Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Tuesday, February 20, 2018

TANGA RAHA- Sehemu ya Tisa ( 9 )

juu
MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA

Rahma akiwa anaendelea kuzungumza na simu kwa mbali nikamuona Mama Fety(Fatuma) akija katika eneo la ninapoishi huku akiwa ameongozana na mwanamke mwengine ambaye sikuweza kumtambua mara moja kwani bado wapo mbali kidogo na nilipo simama mimi
 
ENDELEA
Rahma akamaliza kuzungumza na simu akashush kiio cha gari katika upande nilio simama mimi
“Baby wala siingii ndani hapa baba amenifokea kama nini kwa jinsi nilivyo chelewa”
“Sawa tutaonana kesho shule?”
“Powa.Nakupenda Sir Eddy”
“Hata mimi ninakupenda pia”
Rahma akawasha gari na kuondoka.Nikabaki nimesimama huku nikiwaona Mama Fety na mwenzake wakija nilipo simama
“Mambo Eddy?”
“Powa vipi?”
“Safi mida ya mchana nilikuja sikukuta ulikwenda wapi?”
“Kuna sehemu nilikwenda kufwatilia mambo yangu ndio ninarudhi hivi”
 
“Ahaa vipi chai ulikunywa”
“Ohhh yaani mwanao alipokuwa anaileta yaani nilikuwa ndio naondoka ikanibidi niiweke ndani na sasa hivi kama unavyo niona ndio ninarudi”
Nikamuona rafiki wa Mama Fety akimminya Mama Fety kiunoni kama anapeana ishara ila sikujua ni ishara ya nini
“Karibuni ndani”
Tukaingia chumbani kwangu nikawakaribisha na kuwawashia video waangalie wanachopenda kuangali.
“Baby huyu ni rafiki yangu anaitwa Saumu…..Saumu huyu kama nilivyo kuadisia anaitwa Eddy ndio mahabuba wangu”
Utambulisho alio ufanya Mama Fety haukunifurahisha hata kidogo japo ninajitahidi kuweka sura ya furaha usoni kwangu
“Nashukuru kukufahamu Eddy”
 
“Na mimi pia nasg=hukuru kukufahamu”
Nikachukua Laptop yangu na kuanza kupangilia mada nitakazo fundisha shuleni siki itakayo fwata.Wakaendelea kutazama Video baada ya muda Mama Fety akanyanyuka kutoka katika sofa alilo kaa hadi kwenye sofa nililo kaa mimi.
“Baby”
“Mmmmm”
“Mbona upo kimya jamani hata huzungumzi na sisi?”
“Kuna kazi hapa nina ifanya si unajua kesho ni Jumatatu inanibidi kupangilia kila kitu cha kufundisha mapema ili kesho nisipate tabu”
“Utamaliza saa ngapi?”
“Kwani munataka kuondoka?”
“Hapana ila nilitaka kujua ni saa ngapi utamaliza kwani mimi na rafiki yangu tunataka tukupeleke ukashangae shangae mji”
 
“Kwa hili best itakuwa ngumu”
“Kwa nini jamani?”
“Hap nilipo nimechoka kiasi kwamba nikimaliza tu hii kazi nalala ili kesho nisichelewe kazini”
“Jamani Baby si tunakwenda mara moja mida ya saa tano tano tunarudi”
“Yaani kweli kwa hapo nisamehe baby hembu tufanye siku nyingie”
“Mama Fatuma kweli shemeji Eddy anaonekana amechoka muache apuumzike kwani si yupo kila siku”
“Shemeji umeona eheeee”
“Haya bwana mumeamua kunishambulia watu wawili basi sina jinsi inabindi nikubaliane na nyini”
 
Nikashukuru Mola kwa shemeji Saumu kunitetea.Mama Fety akarudi alipokuwa amekaa awali na kuendelea kutazama video,baada ya dakika kumi wakaaga na kuondoka mimi nikashukuru Mungu.Nikamaliza kufanya kazi zangu nikaingia bafuni nikaoga na kupanda kitandani na kuaanza kuulazimisha usingizi huku kumbukumbu za maisha yangu ya nyuma zikianza kunijia akilini.

==>Endelea Nayo <<kwa Kubofya Hapa>>
chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )