Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Sunday, February 18, 2018

SORRY MADAM -Sehemu ya 96 & 97 (Destination of my enemies)

juu
MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA

Wasiwasi wake alio kuwa nao tayari Shamsa alisha anza kuustukia. Mzee huyo akazidi kukanyaga mafuta hadi akafanikiwa kufika Kibaha. Akkunjaa upande wa pili wa barabara na kuanza kuelekea kilipo kituo cha Polisi
“Huko ndio Dar?”
“Ahaa kuna jamaa ninakwenda kumuona hapo mbele kidogo”
Shamsa akachomoa bastola na kuielekezea kwenye tumbo la mzee huyo, huku akiwa amekazia macho na kama atafanya uzembe hali ya hewa itaharabika.
“Ukilete ujinga nalipasua hili tumbo lako lililo jaa maji”
Shamsa alizungumza huku jasho likimwagika na kumfanya mzee wa watu kusimamisha gari lake, huku mwili mzima ukimtemeka, na haja ndogo ikianza kuichafua suruali yake ya kitambaa aliyo ivaa.

ENDELEA
“Rudisha nyuma gari”
Mzee huyo taratibu akajikuta akirudisha gari lake nyuma kwa amri ya Shamsa aliyo elezwa. Wakaingia tena barabarani na kuendelea na safari yao huku Shamsa akiwa ameielekezea bastola yake kwenye tumbo la mzee huyo.
                                                                                                              ***
    Kikao cha wakuu wa kundi la D. F.E kikamalizika na kutoa maamuzi ya kutuma vijana wenye mafunzo ya kijeshi katika kikosi hicho kuja kumumtafuta mkuu wao huyo anaye sadikika kutekwa.
Eddy macho yakamtoka huku akitazama viongozi hao wakipeana mikono, kupitia laptop hiyo iliyopo kwenye meza ya raisi Godwin.
“Inakuwaje hapa?”
Eddy aliwaza huku akikosa jibu la kuzungumza kabisa. Akatoka katika upande huo wa video na kuanza kufungua faili moja baada ya jingine.  Akakuta faili moja limeandikwa ‘TOP SECREATY’. Akajaribu kulifungua akakutana na namba za siri.

‘Anaweza kutumia namba zipi za siri hiyu mzee?’
Eddy alijiuliza huku akiendelea kuingiza ingiza namba za siri baadhi ambazo alizikumbuka kichwani mwake na zilikuwa zinatumiwa na baba yake huyo. Ila namba zote alizo ziingiza hazikuweza kufanya kazi. Akiwa anawaza ni nini cha kufanya. Pembeni kabisa ya kioo hicho, alama nyekundu ikaanza kuonekana, ikiwaka na kuzima. Akasogeza kimshale cha laptop hiyo na kufungua alama hiyo. Kwa haraka ikaja ramani kubwa iliyo jaa kwenye kioo chake.
“Ni nini hiki?”
Eddy alijiuliza huku akikodolea macho ramani hiyo, ambapo alama hiyo nyekundu iliendelea kujitokeza kwenye lapotop hiyo. Eddy akajaribu kuumiza kichwa chake ili kuweza kufahamu ni nini hicho kinacho waka na kuzima ila hakupata jibu kabisa
                                                                                                              ***
   Rahab akamtazama Raisi Godwin jinsi anavyo hema kwa shida baada ya kumwagia maji baridi na kuzinduka baada ya kuzimia kwa maumivu makali ya kupigwa shoti ya umeme katika sehemu zake za siri.
“Nieleze ni kwani nini uliamua kumuua mume wangu?”
“Sifahamu mimi, kusema kweli sifahamu”
Mzee Godwin alilalama huku machozi yakimwagika. Ubabe, ujanja wote ulizima kama mshumaa unavyo zima.
“Nielekeze D.F.E ni nini na ulikuwa na lengo gani la kuianzisha?”
Swali hilo likamstua sana mzee Godwin na kujikuta akimtole mimacho Rahab ambaye amesimama mbele yake. Kwa maana katika maisha yake anatambua kwamba kikundi hicho ni cha siri sana na si kawaida kwa mtu wa kawaidia kuweza kukifahamu, hata viongozi wengi wa serikali yake hawakijui kikundi chake.
“Nieleze usinitumbulie mimacho”
“D…….D….F.E ni nii kikundi chaa umoja”
“Ni kikundi cha umoja? Hembu zungumza kitua ambacho kinaelekeweka”

Rahab alizungumza huku akiinyanyua suruali ya Mzee Godwin. Akaanza kuingiza kuingiza kiganja cha mkono wa kulia kwenye mfuko mmoja baada ya mwengine. Mfuko wa kwanza hakukuta kitu, ila katika mfuko wa kwanza akakutana na simu, aina ya Iphone 6.
Akaiwasha simu hiyo, kitendo cha kuiwasha simu hiyo kikamfanya mzee Godwin kutabasamu kidogo kwa maana simu yake hiyo imeungwanishwa na mtandao maalumu ambao endapo inapo kuwa hewani basi, wanachama wake kwenye kikundi hicho wote wanafahamu ni wapi alipo mkuu  wao.
   Rahabu akaingiza namba za Agnes ambaye aliweza kumpatia. Akaona si vyema kuzungumza akiwa katika chumba hicho akatoka kabisa ndani ya handaki huku simu akiwa ameiweka sikioni, akisikilizia mziki ambao ni muito wa namba hiyo ya Agnes.
                                                                                                         ***
“Shiii jamani, simu yangu inaita. Raisi ananipigia”
Agnes alizungumza na kuwafanya wezake wote kukaa kimya na kumsikiliza. Agnes akakohoa kidogo kisha akaipokea simu hiyo iliyo anza kuita sekunde kadhaa nyuma zilizo pita.
“Mbona unachelewa kupokea simu wewe”
“Rahab…..!!?”
Agnes alizungumza huku akikaa na kuwafanya Fetty, Halima na Anna kushangaa.
“Ndio, nisikilize, nimemteka huyu fala nipo naye kwenye yale makazi yetu chini ya ardhi”
“Kweli…..?”
“Ndio, nimekuambia wewe kwa maana nahitaji msaada wako”

“Sikia, sikia Rahab. Sasa hivi unakuja huko. Nipo na timu nzima na tulikuwa na mpango wa kuungana nawe kuhakikisha huyo mjinga tunamkomesha na mwanaye”
“Poa kama vipi nyinyi njooni, ila kuweni makini”
“Ahaa makini wapi, siis ni viongozi wa hii nchi bwana au umelisahau hilo”
“Poa fanyeni chap”
Simu ikakatwa, Agnes akawatazama wezake ambao wana shauku ya kutaka kufahamu ni wapi alipo rafiki yao Rahab.
“Yupo kwenye lile handaki letu”
“Kweli?”
“Ndio”
“Kazi imeanza”
Wote kwa pamoja wakatoka ndani, Anna na Fetty wakaingia kwenye gari moja huku Halina na Agnes wakiingia kwenye gari jengine. Safari ikaanza kuelekea nje ya jiji la Dar es Salaam kwenye msitu ambapo ndipo kuna handaki hilo. Kwa jinsi wanavyo ziendesha gari zao kwa mwendo kasi, kila watu walio weza kuziona wliweza kutambua kwamba madereva hao wapo kwenye mashindao

ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )