Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Sunday, November 12, 2017

Lema ataka wabunge wa CUF ya Lipumba waondolewe Bungeni

adv1
Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amemshauri Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai kutumia busara kuwaondoa bungeni wabunge nane walioingia bungeni kuziba nafasi za wabunge nane waliokuwa wamevuliwa uanachama wa chama cha CUF Julai 24.

Lema ametumia mtandao wake wa kijamii kuandika ujumbe huo ikiwa ni siku moja baada ya Mahakama Kuu kutengua uamuzi wa kufukuzwa kwa Wabunge 8 na Madiwani 2 wa Chama cha Wananch CUF mpaka pale shauri la msingi litakaposikilizwa.

“Mh Spika anapaswa, kuzingatia kwa busara uamuzi uliotolewa na mahakama kwa kuwaondoa wale Wabunge wa Lipumba ndani ya Bunge na kuwarejesha Wabunge halali sasa, Mpaka hapo haki itakaposhinda zaidi,”ameandika Lema

Wabunge hao nane walivuliwa uanachama Julai 24 na Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la Chama cha Wananchi, CUF linaloongozwa na Prof. Lipumba  kwa madai ya utovu wa nidhamu yakiwemo kukisaliti chama hicho.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )