Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Wednesday, May 23, 2018

Watumishi wa Ofisi ya RC Arusha wabadilishiwa mashtaka Mahakamani

juu
Ofisa Itifaki wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha, Swalehe Mwidadi na mfanyakazi wa Masijala Amina Mshana leo May 23, 2018 wamepanda kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Arusha na kusomewa shtaka la unyang’anyi wa kutumia silaha.

Akisoma hati ya mashtaka Wakili wa serikali Sabina Silayo mbele ya Hakimu Mkazi Patricia Kisinda, amedai kuwa watuhumiwa hao kwa pamoja wanashtakiwa kwa makosa mawili.

Amedai kuwa kosa la kwanza, wametenda mnamo May 13, 2018 eneo la Sakina washtakiwa hao walimwibia Mwandishi wa Habari wa kujitegemea Lucas Myovela simu aina ya Tekno  C7 ya thamani ya Sh.300,000,  simu aina ya Sumsung yenye thamani ya Sh.50,000 na walifanya unyang”anyi huo kwa kutumia panga na mkanda wa plastiki.

Aliendelea kutaja kuwa vitu vingine walivyoiba ni pamoja na fedha taslimu Sh.75,000 na walijihamishia fedha Sh.9,500 za Mpesa na kadi ya ATM ya benki ya CRDB, huku wakijuwa kufanya hivyo ni kosa kisheria.

Silayo alidai kuwa kosa la pili was wanashtakiwa kuwa mnamo May 13, 2018, eneo la Sakina kwa pamoja walifanya kitenfo cha ukatili na udhalilishaji kwa kumvua Lucas Myovela nguo zake na kumchukua picha akiwa uchi.

Alidai kuwa kufanya hivyo ni kosa kisheria na kufunguliwa kesi hiyo namba 153/2018.

Washtakiwa walikana mashtaka hayo na Wakili Silayo amedai upelelezi haujakamilika na kuomba mahakama kupanga tarehe nyingine ya kutajwa.

Hakimu Kisinda amedai kesi hiyo haina dhamana na shtaka la kwanza halina dhamana hivyo alipanga kutajwa tena June 5 mwaka huu.
chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )