Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Saturday, June 23, 2018

LHRC yalia na katiba mpya, Bisimba afunguka

juu
Timu maalumu ya wataalamu iliyoundwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kufuatilia mkwamo wa mchakato wa Katiba Mpya imependekeza njia tatu za kupatikana kwa Katiba Mpya.

Njia zilizopendekezwa ni Mosi, kuendelea na mchakato kuanzia pale ulipoishia, kwa wananchi kupigia kura Katiba Inayopendekezwa.

Pili, kuundwa kwa timu ya wataalamu watakaoandaa rasimu nyingine ya Katiba ambayo itapelekwa kwa wananchi kwa ajili ya kupigiwa kura ya Ndiyo au Hapana.

Tatu, ni kujenga mwafaka wa kitaifa ili makundi yatakayoingia kwenye Bunge Maalumu la Katiba yawe na dhamira moja ya kuandaa katiba bora kwa maslahi ya Taifa.

Akizungumzia mkwamo wa mchakato wa Katiba mpya jana Ijumaa Juni 22, 2018 kiongozi wa timu hiyo, mhadhiri wa sheria katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Udsm), Dk James Jesse alisema mchakako wa Katiba Mpya ulisababishwa na kukosekana kwa mwafaka wa kitaifa.

Alisema makundi mbalimbali yalikuwa na malengo tofauti katika katiba, jambo lililosababisha wapinzani kususia mchakato huo na kufanya Bunge liwe la upande mmoja.

Alibainisha sababu nyingine kuwa ni uchaguzi wa mwaka 2015 ulisababisha kusimama kwa mchakato huo.

Alibainisha kuwa Serikali na vyama vya siasa vilielekeza nguvu zao kwenye uchaguzi huo na kuacha Katiba.

"Mwafaka wa kitaifa unaonekana ungekuwa suluhisho na kupatikana kwa Katiba lakini haukuwepo ndiyo maana tunaikumbusha Serikali kuhuisha mchakato huo," alisema.

Dk Jesse amlibainisha sababu nyingine ya mkwamo huo ni Serikali ya Awamu ya Tano kusisitiza kwamba Katiba Mpya si kipaumbele chake bali maendeleo ya Taifa.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Dk Hellen Kijo-Bisimba alisema Katiba Mpya ni moja kati ya ajenda tatu za kituo hicho na wataendelea kuhamasisha kupatikana kwake.

Alisema kuna mambo mengi ya muhimu yameondolewa kwenye Katiba Inayopendekezwa kama vile mgawanyo wa madaraka, ukomo wa ubunge na tunu za Taifa.

"Tuendelee na mchakato wa katiba Mpya, haijalishi tutaanzia wapi lakini tunataka iwe na mambo muhimu ambayo yaliondolewa kwenye rasimu ya pili ya katiba kama vile tunu za taifa, ukomo wa ubunge, usawa wa kijinsia na mgawanyo wa madaraka," alisema Dk Kijo-Bisimba.
chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )