Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, June 14, 2018

Salah Ufufua Matumaini Ya Waafrikakombe La Dunia

adv1
Na magdalena kashindye.
Nyota wa Liverpool na timu ya taifa ya Misiri, Mohamed Salah amepona majeraha yake.

Mchezaji huyo anapewa nafasi kubwa ya kukiongoza kikosi cha Misri Ijumaa ya wiki ijayo dhidi ya Uruguay ukiwa ni mchezo wa kwanza kwa taifa hilo katika michuano ya Kombe la Dunia inayoanza leo.

Salah aliumia katika mchezo wa fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya kwa kuchezewa faulo mbaya na nahodha wa Real Madrid, Sergio Ramos na kuondolewa nje wa uwanja hali iliyozua hofu kwa mashabiki wa misiri kuwa angekosa mchezo ya fainali la kombe la dunia inayofanyika nchini Urusi.

Kupona kwa Salah kumefufua  matumaini ya Waafrika  kwenye safu ya ushambuliaji wa timu hiyo kutokana na uwezo  mkubwa aliouonesha uwanjani mwaka huu.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )