Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Monday, May 5, 2014

Picha za mazishi ya sheikh Ilunga Hassan Kapungu aliyefariki dunia usiku wa kuamkia leo.....Mazishi yake yalikuwa ni ya kihistoria, mchanga wa kaburi umefukiwa kwa mikono badala ya jembe


 Maalim Seif akishiriki katika mazishi ya Sheikh Ilunga Shekh Hassan Kapungu yaliofanyika katika makaburi ya Mwinyimkuu Magomeni Dar es Salaam
 Sheikh Ilunga Shekh Hassan Kapungu enzi za uhai wake
 
 

 Wananchi wakishiriki katika mazishi ya Shekh Ilunga  Hasaan Kapungu katika makaburi ya Magomeni Mwinyimkuu jijini Dar-es-Salaam.(Picha na Salmin Said OMKR)
 ******

Na Hassan Hamad.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, amewaongoza maelfu ya waislamu katika mazishi ya sheikh maarufu wa Mkoa wa Mwanza na mwanaharakati wa dini ya Kiislamu marehemu sheikh Ilunga Hassan Kapungu.

Sheikh Ilunga amefariki dunia  usiku wa kuamkia   leo jijini  Dar es Salaam na kuzikwa katika makaburi ya Mwinyimkuu Magomeni.

Katika uhai wake, sheikh Ilunga Kapungu alikuwa mwanaharakati ambaye mara nyingi alikuwa akiendesha mihadhara ya wazi ya dini ya Kiislamu, ambapo mwishoni mwa mwaka 2013 alikamatwa mkoani Tabora na baadaye kuachiwa huru kwa tuhuma za uchochezi wa dini kupitia kanda za CD na VCD  zilizokuwa zikiuzwa  kwa waumini ili  kueneza  chuki na ukabila ikiwemo kuhimiza kuwachinja mapadri.

Kwa mujibu wa taarifa za kimtandao, kabla ya kukamatwa kwake na kuachiwa huru Disemba mwaka 2013, marehemu sheikh Ilunga alikwenda nchini India kwa matibabu baada ya kusumbuliwa na matatizo ya figo pamoja na sukari.

Akizungumza katika mazishi hayo , sheikh Basaleh wa Dar es Salaam, amesema marehemu sheikh Ilunga alikuwa mwanaharakati imara na ni mfano mzuri wa kuigwa katika harakati za dini ya Kiislamu.

Mazishi yake yameweka historia baada ya maelfu ya waislamu kujitokeza kushiriki, hali iliyopelekea mchanga wa kaburi lake kufukiwa kwa mikono badala ya kutumia mapauro na majembe kama ilivyozoeleka.

Masheikh kutoka Mikoa mbalimbali ya Tanzania wameshiriki mazishi hayo akiwemo sheikh Kishk
chn
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )