Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, February 22, 2018

TANGA RAHA- Sehemu ya Kumi na Moja ( 11 )

juu
MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA

   Recho akaongeza sauti ya redio hadi mwisho na kuipunguza haraka haraka na kunitazama usoni.Sikujua na jinsi kwani tayari pombe za mchana zimewachanganya.Recho akaendelea kucheza taarabu nayoimba ‘JAMANI NINA MWAGA RADHI’ huku wengine wakiitikia ‘MWAGAAAA’
Zena akawa anafungua taulo na kulifunaga.Mlango ukagongwa tane nikajua bibi amerudi tena,nikasimama na kwenda kufungua mlango.Moyo ukanistuka baada ya kumkuta ni Mama Fety amesimama huku akihitaji kuingia ndani kwangu

ENDELEA
   Tukatazamana na Mama Fety kwa sekunde kadhaa huku kila mmoja akiwa kimya ikanibidi niuvunje ukimya
“Vipi mbona unakuja bila taarifa?”
“Eddy akuomba unipishe niingie ndani?”
Mama Fatuma alizungumza huku akinisukuma akitaka kupita ndani kwangu kilazima ila hakunishinda nguvu nikamzuia na akabakia amesimama huku sura akiwa ameikunja
“Eddy nataka niingie huko ndani nikamkomeshe huyo Malaya wako”
“Kwani huku ndani ni kwako wewe vipi?”
“Eddy kama unataka nikujazie watu sema sishindwi mimi nakusemesha kiustaraabu unajifanya kuweka kibesi”
Mama Fety akausukuma mkono wangu uliokuwa umemzuai mlangoni na kuingia ndani kwa hasira.
“Mwangalie lilivyo mshuka”
Mwalimu Zena alizungumza huku akimtazama Mama Fety na kumfanya aanze kuangua kicheko huku akikaa kwenye sofa
“Shosti zangu jamani nisameheni kwa kuwatukana jamani”
“Mimi nilivyo isikia sauti yako wala sikujisumbua kunyanyuka kwani tumesha kuzoea”

Madam Recho alizungumza na kunifanya nishangae hapo ndipo nikagundua wanajuana ila sikujua wamejuana juana vipi
“Eddy huyu Asha umejuana naye vipi?”
“Heee Zena hadi kujuana na Eddy unataka kujua hembu acha ushapkuna”
“Sio ushapkuna kwa maana Eddy wa watu hapa Tanga hana hata mwezi bibi wewe umesha anza  kumuwekea wivu”
Wakaachia kicheko kikali huku kikisindikizwa na maneno ya kimbea ‘KANITANGAZE USIPO NITANGAZA NITAKUTANGAZA MIMI’ huku wakigongeana mikono na kunifanya nikae kimya
“Eddy usitushangae huyu Asha sisi tumemjua kutokana na mwanaye anasoma kidato cha pili basi huyo mtoto wake mcharuko kama mama yake haipiti mwezi bila shost huyu kutinga shule kusikiliza kesi ya mwanaye”

“Eddy wala mwanagu si mcharuko wanamsingizia tu ndio maana siku nyingine huwa ninawachambaga waalimu”
“Unatuchamba au tunakuchamba na safari hii  mwanao akileta tu mapepe mapepe tunamtimua”
“Mtimueni kwani shule ni moja nitampeleka ulaya akasome”
“Teeee ulaya kwenyewe unapasikia ndio embuse mwanao apeleke kiuno chake huku kufanya nini”
“Si kusoma”

ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )