Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Wednesday, April 11, 2018

Thea Atoa Pongezi Zake kwa Makonda ....... Ni Baada ya Kampeni ya Kusaidia Wanawake

adv1
Msanii wa bongo movies Ndumbagwe Misayo maarufu kama Thea ameandika ujumbe mrefu kwa ajili ya kumpongeza Mh Paul Makonda baada ya kuanzisha kampeni ya kusaidia wanawake ambao wametelekezwa na wanaume zao na kuwaachia watoto kulea peke yao.

Thea aliandika hivi kuhusu kampeni hiyo ya Mh Paul:
"Kwanza nimpogeze mheshimiwa paul makonda kwa kujitolea na kulikumbuka kundi hili la wanawake waliojitokezwa, kwakweli tatizo hili ni kubwa sana  na kumuachia Mh Makonda peke yake haitwezekana kwa sababu tatizo sio kwa dar peke yake bali ni Tanzania nzima.

"Niombe wadau wa maendeleo ya wanawake tanznia kutafuta suluhu ambayo ni endelevu kwa tatizo hili.upo ukatili unaotokea kama ajali lakini ukatili huu mwingi kwa wanawak na wasichana utokana na umaskini.

"Wanawake hawa waliojitokeza leo inamaanisha kuwa hawajaweza kumudu mahitaji ya msingi, nitoe wito kwa wanawake na wadau wengine kumuunga mkono Mh Paul Makonda ili kuweza pia kuwakwamua wanawake hawa kiuchumi.

"Tuwasaidie wanawake hawa kuwa na uchumi imara kwa sababu sio wanaume wote wanakataa kutoa matunzo kwa makusudi, wengine wamekuwa wakiyumba.

Hata hivyo kutokana na kampeni hii kila mtu amekuwa na muonekano tofauti kwa sababu wapo wanaosapoti na pia wapo wanaosema zoezi haliwezi kumaliza tatizo.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )