Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Wednesday, October 17, 2018

AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 106 na 107 )

juu
MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA- 0657072588
ILIPOISHIA   

Tukaondoka na raisi na kuelekea kwenye hospitali iliyomo humu ndani ya Ikulu. Tukaingia kwenye moja ya chumba, tukamkuta mtoto wa K2 akiwa hoi bin taabani.
“Huyu ni mwangu, huu ugonjwa ulimpata masaa matatu nyuma. Ujio wenu ninaimani mutamsaidia, hapa ninazunguma kama mama na si raisi. Dokta Lameck ninakuomba na timu yako kama kuna uwezekano wa mwangu kupona nitawaongezea mara mbili ya kiasi cha pesa ambacho mulikihitaji kutoka katika serikali yangu”
K2 alizungumza huku machozi yakimlenga lenga, nikatzamana na Cajoli, mwili mzima ukanisisimka baada ya kusikia maneno ya K2, hasira ya mauji ya mwangu pamoja na familia yangu ikaanza kunipanda mawazo ya kumuu mtoto wa K2 yakaanza kunijia kichwani mwangu taratibu na nikadhamiria kuhakikisha kwamba leo ninaondoa maisha ya mtoto wa K2.
   
ENDELEA   
“Nimekuelewa muheshimiwa raisi, tafadhali tungeomba nafasi ili kuweza kumtibu mwano”
“Hakuna shida mimi nipo tayari kukaa hata hapo nje ili mradi mwanangu aweze kupata matibabu na kupona”
“Sawa ila muheshimiwa raisi ninahitaji uweze kuitunza ahadi yako katika hili ulilo lizungumza”
“Usijali dokta Lameck”
“Okay”
 
K2 akatoka nje na walinzi wake. Nikautazama mlango baada ya kufungwa, nikataka kwenda kuufunga ila Cajoli akaniwahi kunishika mkono.
“Unataka kufanya nini?”   
“Nahitaji kuufunga mlango”
“Dokta Lameck”
Cajoli alizungumza kwa sauti ya chini huku akinisogelea karibu yangu
“Natambua kwamba una hasira kali na unakisasi cha kikali dhidi ya K2. Tafadhali ninakuomba utulie”
“Shem ni kitu gani kinacho endelea”
“Nipo sawa shem tuanzeni kazi”
Kila mmoja akachukua gloves nyeupe na kuzivaa viganjani mwake.
“Hapa hakuna kazi kubwa inatubidi kumchoma sindano huyu kijana”
Cajoli alitoa maelekezo huku mimi nikifungua brufcase na kutoa kichupa cha dawa. Nikamkabidhi Cajoli akaisingiza sindano na kuvuta dawa kidogo na kumchoma kijana huyu kwenye mkono wake.
“Itachukua dakika thelathini  kwa virusi wote kufa mwilini mwake.”
 
“Una uhakika na unalo lizungumza?”
“Yaa nina uhakika honey, tukae humu ndani ya hichi chumba hadi dakika hizo zitakapo kwisha”
“Sawa”
Kazi iliyo bakia kwentu ikawa ni kutazama saa ya ukutani jinsi inavyo zungusha mishale yake taratibu, kila nilipo jaribu kumtazama mtoto wa K2 roho ya kishetani na ya mauji inanikaba kooni mwangu huku moyoni mwangu nikisikia sauti mbili zikipingana, moja ikinihitaji nimuue mtoto wa K2 iwe njia moja ya kulipiza kisasi, huku roho nyingine ikinihitaji kuwa mvumilivu nichukue kiachi cha pesa alicho kizungumza K2 na niondoke zangu.
“Dokta”
Shem Cajoli aliniita na kunifanya nigeule, nikamkuta akiwa amesimama pembeni ya kitanda cha mtoto wa K2. Mapunye punye yote yoliyo kuwa mwilini mwake yote yametoweka. Amerudi katika hali yake kama kawaida.
“Mambo kijana”   
Cajoli alizungumza huku akimtazama mtoto huyu usoni mwake.
 
“Safi”
“Unajisikiaje?”
“Vizuri tu”
“Unaweza kushuka kitandani?”
“Ehee”
“Shuka”
Kijana huyu akashuka kitandani, Cajoli akamshika mkono na kumsimamisha mbele ya kioo kilichomo kwenye hichi chumba kijana, huyu  akaanza kujishangaa mwili wake jinsi ulivyo rudi katika hali yake ya kawaida.
“It’s me real”
“Yaa ni wewe”
“Mom”
Mtoto huyu akaita kwa nguvu na kuwafanya walinzi wa K2 kuingia kwa haraka ndani ya chumba hichi. K2 akaingia, alipo muona kijana wake amerudi katika hali ya kawaida, akamkimbilia na kumkumbatia kwa nguvu huku akimpiga mabusu mfululizo mashavuni mwake. Machozi ya asira yakaanza kunilenga lenga, upendo anao uonyesha K2 kwa mwanaye kusema kweli roho yangu ina niuma sana.
“Dokta Lameck asante sana”
K2 alizungumza huku machozi yakimwagika usoni mwake. Nikabaki kutabasamu tu kwa maana sihitaji kuzungumza, isije kinywa changu kikateleza na kuvuruga hali ya hewa bure.
 
“Mom nimepona”
“Yaa I see my son”
K2 akatuomba tutoke katika chumba chumba hichi. Moja kwa moja tukalekea katika ukumbi wa mikutano ambapo hapo tukakutana na madaktari wengine ambao wameshindwa kutengeneza dawa ambayo inaweza kuwaua virusi hawa wanao tesa mamilioni ya Watanzania.
“Munaweza kukaa”
K2 alizungumza huku akielekea kwenye kiti kilichipo mbele ya meza hii kubwa na ndefu yenye viti zaidi zaidi ya kumi kwa kila upande. Muhudumu katika ukumbi huu wa mkutano, akatonyesha viti vya kukaa katika hii meza. Taratibu tukaketi huku macho yangu nikiyapitisha pitisha kwa madaktari hawa ambao hakuna hata mmoja ambaye ninamtambua.
 
“Mabibi na mabwana, ninawatangazia kwamba dawa ya Virusi hivi vilivyo sambaa kwa maji, imepatikana kutana na dokta Lemeck David pamoja na timu yake”
Ikatubidi sote watatu kusimama ili watu waweze kutuona.
“Dokta Lameck David pamoja na timu yake, wameweza kugundua dawa ambayo. Nilijitolea kufanyiwa majaribio katika mwili wa mwanangu na kama munavyo weza kumuona, mwangu yupo salama kabisa na ana afya nzuri na amerudi katika hali yake ya kawaida.”
Madaktari wpte waliomo ndani ya ukumbi huu wakaanza kupiga makofi wakifurahia jambo kupatikana kwa dawa ambayo inaweza kuua virusi vinavyo endelea kuwatesa mamilioni ya Watu
 
“Kusema kweli ninayo furaha kutoka moyoni. Nikiwa kama mama ninaumia kuona watan wanateseka, watanzania wanasitisha kazi zao. Leo nimepokea taarifa juu ya ajali nyingi barabarani. Utakuta dereva anakunywa maji na kupata ugonjwa huu, mwisho wa siku anashindwa kabisa kuhimili gari kwa kuchanganyikiwa na anajikuta akipata ajali.  Kwa uvumbuzi wa dokta Lameck David, ningeomba sasa atupatie ufafanuzi wa hii dawa yake, pamoja na matumizi yake. Dokta Lameck David karibu sana”
K2 alizungumza akiwa na furaha sana, nikashusha pumzi taratibu huku nikiwa na tabasamu pana usoni mwangu ila laiti kama mioyo yetu inge kuwa inaonekana kwa nje, basi K2 asinge niruhusu hata nimkaribie karibu yake. Taratibu nikasimama huku nikiwawazama madaktari katika chumba hichi.
 
“Habari za usiku”
Watu wote wakaitikia, nikaliweka vizuri koti langu la suti kisha nikajikoholesha kidogo na kuiweka miwani yangu sawa ili mradi yote ni madoido ya kulisoma eneo la humu ndani.
“Kama muheshimiwa riasi alivyo weza kutanguliza utambulisho wetu, basi si vyema nikalisema jina langu kamili. Ninaitwa dokta Lameck David Alimeida, ni mtanzania halisi ila nimeweza kusoma inchini India, na nimesomea maswala ya udaktari na ugunduzi wa madawa. Wiki moja iliyo pita niliweza kuingia nchini Tanzania, nikitokea India, nikiwa nimemaliza miaka tisa ya kusomea maswala ya ugunduzi wa dawa za magonjwa sugu kama HIV, EBOLA, na kadhalika.”
Nikanyamaza kidogo na kuiweka sawa miwani yangu, kwani kitu ninacho kizungumza vyote ni uongo mtupu na laiti wangejua kwamba sisi ndio chanzo cha virusi hawa wasinge kubali hata kukaa meza moja na mimi.
 
“Leo asubihi nilipo weza kuona ugonjwa huu wa kutisha, ikanilazimu mimi na timu yangu kuweza kuanza harakati za kutengeneza dawa ambayo itaweza kuokoa maisha ya mamilioni ya Watanzania. Tulipo hakikisha kwamba tumefanikiwa kutengeneza dawa hii kwa haraka iwezekanavyo, niliweza kuchukua jukumu la kumpigia raisi simu, huku nikiwa tayari nimesha fanya jaribio kwa mgonjwa mmoja ambaye ni jirani kabisa na sehemu ninayo ishi.”
 
“Ninamshukuru mama hapa, muheshimiwa raisi kwa kuweza kuwa msikivu, Mungu aliweza kumuongoza, na kutukubalia vijana wake kuja kufanya hichi ambacho tayari tumesha kifanya. Nilikaa na timu yangu nikaona kwamba dawa hii tuipe jina la K2, jina la raisi wetu, kwa maana ni mama shupavu na ni mama ambaye ninaimani atalifikisha mbali taifa letu”
 
Ukumbi mzima ukalipuka kwa makofi, laiti kama watu wengeruhusiwa kupiga vigelele gele basi wangepiga kwa shangwe sana. Yote niliyo yazungumza yanatoka kinywani mwangu na si moyoni mwangu, nimeyazungumza kuhakikisha kwamba ninazidi kuiteka akili ya K2 pamoja na watu wake.
 
“Ohoo this is real suprize, sikutarajia kama dokta Lameck unaweza kuipa dawa yako jina langu”
“Yaa ninakuomba ulipokee kwa mikono yote muheshimiwa raisi”
“Sawa, mimi sina kipingamizi katika hilo. Dokta Lameck nafani ni yako sasa, kuunda timu yako itakayo fanya kazi chini yako kuhakikisha kwamba untengeneza dawa nyingi nyingi za kuwaponya wagonjwa”
 
“Nashukuru muheshimiwa raisi kwa cheo hicho. Ila ninawazo moja kubwa, ambalo linaweza kuifanya Tanzania kupona kwa wakati mmoja na kama si wakati mmoja basi watapishana kwa dakika kadhaa tu”
“Zungumza tu dokta Lameck”
 
“Kutokana ugonjwa huu umeenea kwa maji,basi tunataka maji hayo kuweza kuyaweka dawa yetu, na itakwenda kuua virusi wote ambao wapo kwenye hayo maji na hii itakuwa ni njia raisi kwako muheshimiwa raisi kuwatangazia wananchi kwamba maji wanayo yatumia ni salama na ni dawa kwao”
“Your so real genius. Sijui siku zote ulikuwa wpai kijana mwenye akili kama wewe?”
 
“Nilikuwa India”
Jibu langu likawafanya watu wote ndani ya ukumbi kucheka,hata K2 mwenyewe akacheka sana.
“I real like you dokta Lameck. Okay, madaktari wote sasa hivi mutakuwa chini ya dokta Lameck, mutahakikisha kwamba munafanya naye kazi kwa usihirikiano kuhakikisha kwamba hadi inatimu saa moja asubihi basi kila jambo lipo kwenye mstari na huu ungonjwa, utakuwa ni historia kwenye nchi yetu”
 
“Sawa muheshimiwa”
“Dokta Lameck na timu yako ninawaomba tuongozane”
Kikao kikaishia hapo, huku moyoni mwangu nikiwa nimejawa na matumaini makubwa sana ya ushindi katika ulipizaji wa kisasi. Tukaingia na raisi ofisini kwake.
“Nimeona niwatangulizie nusu ya pesa, ili muweze kupata nguvu ya kufanya kazi”
 
“Sawa, muheshimiwa tutashukuru sana”
K2 akachukua mkonga wa simu iliyopo mezani mwake, akaminya minya namba kadhaa kisha akapiga simu.
“Habari yako mkurugenzi”
“Ninahitaji muweze kuingiza pesa katika akauti nitakayo kutumia dakika chache kuanzia hivi sasa. Na nitahitaji muingizi dola za kimarekani bilioni kumi”
“Sihitaji msawali fanya kama nilivyo kuagiza”
K2 akakata simu na kuirudisha sehemu alipo itoa.
“Watanzania bwana, mtu umemueleza kitu cha kueleweka, ila bado anahoji msawali”
K2 alizungumza huku akitutazama kwenye nyuso zetu.
“Ndio nchi yetu muheshimiwa raisi”   
Cajoli alijibu.
 
“Kweli Cajoli si ndio?”
“Ndio”
“Ninaomba munipatie namba ya akaunti yenu”
Cajoli akataja namba yake ya akaunti, K2 akaituma kwa mkurugenzi wa benki. Ndani dakika tano meseji  ikaingia kwenye simu ya Cajoli akatuonyesha sote. Nilihisi kuchanganyikiwa kwa furaha kwa maana kwenye maisha yangu sikufikiria kumiliki kiasi kikubwa cha pesa kama hichi.
“Mukiifanya hii kazi, ninawahakikishia hiyo pesa nyingine ninawaongezea kutoka mfukoni mwangu mimi mwenywe”
“Sawa muheshimiwa raisi”
“Ngoja sasa niwapeleke maabara”
Tukatoka katika ofisi ya raisi akatupeleka kwenye maabara. Akatuacha ndani ya maabara kwa ajli ya kuanza kuifanya kazi yetu. 
 
“Shem jamani nina ushauri”
“Ushauri gani?”
“Ninakuomba Cajoli hiyo pesa uweze kuihamishia kwenye akaunti nyingine, isije ikatokea ikarudishwa, tukawa tumefanya kazi bure”
“Kweli, ngoja niiweke kwenye akaunti yangu ya Dubai”
“Sawa”
Cajoli akaanza kuminya minya simu yake. Baada ya dakika tano akanyanyua uso wake ulio jaa tabasamu pana sana.
“Dubai wamekubali kuipokea pesa yangu na kuiingiza kwenye akaunti yangu”
“Kumbe huwa wanasumbua sana?”
“Sana, mara nyingi wanahofia kuingiziwa pesa za ufisadi na kuchafua jina la nchi yao”
“Hapo kweli, sasa nitahitaji tuandae chupa za maji ishirini na nne. Kila chupa tuweze kuweka dawa, baada ya hapo chupa zote nitahiji tumuombe muheshimiwa raisi aweze kuzisambazo chupa hici kwenye vyonzo vyote vya maji”
“Sawa dokta”
 
Kabla hatujaanza kufanya jambo lolote, mlango wa maabara ukafunguliwa. Wakaingia wanaume wawili walio jazia miili yao kwa mazoezi huku wakiwa wamevalia sare za jeshi. Wakaniangalia kisha mmoja akazungumza kwa sauti nzito.
“Dokta Lameck David Almeida ongozana na mimi”
Mapigo ya moyo yakaanza kunienda kasi, nikamtazama Cajoli, ninamuona kabisa amejawa na wasiwasi unao pelekea hadi kuanza kulengwa lengwa na machozi.
                                                                                         
AISIIIII……….U KILL ME 107                                                                                              

“Usijali, honey ninakuja. Endeleeni na kazi ambayo nimewaachia”
“Sawa doktar”
Shem Cajoli alinijibu, nikatoka ndani ya maabara na kuongozana na wanajeshi hawa ambao mmoja ametangulia mbele huku mmoja akiwa nyuma yangu. Sikuhitaji kufahamu kwamba ninapelekwa wapi pia sikuhitaji kuonyesha wasiwa wangu usoni. Tukaingia kwenye moja ya ofisi, nikakuta  wakuu wa jeshi wapatao sita wakiwa na vyeo vya juu kabisa.
“Kaa pale” 
       
Mwanajeshi mmoja niliye kuja naye alizungumza huku akinitazama usoni mwangu. Taratibu nikatembea hadi kwenye kiti walicho niomba nikae kisha wanajeshi hawa wawili wakatoka ndani ya ofisi na kuniacha na walinzi hawa.
“Habari yako dokta Lameck David?”
 
“Salama tu”
“Tunatambua machango wako katika katifaa, muda mchache tumeweza kuangalia kikao chako ulicho kuwa unazungumza na raisi pamoja madaktari, ila tunakuomba kukuhoji maswali mawili matatu kama huto jail”
Mzee mmoja mweusi alizungumza huku akiwa amenikazia macho usoni mwangu. Kwa kujiamini nikaanza kutazama kila sura ya kiongozi hawa wa jeshi waliomo humu ndani, kisha nikashusha pumzi kimya kimya pasipo mtu yoyote kuweza kugundua kwamba ninaouondoa wasiwasi wangu moyoni mwangu.
 
“Kabla hujaniuliza swali lolote muheshimiwa. Ningependa kufahamu kwamba kikao hichi raisi anakifahamu?”
Wakuu hawa wajeshi wakatazamana kisha mzee ambaye ndio muongeaji tangu nifike humu ndani akanijibu.
“Ndio raisi anakitambua hichi kikao”
“Ningeomba nizungumze naye kwenye simu ili niweze kukubaliana nanyi kwa kile munacho kizungumza”
“Kwa nini unahitaji kuzungumza na raisi?”
Mzee mwengine alizungumza baada ya kuona ukimya ulianza kuchukua nafasi yake.
 
“Nimekuja hapa kwa mamlaka ya raisi, nilizungumza naye kwenye kikao na amenipa majukumu ya kufanya. Mmekuja kunichukua nikiwa katikati ya kazi ambayo nimekabidhiwa na raisi, ndio maana nikahitaji kuzungumza na raisi”
“Dokta Lameck tulikuita hapa kwa dakika japo tano, tulihitaji kuhoji maswali mawili matatu”
 
“Siwezi kujibu maswali yenu pasipo idhini ya muheshimiwa raisi kwa hiyo ninawaomba munirudishe kule mulipo nitoa nikaendelee na kazi yangu kwa maana timu yangu haiwezi kufanmya kazi pasipo mimi”
Wazee hawa wakaka kimya kwa maana akili zao nilisha zisoma kwa haraka sana ndio maana nikaamua kuwakatisha kwa kigezo cha kuhitaji kupata jibu kutoka kwa raisi, kutokana na kikao hichi kuto kuwa na uhalali wowote.
“Munaweza kuingia”    
 
Mzee ambaye alikuwa ni mzungumzaji alizungumza kwa sauti ya msisitizo huku akiwa ameminya batani kwenye simu iliyopo juu meza. Wakaingia wanajeshi ambao walinileta humu ndani.
“Mrudisheni maabara”
“Sawa mkuu”
Nikanyanyuka kwenye kiti nilicho kalia, moja kwa moja nikaongozana na wanajeshi hawa nilio kuja nao. Moja kwa moja tukarudi maabara na kuwakuta Cajoli wakinisubiria. Wanajeshi hawa walipo funga mlango na kuondoka, Cajoli akanifwata kwa haraka na kunikumbatia kwa nguvu huku akiwa amejawa na furaha.
 
“Wamekuambiaje?”       
“Nilikutana na viongozi wa jeshi walihitaji kunihoji maswali ila nikakataa kuhojiwa”
“Umekataa!!?”
“Ndio nimekataa kutokana sio kikao rasmi”
“Kivipi shem?”
“Ni kikao ambacho kimeitishwa na viongozi hao wa jeshi, ila raisi alikuwa hakifahamu”
“Hapo umefanya jambo la muhimu sana mume wangu. Sasa tumesha weka dawa katika chupa zote ambazo ulihitaji tuziweke maji. Zipo tayari kwa kutumika”
“Tunahitaji kuzungumza na raisi sasa, tumuambia kwamba kazi imekwisha kilicho baki ni dawa hii kusambazwa kwenye vyanzo vyote vya maji mikoani mwote”
“Sawa”
“Ngoja nikazungumze naye”
“Sawa”
 
Nikafungua mlango wa maabara na kutoka, nikamuuliza mlinzi mmoja sehemu ambayo ninaweza kumuona raisi. Akaniomba niongozane naye hadi kwenye ofisi, akazungumza na walinzi wa raisi, mmoja akaingia ndani ya hii ofisi iliyo tengenezwa kuta zake kwa vioo. Idadi ya viongozi waliomo ndani ya ofisi hii ninao waona kwa nje wanafika kumi na tisa, wengi wao wamevalia mavazi ya jeshi, huku ni wachache sawa ndio wamevalia suti. Nikamuona mlizi wa raisi akimnong’oneza K2 masikioni. K2 akanitazama kisha taratibu akanyanyuka kwenye kiti na kutoka nje na mlinzi wake.
“Ndio dokta Lameck”
 
“Kazi imakamilika muheshimiwa raisi”
“Dawa mumetengeneza katika muundo gani?”
“Muundo wa maji, ambayo yatamwagwa katika vyanzo vyote vya maji kwa kila mkoa, na maji hayo yatakapo samba, yataua kila kirusi kinacho patikana kwenye maji na wananchi wakitumia baada ya nusu saa watapona”
“Safi sana daktari basi itabidi chupa hizo zikabidhiwe kwa wakuu wa mikoa na kazi ianze kufanyika usiku huu huu”
“Ni kweli muheshimiwa”
“Ninashindwa kuongozana na wewe kwa maana nina kikao muhimu sana, nchi ipo katika kushambuliwa?”
 “Kushambuliwa?”
“Ahaa wewe ni daktari haya ni mambo ya ulinzi zaidi, kwa hiyo sio vyema nikakuelezea”
 
“Sawa ila kama kutakuwa na mbinu yoyoyote ya kuwasidia ninaweza kuwasaidia”
“Hakuna tatizo. Anjelina ongozana na daktari Lameck hadi maabara atakupa kazi ya kufanya. Ukimalizia hakikisha munawapeleka yeye na timu yake katika chumba cha kupumzikia”
“Sawa muheshimiwa raisi”
Nikaongozana na mmoja wa walinzi wa raisi moja kwa moja tukaelekea  hadi kwenye maabara, nikampa maelekezo ya kitu gani kifanyike akatii.
“Raisi ameniambia kwamba nchi ipo katika kushambuliwa”
“Ipo katika kushambuliwa, kivipi?”
“Hakuniambia kwa undani sana, ila kutokana tumeshapata mkwanja wetu ambao tuliukusudia kilicho baki ni kurocha rocha”
 
“Ndio nini shem?”
“Kuondoka”
“Hahaa haki ya Mungu kumbe shem una maneno ya kihuni namna hiyo?”
“Furaha tu”
“Tunaweza kwenda chumba cha mapumziko”
Mlinzi wa K2 alizungumza, tukatoka naye na kuongozana naye kweneye kordo zilizopo humu ndani ya ikulu. Kitu ambacho kinanishangaza ni hekaheka za wafanyakazi wa ikulu. Kila mmoja anaonekana kuwa bize sana usiku wa siku ya leo.
“Kuna kitu gani kinacho endelea dada?”
“Hakuna kitu dokta”
“Kweli dada?”
 
“Ndio daktari, nilicho agizwa ni kuwapeleka katika chumba cha kupumzikia na hapo munaweza kumsubiri raisi”
Angelina alizungumza kwa sauti ya msisitizo na kutufungulia katika chumba ambacho amegizawa tuweze kuwepo. Chumba hichi telvishion kubwa, masofa pamoja na friji kubwa.
“Tunashukuru”
“Karibuni sana”
Angelina alizungumza na kuondoka, shem Cajoli akajitupa kwenye kitanda huku akiwa na amechoka.
“Tumesha kuwa mabilionea jamani. Huu siamini”
Shem Cajoli alizungumza huku akijilaza vizuri kwenye sofa alilopo.
“Mungu ni mwema, ninaamini mimi na mume wangu hapa tunakwenda kufunga bong…………”
Cajoli hakumalizia sentensi yake, soite tukajikuta tukistushwa na mtetemesho mzito wa ardhi.
“Ni nini hicho mume wangu”
Cajoli alizungumza huku akinikimbilia na kunikumbatia.
“Lala kwenye sofa”
 
Nilizungumza huku nikimlaza Cajoli kwenye sofa.
“Ninawaomba munisubirie hapa hapa ninakuja”
“Dany”
Cajoli aliniita jina ambalo hatukukubaliana kuniita, sikumjibu kitu chochote zaidi ya kuufunga mlago kwa nje. Kila mtumishi wa ikulu, anakimbia kuelekea anapo pafahamu yeye. Walinzi wa raisi nao wapo bize katika kukatiza kila kona ya hii ikulu, ikiashiria kwamba hali kwa sasa ipo mbaya.
“Dada, dada, dada kuna nini huko nje?”
Nilimuita dada mmoja huku nikimshika mkono kwa maana yupo katika harakati za kuyaokoa maisha yake.
“Magaidi, magaidi”
“Wapo wapi?”
“Waneivamia ikulu”
“Mungu wangu!!”
Nilijikuita macho yakinitoka, kwa haraka nikarudi ndani ya chumba ambacho nimewaacha Cajoli na shemeji.
“Tunatakiwa kuondoka hili eneo sasa hivi”
 
“Kuna nni huko nje Dany?”
“Ikulu imevamiwa na magaidi”
“Imevamiwa na magaidi?”
“Ndio, hatuna muda wa kuzungumza, tutafute njia ya kuondokea hapa ikulu haraka iwezekanavyo”
Nilizungumza huku jasho likinimwagika usoni mwangu. Taratibu nikaanza kutembea kwa mwendo wa tahadhari hadi mlangoni. Nikaufungua mlango na kuchungulia nje, nikaona watu walio valia nguo nyeusi wakipambana na kikosi cha walinzi wa raisi.
“Jificheni nyuma ya masofa hakikisheni munanisubiria hapo”
“Shemeji ninakuomba twende wote”
“Hapana baki na Cajoli”
“Shemeji mimi nipo vizuri sana kwenye maswala ya upambanaji kwenda peke yako inaweza kuwa hatari sana kwako”
 
“Ok Cajoli baki hapo sawa?”
“Sawa”
Cajoli alinijibu huku machozi yakimwagika usoni mwake. Kitu nilicho kigundua kwa mke wangu, ni mwepesi sana kwenye swala la kumwagikwa na machozi. Tukatoka na shem Cajoli na kuanza kutembea kwa tahadhari kwenye kordo hii, huku macho yetu yakiangaza huku na kule kutafuta bunduki kwa maiti yoyote ambayo imepigwa risasi. Nikabahatika kupata bastola mbili, kutoka kwa mlinzi mmoja wa raisi niliye mkuta ameuwawa.
“Chukua hii”   
Nilizungumza huku nikimkabidhi shem Cajoli bastola mmoja, taratibu tukaanza kutembea kwa kunyata na kwa umakini katika hii kordo.
 
“Shem tunakwenda wapi?”
“Kumtafuta K2”
“Shem ngoja kwanza, K2 ni wa kazi g
ani kwa sasa. Kwa nini tusitafute njia ya kuondokea humu ndani”
“Cajoli huu ndio muda wangu wa kuhakikisha kwamba ninaiondoa roho ya K2, sina nafasi nyingne nitakayo ipata kwenye maisha yangu zaidi ya hii”
Nilizungumza kwa msisitizo huku nikiwa nimekazia macho shem Cajoli, usoni mwake, hakuwa na cha kubisha zaidi ya kutingisha kichwa kukubali kwa kile nilicho kizungumza mimi.

==>>ITAENDELEA KESHO
chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )