Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Wednesday, April 18, 2018

Aliyedai kuwa ni mtoto wa Lowassa atiwa mbaroni

juu
Jeshi la Polisi Kanda Maalum linamshikilia Fatma Chikawe 31 kwa kosa la udhalilishaji na kusababisha taharuki kwa jamii.

Kamanda  wa Polisi wa Kanda Maalum, Lazaro Mambosasa amesema msichana huyo wananamshikilia na kumhoji kwa kosa la kumdhalilisha kiongozi mstaafu Edward Lowassa na kusababisha taharuki kwa jamii.

“Ni kweli tunamshikilia huyo msichana aliyejitokeza na kudai ni mtoto wa Lowassa hivyo tunamhoji baada ya kukiri amedanganya kwa makosa ya kumdhalilisha na kusababisha taharuki kwa jamii,”amesema Kamanda Mambosasa.

Kamanda Mambosasa amesema wanaendelea na upelelezi na utakapokamilika watamfikisha mahakamani kujibu mashtaka yanayomkabili.

Aprili 10 msichana huyo alikuwa ni miongoni mwa watu waliojitokeza kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa akitaka kupewa msaada wa kisheria baada ya kudai baba yake ni Edward Lowassa na toka azaliwe hajawahi kumuona baba yake.

Aprili 15 ilionekana video ya msichana huyo ikisambaa kwenye mitandao ya kijamii akiomba radhi kwa kumdhalilisha Lowassa na kusema tukio hilo limechukuliwa kisiasa na sasa anakosa amani.
chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )