Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, February 15, 2018

Lukuvi Aja na ‘Funguka kwa Waziri’

adv1
Waziri  wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, ameanzisha kampeni maalum ya kusikiliza kero za wananchi kuhusu migogoro ya ardhi, ijulikanayo kama ‘Funguka kwa Waziri.’

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kusikiliza kero za ardhi kwa Kanda ya Pwani katika ofisi za Kanda hiyo jijini Dar es Salaam jana, Lukuvi alisema amemua kuanzisha kampeni hiyo kwa kuzunguka nchi nzima kusikiliza kero za migogoro ya ardhi kutoka kwa wananchi.

Alisema katika kampeni hiyo watakuwa wanaambatana na Naibu Waziri wake, Angelina Mabula, na kwamba wakimaliza katika Kanda ya Pwani, watakwenda katika Kanda ya Kagera.

Mikoa mingine ambayo amesema wamepanga kwenda katika awamu hii ni Kagera na Shinyanga na baada ya hapo kampeni itahamia katika kanda zingine.

“Tunao mpango wa kutembea nchi nzima mimi na Naibu Waziri. Tunajua ziko kero nyingi za mashamba katika maeneo ya vijijini na mijini, kero za mipaka na nyingine, kwa hiyo lengo letu ni kuhakikisha tunatatua kero hizo, ndio maana tumeanzisha mpango huu wa funguka kwa Waziri,” alisema Lukuvi.

Lukuvi alisema pamoja na kuwapo kwa kero za ardhi katika maeneo mengi nchini, Dar es Salaam ndio mkoa unaoongoza kwa kero za viwanja vya mjini, huku wilaya ya Kinondoni eneo la Tegeta likiwa kinara na kufuatiwa na Ubungo katika eneo la Mbezi.

Alisema maeneo hayo yaligawiwa hati nyingi wakati viwanja vilikuwa vichache na kwamba tayari imeundwa idara maalum inayoshughulikia Mbezi na Tegeta na kwamba kero katika maeneo hayo zimedumu kwa muda mrefu.

Alisema kampeni hiyo ya kusikiliza kero ni ya wazi, na wamepanga kwamba endapo kero hizo kwa Kanda ya Pwani hayatamalizika kwa wakati, wataendelea kusikiliza kwa mwaka mzima mpaka pale watakapohakikisha wanazimaliza.

Katika kusikiliza kero hizo jana, Lukuvi pia alikutana na mgogoro wa wasanii wa uchongaji wa vinyago katika eneo la Mwenge ambao wamegawanyika katika makundi mawili yakigombania umiliki katika eneo hilo.Hata hiyo Lukuvi aliahidi kusikiliza tena kero yao kesho kwa kukutanisha pande zote mbili.

adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )