Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Monday, March 5, 2018

Katibu Mkuu CHADEMA Ahojiwa na Kuachiwa Kwa Dhamana

juu
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Vicent Mashinji amehojiwa na polisi kwa saa mbili na kuachiwa kwa dhamana.

Wakati Mashinji akihojiwa, vigogo wengine watano wa chama hicho alioambatana nao hawakuhojiwa, badala yake wote kwa pamoja wametakiwa kuripoti tena Kituo Kikuu cha polisi Machi 13, 2018.

Mmoja wa mawakili wa viongozi hao Alex Massaba amesema Dk Mashinji amehojiwa kwa tuhuma za kusababisha mkusanyiko isivyo halali.

Mashinji amehojiwa kuanzia saa 5:30 asubuhi hadi saa 7:30 mchana.

Februari 27, 2018 viongozi hao wakiongozwa na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ambaye leo hakuwepo baada ya kuugua ghafla na kulazwa Hospitali ya Rufaa ya KCMC mjini Moshi, walifika kituoni hapo na kuhojiwa kwa takribani saa tano, kisha kuachiwa kwa dhamana na kutakiwa kuripoti tena leo.

Leo viongozi hao wakiongozwa na Dk Mashinji ambaye Februari 27, 2018 hakufika kuhojiwa kutokana na kuwa nje ya nchi, mpaka saa nane mchana walikuwa wameondoka kituoni hapo.

Mbali na Mashinji, viongozi wengine waliofika kituoni ni naibu makatibu wakuu, John Mnyika (Bara) na Salum Mwalimu (Zanzibar).

Pia, wamo mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha), Halima Mdee; mwenyekiti wa kanda ya Serengeti, John Heche na Esther Matiko ambaye ni mweka hazina wa Bawacha.

Kwa mujibu wa Massaba, wengine walioambatana na Mashinji hawakuhojiwa.

"Awali Mashinji  hakuwepo wakati wenzake wanahojiwa lakini leo amefika na amehojiwa kwa kosa moja la kufanya mkusanyiko usio halali,” amesema Massaba.

Amesema ikiwa Machi 23, viongozi hao hawatapelekwa mahakamani, hawataripoti tena kituoni hapo kwa mdai kuwa utakuwa usumbufu.

Amesema hilo linatokana na baadhi ya viongozi hao kuwa wabunge, hivyo wanahitaji kushiriki vikao vya Bunge vitakavyoanza mapema Aprili, 2018.

Februari 20, 2018 Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam iliagiza kukamatwa viongozi saba waandamizi wa Chadema akiwamo Mbowe.

Wito huo ulikuja siku chache baada ya tukio la kuuawa kwa mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwilini.

Akwilina aliuawa kwa kupigwa risasi akiwa ndani ya daladala eneo la Mkwajuni, Kinondoni jijini Dar es Salaam wakati polisi wakiwatawanya wafuasi wa Chadema waliokuwa wakienda ofisi za mkurugenzi wa Halmashauri ya Kinondoni kudai viapo kwa mawakala wao.
chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )