Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Sunday, September 16, 2018

Waitara Apiga Kura Ukonga....Azungumzia Mwitikio Hafifu wa Wapiga Kura

juu
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Ukonga kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi CCM Mwita Waitara amezungumzia juu ya muamko hafifu wa upigaji kura katika Jimbo hilo changamoto ambayo pia ilitajwa na Msimamizi wa Uchaguzi Jumanne  Shauri.

Amesema huenda kuna sababu mbalimbali zilizopelekea muamko hafifu na kuwataka wananchi kujitokeza kabla ya saa kumi ili kupiga kura.

Waitara amesema hayo mara baada ya kupiga kura kwenye kituo cha Kerezange kilichopo Kivule asubuhi ya leo Septemba 16, 2018.

“Wananchi wanajua zoezi linaisha saa kumi jioni, kuna wengine wanashughuli mbalimbali mi naona zoezi linaenda vizuri hali ni shwari na bado kuna muda wa kutosha wa watu kuendelea kupiga kura…” amesema Waitara

Akizungumza kuhusu tishio la vurugu, Waitara amesema hakuna vurugu kwa sababu wageni waliokuja wakati wa kampeni wameshaondoka waliobaki ni wenyeji.

"Hili ni jimbo letu sisi mwisho wa siku tumebaki wenyewe wajuaji wameshaondoka, hivyo hakuna vurugu.

"Ukumbuke hili jimbo lina mitaa 70 saba tu ndiyo ya upinzani na 63 ni CCM, unaweza kuona ni kwa jinsi gani hakuwezi kuwa na vurugu hakuna anayeweza kuifanyia vurugu CCM," amesema Waitara.

Uchaguzi wa jimbo la Ukonga unarudiwa kufuatia aliyekua Mbunge wa jimbo hilo kupitia CHADEMA Mwita Waitara kutangaza kujivua nafasi hiyo july 28 mwaka huu kwa madai ya kuwa na mgogoro na Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe.
chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )