Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Tuesday, October 16, 2018

AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 104 na 105 )

juu
MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA- 0657072588
ILIPOISHIA       

Nilizungumza huku taratibu nikifungua kichupa hichi. Nikaanza kushuhudi jinsi kinavyo pungua maji yake taratibu. Nikashuka na kuwakuta Cajoli wakinisubiri,
“Kinapungua kweli aisee”   
“Yaa hiyo itakuwa ni kazi, hapa virusi hao wanakimbilia sehemu yenye maji. Na hewa hii itasambaa Tanzania mzima”
“Vipi kwa wale wa Kenya, kwa maana hii hewa haina mipaka?”
Ukimya ukatawala kati yetu huku kila mmoja akifikiria jambo hilo.
“Ngoja tuangalie itakuwaje, ikionekana vipi nao wacha waje tu. Ni moja ya biashara, unacho kihitaji wewe Dany ni pesa na nguvu”
Cajoli alizungumza kwa kujiamini na kuzidi kunifanya nijione mshindi katika kisasi changu ambacho kwa sasa sihitaji kutumia nguvu sana kulipiza, ila ninatumia akili kuhakikisha maadui zangu wanaisoma namba.

ENDELEA
Tukarudi ndani, huku kila mmoja akiwa na matumaini makubwa sana kwa kili ambalo tumelifanya.
“Kazi niliyo ibakisha ni kutengeneza antbiotic itakayo waua virusi hao endapo serikali itajitaidi na kushindwa kuhimili ugonjwa”
“Ila wataweza kweli kutafuta dawa?”
“Hakuna hawatoweza kutafuta dawa pasipo mimi. Kilicho salia hivi sasa ni kiwa macho katika vyombo vya habari kutazama ushindi wetu”
 
Cajoli alizungumza na kuzidi kunipa matumaini kwa kile ambacho amekifanya. Cajoli hakuwa na muda wa kupoteza, akaanza kutengeneza dawa ya kuua virusi ambao kwa sasa tayari wemesha anza kusambaa kwa kasi kama anavyo seme. Hadi inafika saa kumi na moja alfajiri akawa amemaliza kila kitu.
“Inabidi upumzike sasa mke wangu”
“Honey siwezi kupumzika hadi kufahamu ni majibu gani ambayo yatapatikana kwenye kile nilicho kifanya”
“Basi twendeni sebleni, tukiwa tunasubiri kupata majibu kwenye Tv, mimi ninaendelea kutengeneza kifungua kinywa”
“Shem hapo umenena la maana”
 
Tukaelekea sebeleni huku kila mmoja akiwa na hamu na shauku ya kufhamu kilicho tokea. Shem Cajoli akawasha tv yake, mimi na Cajol tukakaa kwenye sofa moja na kuendelea kuangalia ni kitu gani ambacho kinaendelea kwa maelefu ya watan
Hadi inatimu saa moja kamili asubihi hakuna taarifa yoyote ambayo inahusiana na ugonjwa ambao ni mpya.
“Jamani tunyweni chai kwanza”
“Labda virusi wangu hawajafanya kazi?”
Cajoli alizungumza kwa sauti ya unyonge na ya kukata tamaa, nikamvuta taratibu na kumlaza kichwa chake kwenye bega langu huku nikimpapasa pasasa kwa kiganja cha mkono wangu kwenye mgongo wake.
 
“Ngoja tuangalie muda mbona upo”
“Cajoli kwa hali hiyo hato kunywa chai mpaka jambo lake lifanikiwe”
“Honey twende tukanywe chai”   
“Hapana Dany, sina amani kabisa sipendi kufanya kitu na sikifanikiwe mpenzi wangu. Hususani kitu nimekifanya kwa ajili yako”
“Natambua hilo mpenzi wangu ila ninakuomba tukanywe chai tafadhali”
“Ngoja ngoja……”
Cajoli alizungumza huku akichukua rimoti na kuongeza sauti kwenye tv. Sote na macho na masikio yetu yakaelekea kwenye Tv kuangalia na kusikiliza taarifa hii ya dharura katika kituo cha taiafa
 
“Watu kumi, wamegundulika na ugonjwa ambao hadi sasa haujapatiwa jina. Ugonjwa huu ambao hadi sasa hivi haujajulikana umesababishwa na nini, umewakuta watu hao wambao kwa sasa wapo hospitali ya Taifa . Tujiunge na muandhishi wetu kwa taarifa kamili”
Nikajikuta nikikaa vizuri kwenye sofa huku nikiitazama taarifa hii.
“Majira haya ya asubuhi wagonjwa wapato kumi wameweza kufikishwa kwenye hospitali yetu. Ugojwa huu ambao nnaweza kuufananisha na mapunye, kusema kweli kwa miaka yangu thelathini ya kazi sikuwahi kuuona. Hadi sasa madaktari wanaendelea kufanya uchunguzu kuweza kubaini kwamba ugonjwa huu umesababishwa na nini”
 
Daktari alizungumza kisha taarifa hii ikakatishwa. Tukajikuta wote tukishangilia kana kwamba hili ambalo tumeliona ni jambo zuri.
“Baby umefanikiwa”
Nilizungumza huku nikimkumbatia Cajoli kwa nguvu. Shem Cajoli naye akatukumbatia kwa pamoja kwa maana huu ni  ushindi mkubwa sana kwenye maisha yetu. Tukajikuta sote watatu tukikaa kwenye meza moja na kupata kifungua kinywa kilicho andaliwa na shemeji.
“Jamani mimi inabidi niende mjini nikafanye uchunguzi kuangalia ni kitu gani kinacho endelea”
“Sawa”
 
“Wajina kama itawezekana ninakuomba umnunulie shemeji yako nguo. Si unamuona hana nguo za kueleweka”
“Sawa hilo halina shida kabisa”
“Shemji ikiwezekana ukiona wagonjwa huko mjini wewe wapige picha tuje kuwaona”
“Hilo hata usinge lizungumza mimi ningelifanya. Nina kamera yangu, nitarekodi matukio yote. Nitakwenda hospitali karibia zote za hapa Tanga mjini, ili mradi nijionee watu walivyo kuwa”
“Ila jamani tunashangilia kama mazuri”
“Mmm baby huu ndio mwanzo wa kulipiza kisasa. Hapa akili ndio inahiyajika. Sijui useme uende kutumia silaha utajikuta unaingia kwenye matatizo makubwa sana”
 
“Kweli mke wangu your genius”
Shem Cajoli akamaliza kupata kifungua kinywa, akaelekea chumbani kwake akajiandaa, hakuchukua muda mwingi akatoka akiwa amejiremba sana.
“Ehee shem umejiremba kama unakwenda harusini”
“Weee kwa staili hii hakuna ambaye anaweza kunigundua wala kunihisi kama mimi nipo nyuma ya mpango  wa huu wa hili gonjwa jipya”
“Kweli”
“Wajina hakikisha unakuja na make up za kumbadilisha sura bwana mkubwa”
“Usijali”
Shem Cajoli akatoka nje huku akiwa ameongozana na Cajoli ambaye anakwenda kufunga geti. Cajoli akarudi ndani, kwa haraka akanikumbatia na kuanz akuninyona midomo yangu.
“Siamini kama nimefanikiwa mume wangu”
 
“Sasa ninaanza kuona faida ya mimi kuwa na wewe”
“Real”
“Yeaa akili  yangu, mawazo yangu nikisha yapeleka katika utumiaji wa silha”
“Usijali mume wangu, nitahakikisha kwamba tunawaangusha maadui zako wote”
Taarifa nyingine ya habari inayo onyesha ongezeko la ugonjwa ambao kwa Tanzania ndio mara ya kwanza kuonekana, zikazidi kutawala kwenye kila televishion ya Tanzania. Hata mashirika makubwa kama BBC, SKY NEWS pamoja na CCN nayo yakaanza kutoa taarifa juu ya ungojwa huu. 
 
Kadri muda ulivyo zidi kwenda ndivyo maelfu  walivyo zidi kuongezeka kwa kuugua.
“Ngoja niangalie meseji kwenye simu yangu”
Cajoli alizungumza huku akinyanyuka kwenye mapaja yangu, kwa maana muda wote alikuwa amelaza kichwa chake pajani. Akachukua simu yake kwenye meza ya chakula na kurudi nayo kwenye sofa.
“Wajina amenitumia picha Whatsapp”   
“Hembu zifungue”
Cajoli alaanza kufungua picha hizi ambazo nizaidi ya ishirini.
“Mungu wangu!!”
Cajoli alijikuta akishangaa, jinsi wananchi wanavyo pata shida juu ya ugonjwa huu. Mahospitalini wagonjwa wamejaa, si madaktari wala manesi nao wanaugua ugonjwa huu.
“Dany hembu angalia jamani”
 
“Unawaonea huruma”
“Ahaa jamaani roho inaniuma, sikudhani kama wale virusi wataathiri watu wengi kiasi hichi”
“Ndio hivyo honey, acha serikali ichanganyikiwe”
Katika picha alizo zituma shem Cajoli, nikaona picha ya baadhi ya askariwa NSS akiwemo mkuu wao Babyanka naye akiwa ni miongoni mwa wagonjwa walio toka mapunye uso mzima.
“Dany unaonaje ukatafuta njia ya kuonana na raisi”
“Ili?”
“Muweze kuyamaliza haya, roho inaniuma kuona hadi watoto wadogo wakiwa katika hali mbaya kama hii”
“Cajoli acha serikali itutafute, hadi jioni tutaangalia imekuwaje”
Cajoli  hakuwa na kipingamizi chochote katika nililo liamua. Majira ya saa tisa alasiri, wagonjwa ambao hadi sasa wameathirika wamefika idadi zaidi ya watu milioni ishirini.
“Dany kusema  kweli ninazidi kuogopa kila ninapo iona hii taarifa”
 
“Cajoli una niamini?”
“Ndio ninakuamini”
“Hili  swala niachie mimi usiogope chochote, kwa kuwa hadi sasa hivi hakuna mgonjwa hata mmoja ambaye amefariki basi kuwa na amani moyoni mwako”
“Sawa”
Majira ya saa kumi na moja jioni shem Cajoli akarudi akiwa na begi kubwa la nguo pamoja na begi jengine la mgongoni.
“Jamani, sijapata ona, kwa hili pigo seriikali isipo fanya maamuzi magumu kwa ajili ya huu ugonjwa basi hadi kesho nchiwatu watakuwa na mapunye mwili mzima”
Shem Cajoli alizungumza huku akikaa kwenye sofa.
“Rafiki yako hapa anaogopa”    
 
“Anaogopa nini?”
“Anawaonea huruma wagonjwa?”
“Weee, shosti kwa hili dili mimi ninakuambia tunakwenda kuwa matajiri”
“Ila jamani tuangalie utu, watu wanateseka”
“Honey ila hayo si mateso ya muda mchache”
“Sawa, ila mwenzenu roho yangu inaniuma sana”
Taarifa nyingine ya habari ikatufanya kukatisha mazungumzo yetu na kuitazama.
“Uchunguzi ambao tumeufanya hadi sasa hivi kwa kusaidia na madaktari kutoka nchini Marekani, tumegundua kwamba ugonjwa huu unasababishwa na maji. Tunawaomba ambao bado hawajakubwa na ugonjwa huu. Wahakikishe kwamba maji wanayo kunywa wanayechemsha kuhakikisha vilemelea vya ungonjwa huu vinakufa”
Waziri wa afya alizungumza na waandishi wa habari ambao wamemzunguka. 
 
“Bado wamefeli”
Cajoli alizungumza na kutufanya tumtazame.
“Una maanisha nini wajina?”   
“Hawawezi kuwaua virusi kwa kuchemsha maji, kwa maana virusi wangu hawafi kwa mji ya moto”
“Ngoja tuangalie”
“Ila nina wazo moja”
“Wazo gani?”
“Nahitaji tujichome sindano za dawa ya hawa virusi hata tukiwa nje huko, kuna kupitiwa mtu unaweza ukanywa maji na kujikuta ukipata ugonjwa”
 
“Sawa”
“Shem nimekuja na make up ambazo ninahitaji kukufanyia kuibadilisha sura yako, hata ukikutana na watu ambao wanakujua washindwe kukufahamu kabisa”
“Kweli, hilo mume wangu unaweza kulifanya hata ukutane na raisi”
“Akutane na raisi!!?”
“Ndio nimemuambia kwamba akutane na raisi ili kumshirikisha juu ya ugunduzi wa hii dawa yake”
“Huoni kama inaweza kuwa hatari kwa shemeji?”
“Hapana hiyo ndio itakuwa safari moja wapo ya yeye kuwa kulipiza kisasi”
“Hilo analo lizungumza Cajoli ni swala muhimu sana. Shem tuanza hiyo kazi haraka iwezekanavyo.”
“Sawa”
 
Cajoli akaelekea maabara akarudi akwia na chupa yenye dawa ambayo inaweza kutusaidi kujikinga na maambukizi ya gonjwa hili jipya. Akaanza kumchoma sindano shem Cajoli kisha, akanichoma na mimi, kisha na mimi nikachukua jukumu la kumchoma sindano hii aliyo weka dawa. Shem Cajoli akaanza kazi ya kunifanya mautundu ya sura kwa ajili ya kunibadilisha. Zoezi la shem Cajoli likachukua zaidi ya masaa mwaili.
“Hembu jiangalie kwenye kioo”
Shem Cajoli akanikabidhi kioo, nikajitazama kusema kweli sura yangu imebadilika kwa kiasi kikubwa sana. Hotuba ya raisi K2 ikatufanya kuacha kila tunacho kifanya na kuitazama.
 
“Habari za muda huu Wananchi. Kila mmoja ninaamini atakuwa anafahamu ugonjwa huu ambao umeibuka nchini mwetu. Wanasiasa mbali mbali kutoka duniani, wamajaribu kuhakikisha kwamba wanafumbua dawa ya kuweza kuuzuia ila hadi wakati huu hakuna ambaye ameweza kutupatia jawabu la kuweleweka.
Nikiwa raisi nimeamua kufungua milango kwa madaktari wa tiba asili nao kujaribu kuliokoa taifa kwa maana ni mamilioni ya watanzania wanaugua gonjwa hili la hatari”
“BINGO”
Cajoli alizungumza kwa haraka huku akinyanyuka kwa kasi katika sofa na kunikumbatia kwa furaha kwa maana mafanikio ya mpango wetu yanazidi kufanikiwa kadri muda unavyo zidi kwenda.

AISIIIII……….U KILL ME 105                                                                                               

 “Wameingia choo cha kike”       
Nilizungumza huku nikiwa nimejawa na furaha sana moyoni mwangu.
“Honey kuna wao ambalo nimelipata”   
“Zungumza”
 
“Kwa kuwa serikali imesha amua kuchukua hadi madaktari wa tiba hasili, ili kwenda kulishuhulikia hili jambo, ninakuomba uwezekutafuta namba ya simu ya raisi ili uzungumze naye moja kwa moj”
“Namba ya raisi!!?”
Shem Cajoli aliuliza huku macho yakimtoka.
“Ndio ninahitaji azungumze na raisi. Moja amuhakikishie kwamba ana dawa ambayo anaweza kutibu ugonjwa huu. Pili aingie makubaliano ya kulipwa kiasi ambacho yeye atakihitaji”
Nikaka kimya kwa sekunde kadhaa huku nikifikiria jambo alilo lizungumza Cajoli.
“Inabidi nibadilishe sauti yangu”   
“Kwa nini shem?”
“Sauti yangu K2 anaifahamu vizuri sana, alisha wahi kuwa bosi wangu na nimedumu naye kwenye kazi hiyo kwa kipindi fulani hivi”
 
“Hilo la kubadilisha sauti honey ni jambo la muhimu sana. Kama itawezekana hii ndio itakuwa nafasi ya pekee kwetu kuwa mabilionea”
“Itawezekana, inabidi kuwasiliana na NSS, baada ya hapo wao ndio wanaweza kuniunganisha na raisi moja kwa moja”
“Kama inawezekana basi fanya hivyo mume wangu”
“Ile computer kule chini ina internert?”
“Ndio inayo”
“Twendeni”
Tukaelekea katika chumba kilichopo chini ya ardhi. Shem Cajoli akawasha computer. Nikaingia kwenye mtando wa NSS, nikaingiza namba za siri ambazo ni kupitia akaunti ya K2. Nikachukua namba ya sekretari katika kitengo cha mawasiliano. Nikamuomba shem Cajoli simu yake na kuingiza namba hizo na kumpigia sekretari.
 
“Tina kutoka NSS”
“Unazungumza na dokta Lameck, ninahitaji kuzungumza na raisi”
“Dokta Lameck unahitaji nini, hadi uzungumze na raisi?”
“Ametoa ofa kwa madaktari wa dawa za asili, ninahitaji kuzungumza naye moja kwa moja”
“Subiri”
Sikukata simu nikawa ninasikilizia anacho kizungumza sekretari huyu.
“Dokta Lameck raisi yupo hewani unaweza kuzungumza sasa”
“Habari yako muheshimiwa raisi”
“Salama ninazungumza na nani?”
“Ninaitwa dokta Lameck David, nipo mkoa wa Tanga, nimeona huu ungojwa pamojana hutoba yako. Tafadhali kama ulivyo zungumza ninaomba nafasi ya kuweza kutibu ugonjwa huu kupitia dawa yangu”
 
“Nita amni dawa yako inaweza kutibu?”
“Nina amini dawa zangu zinaweza kusaidia. Ila nitaifanya kazi hii kwa masharti mawili”
“Masharti gani?”
“Kwanza ninahitaji kuonana na wewe uso kwa uso, na uniandalie mgonjwa mmoja aliye athirika na huu ogonjwa, nimpatie dawa. Pili mgonjwa akipona, ili kulihudimia taifa nitahitaji serikali inilipe zaidi ya dola za Kimarekani Bilioni kumi, la sivyo sinto ifanya kazi hiyo”
 
Nikamshikia K2 akishusha pumzi nyingi, akakaa kimya kwa sekunde kadhaa nina amini anafikiria hili sharti langu la mwisho.
“Nimekubalina kuonana na wewe, na pia nimekubali kutoa kiasi hicho cha pesa. Sema ni saa ngapi tuweze kuonana hata kama ni usiku huu kazi hiyo iweze kuanza kufanyika mara moja”
“Muheshimiwa raisi kutokana nipo mkoa wa Tanga, ni vyema ukanitumia ndege mimi na timu yangu wa watu wawili. Wewe ndio utatuambia ni wapi tuweze kukuta na wewe”
 
“Ok nenda uwanja wa ndege hapo Tanga wewe na timu, mutachukuliwa katika ndege na moja kwa moja mutaeletwa hadi  ikulu”
“Sawa muheshimiwa raisi”
Nikakata simu na kuwageukia Cajoli.
“Tujiandae kwa safari, tunaelekea Dar es Salaam sasa hivi”
“Sawa”
“Ila honey huu kweli sio mtego?”
“Mtego kivipi?”
“Wanaweza kutuhisi kwamba sisi ndio tumetengeneza hawa virusi”
“Hakuna ambaye anaweza kutushuku katika hilo, kwa maana akili za viongozi wengi ni juu ya hili gonjwa”
“Wajina usiwe na shaka, endapo watatubadilika nchi hii tutaigeuza juu chini, chini juu”
“Umeona eheee”
“Yaa tujiamini na wala tusiwe na wasiwasi katika hili”
“Okay”
 
Tukaanza maandalizi ya haraka kuelekea jijini Dar es Salaam. Kichupa chenye dawa ya kutibu ugonjwa nikakiweka kwenye brufcase maalumu ambayo sio rahisi kwa kichupa hichi ambacho ni muhimu sana kuweza kuvunjika. Nikavaa suti nyeusi ambayo ameniletea shem Cajoli. Kila mtu alipo hakikisha kwamba tumemaliza kujiandaa. Nikabeba brufcase na kueleka kwenye gari.
“Dany utaendesha”
“Honey jina la Dany life kwa sasa, muzoee kuniita Dokta Lameck David”
“Sawa dokta tumekuelewa”   
Tukaingia kwenye gari, shem Cajoli akafungua geti, nikatoa gari nje, akafunga geti na kuingia kwenye gari na kuondoka hapa nyumbani kwake. Kutoka Kange hadi ulipo uwanje wa ndege ni muda wa dakika tano. Tukafika kwenye uwanja  wa ndege na kupokelewa na mkuu wa wilaya.
 
“Dokta Lameck David”
“Yes habari yako muheshimiwa?”
“Salama, nimepokea taarifa ya ujio wenu”
“Ndio, nilizungumza na muheshimiwa raisi muda mchache ulio pita. Maandalizi ya ndege yapo tayari”
“Shukrani muheshimiwa”
Sikuona haja ya kuwatambulisha Cajoli kwa mkuu wa wilaya. Kwa jinsi ya sura yangu ilivyo badilishwa na shem Cajoli pamoja na miwani hii niliyo ivaa ni ngumu sana kwa mtu kuweza kunitambua kwamba mimi ni gaidi ambaye wananitafuta kila kukicha. Tukaingia kwenye ndege ndogo ya abiria watano. Safari ikaanza taratibu kuelekea jijini Dar es Salaam.
“Siamini kama hili swala limekwenda kama tulivyo panga”
Cajoli alizungumza kwa sauti ya chini sana ambayo sisi peke yetu ndio tumemsikia, hata marubani waliopo mbele nina imani kwamba hawajasikia kitu chochote kile.
“Mungu ni mwema”
“Ila jamani tuwe makini”
“Usijali shemji kila jambo mutaniachia mimi tukifika ikulu, nyinyi wala musizungumze kitu cha aina yoyote”
“Sawa dokta”
 
Ndani ya dakika arobaini na tano, tukafika jijini Dar es Salaam. Jiji ambalo niliondoka miaka kadhaa nyuma kwa kujificha ficha. Uwanja wa ndege tukapolewa na msemaji wa ikulu  aliye jitambulisha mbele yetu kwa jina la Bwana Omary Saidi. Tukaingia kwenye helicopter ya ikulu iluyo kuja kutuchukua eneo hili kwa ajili ya kuepuka foleni pamoja. Taratibu helicopter ikashuka kwenye uwanja maalumu iliyopo hapa ikulu. Tukashuka kwenye helicopter, tukakaguliwa na walinzi wa hapa ikulu, kisha moja kwa moja tukapelekwa sehemu alipo raisi.
Tukaingia kwneye seble moja kubwa iliyo hapa ikulu, ambayo si mara yangu ya kwanza kuingia hapa. Kitu kilicho badilishwa kwenye hii seble ni thamani za ndani pamoja na rangi za ukutani tu.
“Muheshimiwa raisi atafika hapa ndani ya dakika tano kuna kikao ana kimalizia”
“Sawa”
 
“Labda muandaliwe kinywaji gani?”
“Hapana tupo vizuri”
Kama nilivyo walezea Cajoli, maswali yote wakaniachia mimi mwenyewe. Kweli baada ya dakika tano K2 na walinzi wake wawili wa kike wakafika ndani ya seble. Kwa heshima ikatubidi kusimama na kusalimiana naye. Kitendo cha kumpa mkono K2, hasira ikaanza kunipanda taratibu, mawazo ya mauaju ya familia yangu yakaanza kunijaa akilini mwangu.
‘Oohoo Mungu nisaidie’
Nilizungumza kimoyo moyo huku nikimtazama K2 usoni, huku nikiwa nimeachia tabasamu pana ila hasira ndio inafurukuta ndani ya moyo wangu.
 
“Karibuni”
“Asante muheshimiwa raisi. Ninaitwa dokta Lameck David. Huyu ni Cajol Lameck na huyu ni Cajoli Rajah”
“Ohoo ninashukuru kuwafahamu, huyu ni mke wako?”
“Ndio ni mke wangu na huyu ni shemeji yangu”
Sauti ambayo ninazungumza nayo hapa ni tofauti kabisa na sauti yangu ya kawaida ambayo K2 anaifahamu, cha kumshukuru Mungu nina uwezo mkubwa sana kwa kubadilisha sauti yangu na hata kipindi nilipo kuwa nimejibadilisha na kuwa msichana basi hakuweza kunifahamu kabisa.
 
“Karibuni sana wapendwa, hapa ndio ikulu "
“Asante muheshimiwa”
“Tunaweza kuzungumza kikao, sijui tuzungumzie hapa au ofisini kwangu”
“Popote tu muheshimiwa, kilicho tuleta hapa ni kuhakikisha kwamba dawa ambayo tumeitengeneza basi inaweza kwenda kukabiliana na ugonjwa huu mpya unao endelea kumiza mamilioni "
“Kweli hilo ndio jambo nilio penda kulisikia na ndio maana hata ulipo wasiliana nami niliweza kujawa na imani kubwa sana juu yako”
 
“Sawa muheshimiwa raisi, nitahakikisha kwamba hakuna jambo ambalo linakwenda kuharibika. Kikubwa ni kuanza kufanya majaribio ya haraka kwa mgonjwa ambaye ameathirika na huo ugonjwa”
“Mgonjwa yupo, na anasubiri matibabu yenu”
“Tunakuomba tumuone”
“Sawa”
Tukaondoka na raisi na kuelekea kwenye hospitali iliyomo humu ndani ya Ikulu. Tukaingia kwenye moja ya chumba, tukamkuta mtoto wa K2 akiwa hoi bin taabani.
 
“Huyu ni mwangu, huu ugonjwa ulimpata masaa matatu nyuma. Ujio wenu ninaimani mutamsaidia, hapa ninazunguma kama mama na si raisi. Dokta Lameck ninakuomba na timu yako kama kuna uwezekano wa mwangu kupona nitawaongezea mara mbili ya kiasi cha pesa ambacho mulikihitaji kutoka katika serikali yangu”
K2 alizungumza huku machozi yakimlenga lenga, nikatzamana na Cajoli, mwili mzima ukanisisimka baada ya kusikia maneno ya K2, hasira ya mauji ya mwangu pamoja na familia yangu ikaanza kunipanda mawazo ya kumuu mtoto wa K2 ikaanza kunijia kichwani mwangu taratibu na nikadhamiria kuhakikisha kweli leo ninaondoa maisha ya mtoto wa K2.

==>>ITAENDELEA KESHO
chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )