Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Saturday, May 19, 2018

Makonda Kuwachukulia Hatua Kali Viongozi wa Michezo

juu
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amesema atachukua hatua kwa viongozi wa michezo ambao hawajafanya marekebisho ya uwanja wa Taifa wa ndani 'indoor' licha ya kuwakabidhi pesa na vifaa mwaka jana.

Makonda amesema Mei 18, 2018 wakati akiongea na waandishi wa habari na kuongeza kuwa alikubali kujinyima na familia yake ikae gizani kwa kutoa jenereta la nyumbani kwake ili kutimiza ahadi ambayo aliwahidi wanamichezo hao lakini imekuwa kinyume na mategemeo.

“Lile jenereta nililihamisha badala ya kuwepo nyumbani kwa mkuu wa mkoa nikalikabidhi mwaka jana, sasa kama mpaka leo hii halijaenda basi kutakuwa kuna shida mahala, na niwaambie tu siwezi kuahidi kitu nisifanye hata kama ni cha kwangu nitajinyima, nimeinyima familia yangu wakae gizani ili nihakikishe kwamba jenereta linakwenda kwa wapenzi wa mpira” amesema Makonda.

Makonda ameongeza kuwa atawasiliana na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam, Lazaro Mambosasa ili aweze kuwachukulia hatua watu ambao wameshibdwa kutimiza majukumu yao

Mkuu wa Mkoa Makonda amesema mwaka jana alikabidhi pesa, mipira, mabati na jenereta ili kusaidia uwanja wa Taifa wa ndani uliokuwa katika hali mbaya na hivyo anashangaa kusikia bado hakuna kilichofanyika mpaka sasa.
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )