Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Friday, June 1, 2018

Wizara Yalaani Vitendo Vya Ukatili Wa Kijinsia Vinavyoshamiri Nchini

adv1
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inalaani na kukemea matukio ya ukatili wa kijinsia hasa kwa wanawake yaliyotokea hivi karibuni katika Mkoa wa Dodoma  Pwani na Mwanza.

Wizara imepokea taarifa za ukatili kwa wanawake hao kwa mshituko makubwa, na ina kemea vitendo hivyo vya ukatili maana ni ukiukaji wa Haki za Msingi za binadamu.

Matukio hayo yaliyotokea Dodoma Pwani na Mwanza ni tukio la Mei 26 Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) Rose Malfred (31), mkazi wa Swaswa aliyeuawa kikatili na mumewe ambaye inadaiwa kuwa ni Mchungaji wa Kanisa la TAG Bw. John Mwaisango, kwa kumchoma visu sehemu mbalimbali za mwili hadi kufa. 

Tukio linguine lilitokea Mei 25, mwaka huu, ambapo mwili wa Muuguzi wa Hospitali ya Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani, Rosemary Mgombela, ulikutwa umefukiwa pembeni ya nyumba wanayoishi.

Aidha, tukio lingine lililoripotiwa Aprili 30, mwaka huu ni la mfanyabiashara wa samaki mkazi wa mtaa wa Mahakama wilayani Ilemela, Bw.Nicholas Light (25) ambaye alimuua mpenzi wake, Victoria Swai (26) kwa kumnyonga na kumkaba shingo kwa wivu wa mapenzi.

Matukio hayo yote ni kinyume cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,ya mwaka 1977 inayoeleza bayana haki ya kuishi kwa kila raia, Ibara ya 14 ya Katiba hiyo imeeleza kuwa kila mtu ana haki ya kuishi na kupata kutoka kwa jamii hifadhi ya maisha yake kwa mujibu wa Sheria.

Wizara inapenda kuchukua fursa hii kuiasa jamii kutoa taarifa kwa vitendo vya ukatili kwa wanawake katika jamii ili kudhibiti matukio ya ukatili hususan mauaji ya wanawake ambao unafanywa na watu waovu na kusababisha hofu kubwa katika jamii.

Wizara inaikumbusha jamii kuwa udhibiti wa vitendo vya ukatili kwa wanawake na vitendo vingine viovu vinahitaji  juhudi za pamoja katika kuvitokomeza; ikiwa ni pamoja na kuimarisha ushiriki wa wananchi katika kuripoti vitendo vya ukatili.

Tunaliamini Jeshi la Polisi kwa umakini wake na kwamba litahakikisha linasimamia Sheria ili iweze kuchukua mkondo wake kwa wale wote waliohusika na kufanya vitendo vya ukatili kwa wenza wao  ili iwe Aidha, fundisho kwa wengine.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )