Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Monday, June 11, 2018

Kamanda Wa Polisi Mkoa Wa Mwanza Atoa Ufafanuzi Juu Ya Tukio La Polisi Anayetuhumiwa Kufanya Mauaji Wilayani Misungwi

juu
Kwamba tarehe 09.06.2018 majira ya saa 23:00hrs usiku katika mtaa wa Misungwi kati eneo lenye maduka wilaya ya Misungwi mkoa wa Mwanza, kikundi cha walinzi wanaolinda maduka katika eneo hilo walimkamata  mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Christian Audock Joseph miaka 31, muuguzi katika hospitali ya Misungwi, kwa tuhuma za kutaka kufanya kosa la wizi katika maduka hayo.

Inasemekana kuwa wakati walinzi hao wakiwa na mtuhumiwa, walimwona  askari polisi mmoja aitwaye Abushee akipita akienda kula daku huku akiwa amevalia sare za jeshi la polisi ndipo walimsimamisha na kumweleza askari kwamba wamemkamata mtu huyo kwa kosa la kutaka kufanya wizi katika maduka wanayoyalinda, lakini inasadikika kuwa mtuhumiwa alikuwa katika hali ya ulevi.

Inadaiwa kuwa baada ya askari huyo kupewa taarifa hizo alimshika mtuhumiwa huyo kisha inadaiwa alimtembezea kipigo hadi akazirai, kisha walinzi waliondoka na baadae pia askari aliondoka huku wakimwacha mtuhumiwa akiwa amezirai hapo chini.

Inadaiwa kuwa pindi ilipofika asubuhi alionekana mtu yule tayari amefariki dunia ndipo wananchi walitoa taarifa polisi, ambapo askari walifanya ufuatiliaji wa haraka hadi eneo la tukio na kuukuta mwili wa marehemu mahali hapo, pamoja na kufanya uchunguzi na mahojiano. 

Polisi wanamshikilia askari Abushee kwa mahojiano zaidi, vilevile upelelezi unaendelea juu ya tukio hilo ili kuweza kupata ukweli halisi wa kifo hicho, mwili wa marehemu umehifadhiwa hospitali ya Misungwi kwa ajili ya uchunguzi, pindi uchunguzi ukikamilika utakabidhiwa kwa ndugu wa marehemu kwa ajili ya mazishi.

Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Naibu Kamishina wa polisi Ahmed Msangi anatoa rai kwa baadhi ya waandishi wa vyombo vya habari hususani blog na magazeti akiwataka kuacha tabia ya kuongeza chumvi katika uandikaji wa taarifa zao ambapo katika tukio hili baadhi ya vyombo vya habari vimedai kuwa kundi la polisi ndio lililomkamata marehemu, huku vyombo vingine vikidai kuwa kundi la askari ndilo lililomshambulia marehemu kitu ambacho sio kweli

Hivyo anawaomba waandishi kabla ya kuandika taarifa zao wawe wanauliza kwanza ili kuweza kupata ukweli wa taarifa toka pande zote mbili.
chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )