Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Tuesday, April 3, 2018

AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 75 na 76 )

juu
MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA-

ILIPOISHIA  

Nilipo hisi ninaweza kufa kwa kumwagiwa maji haya yenye nguvu, nikajigeuza na tumbu langu nikalielekezea kwenye ukuta, nikawaachia mgongo ambao wakaendelea kuushambulia kwa maji hayo nyenye nguvu hadi nikaishia wanguvu kabisa na kujikuta nikilala chini. Walipo niona nimelegea kabisa, wakanicha na kuufunga mlango wa chumba hichi cheye maji mengi na kunifanya nilale hapa chini huku machozi yakinimwagika na kujiuliza ni kitu gani kinacho endelea kwneye maisha yangu ya hivi sasa.

ENDELEA
Taratibu nikajinyanyua huku mwili wangu ukiwa umejawa na maumivu makli sana yaliyo tokana na kumwagiwa maji yenye nguvu. Nijajarubu kusimama ila mwili mzima ukakosa nguvu, sikuwa na jinsi zaidi ya kuendelea kukaa hapa chini. Haukupita muda mwingi, mlango ukafunguliwa wakaingia wasichana wanne ambao  ni tofauti kabisa na wale ambao walinimwagia maji. Wasichana hawa ambao miili yao imejengeka kwa misuli kama wanaume, wakanifwata na kuninyanyua, wakaanza kuniburuza
na kunitoa nje ya chumba hichi.

Wakanipitisha katika kordo ambayo ina vyumba vingi vya wafungwa na vina mageti ya vyuma. Karibia wafungwa wote ambao wapo ndani ya vyumba vyao waliendelea kunitazama kwa umakini huku wengi wao wakionekana kunikasirikia sana. Mlango wa chumba kimoja ukafunguliwa. Wakanisukumia ndani ya chumba hichi chenye hewa nzito sana. Nikaanguka  chini huku nikiwa nina hema sana. Nikastukia nikiwa nimeguswa mgongoni, taratibu nika na kumtazama aliye nishika. Nikakuta ni yule kijana wa kiharabu ambaye alinikaribisha katika kiti cha pembeni alicho kuwa amekikaa.
”Pole”
Alizungumza huku  akinitazama usoni mwangu, taratibu akanipa mkono wake, akaninyanyua huku akinitazama usoni mwangu. Taratibu akanisaidia kunikalisha kitandani, nikakitazama chumba hichi chenye vitanda viwili ambavyo vina vitanda vya juu na chini ambavyo vijajulikana kwa jina la double deka.

“Hivi hapa ni wapi?”
Niliuliza huku nikihema sana.
“Kusema kweli mimi bado sijaelewa hili eneo, mimi nilitekwa tu na kujikuta nikiwa humu ndani ya hili gereza”
“Una muda gani hadi kuwemo kwenye hili gereza?”
“Ni mwaka sasa, ni siku nyingi sana nimetekwa, sifahamu kama familia yangu ina hali gani?”
“Na kwenye hichi chumba unaishi na nani?”
“Tulikuwa watatu, ila wawili wamesha kufa kwenye yale mapambano kwenye ule ulingo. Yaani hili gereza kwa haraka haraka hii ni sehemu ya kifo, mtu anaingia ila hakuna ambaye anaweza kutoka”
Taratibu nikashusha pumzi huku nikiutazama mlango ulio tengenezwa na nondo. Kusema kweli nilisha ingia kwneye magereza kadhaa kama mtembezi, hata gereza nililo kuwa nimefungwa miezi kazaa iliyo pita lina nafuu tena kubwa sana, kwa maana nilifungiwa tu kwenye chumba kimoja ila hili lina mchanganyiko mkubwa wa watu wa kila aina na karibia asilimia tisini na tisa ya watu wa humu ndani ya hili gereza wana roho mbaya sana.

chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )