Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Saturday, February 17, 2018

Uchaguzi Kinondoni: Mambosasa Asema Jeshi la Polisi halitamvumilia mtu

juu
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, SACP Lazaro Mambosasa amesema kuwa jeshi lake limeimarisha ulinzi wa kutosha kila eneo ili kuhakikisha hakuna vitendo vyovyote vya uvunjifu wa amani vitakavyotokea.

Akizungumza na wana habari, Mambosasa amesema  kuwepo askari wengi katika maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Kinondoni ni dalali njema za kuwepo kwa amani na utulivu hivyo wananchi wasihofie kuwepo kwa vurugu yoyote

“Askari wapo Stand by kutoka eneo lolote la wilaya za Dar es Salaam pale watakapohitajika kuongeza nguvu katika Wilaya ya Kinondoni,” alisema.

Akaongeza kuwa usalama wa raia upo vizuri na hakuna vurugu yoyote iliyotokea kuanzia asubuhi hadi majira ya saa kumi, lakini ametoa onyo kwa tetesi ambazo amesikia kwamba kuna makundi ya watu wanaotarajiwa kutokea maeneo ya Ilala la Temeke kuelekea Kinondoni kwa ajili ya kujikusanya na kufanya uhalifu, hivyo jeshi lake halitamvumilia mharifu.

Kwa upande mwingine, zoezi la kupiga kura sasa limekwisha fungwa kwa wananchi kulingana na sheria za Tume ya Uchaguzi ambako sasa wasimamizi wa vituo kwa kushirikiana na mawakala wa vyama mbalimbali wameanza kuhesabu kura zilizopigwa.
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )