Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Tuesday, July 10, 2018

Mwigulu Nchemba Akabidhi Ofisi kwa Kangi Lugola Huku Akiwalilia Bodaboda

juu
Hatimaye aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani na mbunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu Lameck Nchemba, amekabidhi ofisi kwa waziri Kangi Lugola. Makabidhiano hayo yamefanyika mapema leo asubuhi kwenye makao makuu ya wizara hiyo yaliyopo jijini Dodoma.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Mwigulu amesema kuwa anamtakia majukumu mema Lugola katika utumishi wake kwa watanzania na kuongeza kuwa mbali na kukabidhi ofisi, amekabidhi pia hotuba ya bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2018/2019 ambayo ina majukumu yaliyopo mbele yake kwa sasa.

“Mbali na ofisi nimekabidhi pia hotuba ambayo ndiyo yenye majukumu ambayo yalikuwa yamepangiliwa kama wizara na serikali katika bajeti hii na kikubwa ni mabadiliko ya baadhi ya sheria zilizokuwa na mapungufu hasa kwa Jeshi la Polisi”, amesema Mwigulu.

Mwigulu ametaja moja kati ya majukumu aliyoacha mezani kuwa ni, kupunguziwa faini kwa madereva bodaboda na bajaji iwe tofauti na madereva wa magari makubwa kwani kuwekwa kwa kiwango sawa ni uonevu kwa madereva hao.
chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )