Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, August 16, 2018

Kesi ya Tido Mhando Yapigwa Kalenda Tena

juu
Kesi inayomkabili  Mkurugenzi mkuu wa zamani wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Tido Mhando imepigwa kalenda tena hadi Agosti 27, 2018 ambapo mashahidi wa upande wa Mashitaka wataendelea kutoa ushahidi wao.

Kesi hiyo ilipaswa kuendelea kusikilizwa leo Alhamisi Agosti 16, 2018 lakini wakili wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Leonard Swai ameieleza mahakama kuwa hawana shahidi na akaomba kesi ipangiwe tarehe nyingine ili iendelee kusikilizwa.

Hata hivyo, Hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo, Kelvin Muhina amesema Hakimu Mkazi Mkuu, Huduma Shaidi anayeiendesha kesi hiyo anaumwa na kupanga tena tarehe hiyo.

Tido anakabiliwa na mashtaka manne ya kutumia madaraka vibaya na moja la kuisababishia Serikali hasara ya Sh887.1 milioni.
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )