jenerali Othman alikuwa Kamishna wa Utafiti na Maendeleo Jeshini (Commissioner for Research and Military Development) katika Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.

Read More

Jeshi la Sudan lashambulia eneo linalozozaniwa katika mpaka na Ethiopia


Majeshi ya Sudan yalifyatua mizinga mikubwa wakati wa mapigano katika eneo la mashariki linalozozaniwa la al-Fashaqa linalopakana na Ethiopia.

Hayo yamedokezwa na afisa wa Ethiopia huku kukiwa na wasiwasi wa kuibuka tena mvutano baina ya nchi hizo mbili kuhusu  mzozo wa muda mrefu katika eneo hilo la mpaka wa pamoja.

Jumanne Sudan iliweza kuteka eneo la Jabal Kala al-Laban, lililo karibu na mpaka unaozozaniwa, kufuatia shambulio la anga, kwa mujibu wa afisa wa  kijeshi wa Sudan ambaye hakutajwa jina akizungumza na shirika la habari la Reuters.

Siku ya Jumatatu, Ethiopia ilikanusha shutuma za Sudan kwamba jeshi lake lilikamata na kuwanyonga wanajeshi saba wa Sudan na raia mmoja, badala yake ikasema mauaji hayo yametekelezwa na wanamgambo wa eneo hilo.

Duru za serikali ya Sudan zilisema kuwa Sudan imewasilisha malalamiko rasmi kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu mauaji hayo.

Jeshi la Sudan lilifyatua mizinga ya masafa marefu kuanzia Jumatatu asubuhi hadi Jumanne alasiri, lakini hakuna aliyejeruhiwa, alisema Assefa Ashege, afisa mkuu wa usalama katika eneo la Amhara nchini Ethiopia.

Wakaazi wawili wa eneo hilo walisema kuwa jeshi la Sudan limechukua udhibiti wa eneo la Jabal Kala al-Laban.

Mzozo kuhusu al-Fashaqa, ambayo ipo ndani ya mipaka ya kimataifa ya Sudan lakini imekaliwa na wakulima wa Ethiopia kwa miongo kadhaa, umeongezeka katika miaka ya hivi karibuni sambamba na mzozo wa kidiplomasia kuhusu ujenzi wa Ethiopia wa bwawa la kufua umeme wa maji.

Read More

Rais Samia Afanya Uteuzi wa Viongozi Mbalimbali

Read More

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo June 30

Read More
End: