Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, October 18, 2018

AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 108 na 109 )

juu
MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA- 0657072588
ILIPOISHIA   
Nilizungumza huku nikimkabidhi shem Cajoli bastola mmoja, taratibu tukaanza kutembea kwa kunyata na kwa umakini katika hii kordo.
“Shem tunakwenda wapi?”   
“Kumtafuta K2”
“Shem ngoja kwanza, K2 ni wa kazi gani kwa sasa. Kwa nini tusitafute njia ya kuondokea humu ndani”
“Cajoli huu ndio muda wangu wa kuhakikisha kwamba ninaiondoa roho ya K2, sina nafasi nyingne nitakayo ipata kwenye maisha yangu zaidi ya hii”
Nilizungumza kwa msisitizo huku nikiwa nimekazia macho shem Cajoli, usoni mwake, hakuwa na cha kubisha zaidi ya kutingisha kichwa kukubali kwa kile nilicho kizungumza mimi.
           
ENDELEA       
Tukaendelea kusonga mbele kuhakikisha kwamba ninampata K2, sehemu tulipo hijika kuua na kupambana na magaidi hawa ambao hadi sasa hivi sifahamu wametokea wapi na wala wametumwa na nani, ilitubidi kupambana kuyaokoa maisha yetu. 
 
“Dany sidhani kama raisi anaweza kuwa hapa”
Shem Cajoli alizungumza huku jasho likimwagika usoni mwake.
“Turudi”   
Tukaanza kukimbia kwenye kordo hii ndefu huku tukiwa katika sana. Tukafika katika chumba ambacho tulimuacha Cajoli. Kila mmoja wasiwasi mwingi ulianza kupata baada ya kukuta chumba kikiwa kitupu kabisa.
“Cajoli”
Nilianza kuita huku nikiwa nimechanganyikiwa sana, tukawa tunasaidiana na shem Cajoli kumtafuta mke wangu ila hatukupata mafanikio yoyote. Hatukutaka kubaki ndani ya chumba hichi tukatoka na kueleka katika baadhi ya vyumba ambavyo tunahisi kwamba tunaweza kumpata Cajoli ila hatukufanikiwa kuweza kumpata.
Tukiwa katika kutafuta tafuta kwenye hivi vyumba, jeshi la ulinzi wa taifa likafika ikulu na kuwadhibiti magaidi ambao wamesalia katika ikulu.
 
“Dokta Lemeck David”       
Mkuu wa jeshi alinifwata huku akionyoosha mkono wake mbele.
“Ndio muheshimiwa”
“Ninaitwa generali Dickson Konzo. Kwanza tunaomba pole kwa kila jambo ambalo limejitokeza kwa wakati huu”
“Shurani muheshimiwa”
“Muheshimiwa raisi alitutuma tuweze kuja kukuchukua katika eneo hili wewe pamoja na timu yako na ninamshukuru Mungu kwamba tumefanikiwa kukukuta hai”
“Ni kweli, ila mke wangu hadi kwa sasa sijaweza kumuona”
“Timu mzima, hakikisheni kwamba munatafuta kila eneo kuhakikisha kwamba tunampata mke wa doka Lameck David, ana asili ya kiarabu”
Generali Dickson Konzo alizungumza kupitia simu yake ya upepo kufikisha ujumbe kwa vijana wake alio kuja nao katika eneo hili la ikulu.
“Muheshimiwa raisi anatusubiria kwenye kambi yetu ya jeshi”
“Sawa generali, ila siwezi kuondoka eneo hili hadi niweze kumpata mke wangu”
“Mke wako atapatikana, kikubwa ni kwenda kusikiliza wito wa raisi kwa kile anacho kuitia”
 
Tukatazama na shem Cajoli, akatingisha kichwa chake akiniomba nikubaliane na kile alicho kizungumza mkuuw a kikosi hichi kilicho kuja nacho hapa.
“Ninakuomba unahakikisha kwamba unamtafuta mke wangu popote pale alipo”
“Sawa dokta Lameck tutahakikisha kwamba mke wako anapatikana”
“Shukrani”
Tukaongozana na wanajeshi wanne, tukaingia kwenye gari nyeusi aina ya Hammer, ambazo nyingi zinatumiwa na wanajeshi. Katika gari letu kuna wanajeshi wawili walio kaa siti ya mbele huku nyuma kukiwa na gari jengine la jeshi likitusikindikaza katika safari hii. Safari ya kuepelekwa kwenye kambi ambayo hadi sasa hivi hatuitambui ikaanza.  Tukapia katika daraja la Kigamboni, hapo ndipo nikaelewa ni wapi tunapo elekea, tukiwa katikati ya daraja hili, kwa mbele tukaona gari mbili nyeusi zikitufwata kwa kasi.
 
“Dereva vipi?”
Niliuliza huku nikimtazama dereva wa huli gari.
“Hizi gari wala zizielewi”
Dereva huyu alizungumza huku mwili ukimtetemeka sana, nikashindwa hata kuelewa kama huyu ni mwanajeshi wa namna gani. Dereva wa gari letu akafunga breki za gafla, gari lililopo nyuma yetu, likatupita kwa pembeni na kutangulia.  Cha kushangaza gari mbili zilio kuwa zinakuja mbele yetu kwa wmendo wa kasi zikasimama na kugeuza kuelekea tunapo elekea sisi.
“Hawa ni NNS”
 
Dereva alizungumza kwa sauti iliyo jaa utetemeshi mwingi sana. Taratibu nikashusha pumzi huku kwa mkono wa kulia nikimshika shem Cajoli ambaye muda wote yupo kimya sana. Tukafika kwenye kambi ya jeshi iliyopo hapa Kigamboni. Tukasindikizwa kwenye ukumbi wa mikutano na kumkuta raisi pamoja na walinzi wake, huku kukiwa na wakuu wengine wa jeshi.
“Karibu dokta Lameck”
K2 alizungumza akiwa na tabasamu usoni mwake.
“Shukrani muheshimiwa raisi”
Nikaka kwenye moja ya kiti, kisha shem Cajoli naye akaka kiti cha pembeni yangu. 
 
“Dokta Lameck nimeshauriana na wakuu wa jeshi hapa, tukaona ni vyema tukushirikisha katika hali hii ambayo inaendelea hapa
K2 alizungumza huku akinitazama uosni mwangu. Nikabaki kimya nikiendelea kumsikiliza kwa umakini sana.
“Tanzan, katika siku chache zilizo pita, tuliingia katika mfarakano wa kidiplomasia na nchi ya Somali. Tatizo kubwa lililo tokea kati yetu sisi na Somalia, ni tukio la inchi ya Somalia kumtunza gaidi ambaye siku zote tulikuwa tunamtafuta kwa udi na uvumba”
 
Tv kubwa iliyopo katika chumba hichi cha mikutano ikaonyesha picha yangu kipindi nipo katika kiosi cha Al-Shabab. Mwili mzima ukaanza kuzizima huku mapigo ya moyo yakinienda mbio sana, kitendo hichi shem Cajoli aliweza kukistukia kwa haraka sana na kujikuta akinifinya taratibu pasipo mtu yoyote kutuona.
“Jina lake anaitwa Daniel, alikuwa ni miongoni mwa wasaidizi wangu katika kikosi cha NSS. Kwa hapo awali alikuwa ni kijana mzuri sana, mwenye werevu na msikivu. Ila alibadilika gafla, na kuwa miongoni mwa magaidi ambao ni hatari sana Afrika”
 
Maneno ya K2 yakaanza kunipandisha hasira taratibu hadi nikajikuta nikianza kukunja vidole vyangu vya miguuni taratibu japo nimevaa viatu vinavyo bana ila vidole vinamejikunja pasipo kupenda.
“Hii ni video ambayo inamuonyesha Dany akiwa katika mpango wa kulipua Tanz kwa bomu la nyuklia”
Video ikaanza kuonekana kwenye tv hii kubwa. Kitu kinacho nishangaza Dany ninaye muona kwenye hii video anafanana kabisa na mimi, sauti ni kama mimi, pembeni yake amesimama baba Hawa, pamoja na Hawa mwenyewe.
 
“Tanzani, ujumbe huu ninautuma kwa muheshimiwa raisi. Umeweza kuua vijana wangu katika uongozi wa raisi aliye pita kwa ukatili mkubwa sana. Nikaka kimya na kuiheshimu nchi yako kutokana ndio nyumbani kwangu nilipo zaliwa. Ukaona haitoshi, ukaua vijana wangu wengine ambao hawakuwa na mpango na wowote na nachi yako japo walikuwa wamejificha katika mapango ya Amboni kwa ajili ya usalama wao na mafunzo yao binafsi lakini wewe ukaingilia na kuwatekeza wanajeshi wangu hao. Hivyo basi muheshimiwa raisi K2 ifikapo tarehe kumi na mbili mwezi huu, tutahakikisha nchi yako itateseka na bomu la nyuklia litakwenda kulipuka majira ya saa sita mchaba baada ya wananchi wako kuteseka na kuumia vya kutosha.”
 
Nikajikuta nikishusha pumzi na kujiuliza Dany huyu ninaye muona kwenye hii video ametokea wapi na imekuwaje Al-Shabab wamemtumia mtu anaye fanana na mimi katika kuhitaji kutekeleza azimio lao.
“Magaidi hawa, tayari wao ndio wamesababisha virusi hawa kwa kutumia maji, na tunashukuru sana dokta Lameck David kwa kuweza kutuletea dawa, na nimepata ripoti muda mchache ulio pita kwamba wananchi walio anaza kutumia maji hayo wamepata nafuaa na wengine wamepona kabisa.”
“Asante muheshimiwa raisi kwa hilo”
“Sawa, katika mazungumzo yako uliniambia kwamba wewe ni daktari ambaye ni mgunduzi katika maswala ya madawa”
“Ndio muheshimiwa”
“Tunahitaji kufahamu ni madhara gani ambayo yanaweza kutokea baada ya bomu hili la nyuklia ambalo kesho saa sita kamili mcha hapa linaweza kulipuka, na kuathiri wananchi wengi sana”
 
“Muheshimiwa raisi, umeshasema kuna madhara makubwa sana ambayo yanaweza kutoke kwa wananchi wengi wa Dar es Salaam. Madhara makubwa ni vifo vya wananchi wasio na hatia”
“Nahisi hujanielewa doka Lameck, lengo langu na nia yangu ni kwamba ni dawa gani ambayo tunaweza kuitumia pale bomu litakapo kuwa limelipuka, na wananchi walio salia wakaweza kutibiwa na hiyo dawa”
Nikajikuta nikishusha pumzi, kabla sijazungumza kitu chochote, shem Cajoli akanikanyaga mguuni na akaanza kuzungumza yeye.
“Muheshimiwa raisi hilo swali ninaomba nilijibu mimi, kwa maana hapa kichwa cha daktari wangu ninakiona hakipo sawa kutokana na kutoweka kwa mke wake”
“Unaweza kujibu tu Cajoli”
 
“Ili tuweze kugundua dawa hiyo ni lazima tuweze kujua bomu hilo litakuwa limechanganywa na kemikali za aina gani, tukisha lifahamu hilo basi tunaweza kuingi maabara na kutengeneza dawa hiyo”
“Kweli muheshimiwa kama alivyo seme Cajoli ni lazima tuweze kugundua ni kemikali gani zimetumika katika bomu hilo. Pili kwa nini bomu hilo lisitafutwe na kuteguliwa kama inawezekana, kuliko kusubiria mamilioni ya watu wa Dar es Salaam yawakute matatizo ndio sisi tutengeneze dawa?”
Ukumbi mzima ukaka kimya huku viongozi hawa wakitafakari cha kuzungumza.
“Upelelezi na uchunguzi unaendelea kuweza kugundua ni wapi bomu hili litategwa”
 
‘Muheshimiwa raisi kuna video nyingine’
Simu maalumu  iliyopo mezani ilisikika ikizungumza, ikatubidi kukaa kimya, K2 akachukua rimoti mezani na kuiwasha Tv hii. Nikastuka sana baada ya kumuona Cajoli kwenye video hii akiwa amefungwa kwenye kiti huku akiwa amechuruzikwa na damu nyingi usoni mwake. Akasimama Dany huyu feki huku akitabasamu
“Kwenye ikulu yako tuligundua kwamba kuna mtu muhimu sana ambaye kupitia yeye basi tunaweza kubadilisha mawazo yetu. Tunamuhitaji dokta Lameck David ndani ya masaa mawili kuanzia hivi sasa, likishindikana hili basi mke wake na nchi nzima itaingia kwenye anguko”
Video hiyo ikaishia hapo, jasho jingi likaanza kunitiririka, nikasimama kwenye kiti nilicho kalia na kuwafanya watu wote kunitazama. Shem Cajoli akasimama, akanishika mkono.
“Samahani waheshimiwa ninaomba nizungumze na shemeji yangu mara moja”
 
Tukatoka katika chumba hichi, tukatafuta sehemu ambayo hakuna kamera ya ulinzi na kusimama.
“Shem shem hembu tulia”   
Shem Cajoli alizungumza huku akinishika mashavuni mwangu na kunifanya nimtazame usoni mwake.
“Kuna kitu ambacho kinaendelea hapa, siwezi kuamini huyu Dany ametokea wapi?”
“Shii shem usizingumze kwa sauti kubwa ambayo inaweza kusikika”
“Cajoli mbona nahisi kuchanganyikiwa”
“Shemmmmm nisikilize, vuta pumzi na uishushe taratibu”
Nikafanya kama anavyo nielekeza shem Cajoli, nikavuta pumzi nyingi kisha nikaishusha taratibu huku nikimtazama shem Cajoli usoni mwake.
“Cha kushukuru Mungu sura yako bado haijangundulika”
“Make up uliyo niweka bado haijabadilika?”
“Ndio badi ipo katika ubora wake. Ninaamini kwamba unawajua watu walio mteka wajina”
 
“Ndio ninawafahamu vizuri sana, ila kitu ambacho kinacho niumiza kichwa ni kuhusiana na wao kufahamu mpango wetu wa kupandikiza hawa virusi, ambao kazi yetu kubwa ilikuwa ni kupata pesa kisha tunaondoka”
“Hilo jambo ninahisi Cajoli baada ya kutekwa, basi wakaamua kumchunguza ili kuweza kujua ni kitu gani kinacho endelea”
“Haileti maana kabisa akilini mwangu”
“Ila tambua kwamba wanakuhitaji wewe”
“Sihitaji kurudi kwenye kundi la Al-Shabab, na kwa nini wametumia sura yangu?”
“Katika hilo swala la kutimiwa sura yako kusema kweli mimi siwezi kufahamu, ila kitu cha kujadili hapa ni wapi Cajoli alipo, pili ni kuhakikisha kwamba tunamkomboa. Dany sote tunafahamu uwezo wetu katika upambanaji, si wakati wa kusubiria serikali itufanyie nini, kikubwa ni kumpata mwenzetu kisha hayo mengine yatafwata”
 
Sikumjibu kitu chochote shem Cajoli zaidi ya kuanza kutembea kwa mwendo wa kasi hadi kwenye ukumbi wa mikutano. Nikaingia na kurudi katika kiti nilicho kuwa nimekalia, ila safari hii sikuhitaji kabisa kukaa kwenye kiti hichi.
“Muheshimiwa raisi, nitakuomba kuanzia sasa uniidhinishe niwe miongoni mwa watu watakao fanya kazi ya kumkomboa mke wangu na bomu la nyuklia, sinto hitaji kupelekwa katika kundi la Al-Shabab na taaluma yangu ikatumika vibaya tofati nay ale niliyo kuwa nimekusudia kuyapanga kwenye maisha yangu”
Kauli yangu niliizungumza kikakamavu na kumfanya K2 kuanza kunyanyuka taratibu kwenye kiti alicho kuwa amekali huku akiwa amenikodolea macho akishangaa kwa kile ninacho kizungumza.

AISIIIII……….U KILL ME 109 


Tukatazamana machoni na K2 kwa zaidi ya dakika mbili huku ukumbi mzima ukiwa kimya. Taratibu akaka kwenye kiti chake huku akiendelea kunitazama kwa umakini sana.
“Dokta Lameck una uhakika na kile unacho kizungumza?”
“Ndio muheshimiwa raisi nina uhakika na ninacho kizungumza”
“Ila wewe professional yako ni daktari?”
“Muheshimiwa raisi hapa tunazungumzia kuhusiana na nchi pamoja na mke wangu, nipe kazi hii kisha utaona”
Niliendelea kuzungumza kwa kujiamini huku nikimtazama K2 machoni mwake. 
 
“Meja Gerad, unaweza kumuandaa dokta Lameck na kuanza kumpa habari nzima za hili tukio”
“Sawa muheshimiwa”
“Ningeomba kuongozana na shemeji yangu katika hili swala”
“Hapana hili swala Cajoli ni hatari sana, kwa hiyo hauwezi kwenda kulifanya, tutahakikisha kwamba dokta Lameck anaongozana na timu mzima ya NSS, kwenda kulifanya hili tukio”
Shem Cajoli hakuwa na jambo la kuzungumza zaidi ya kuendelea kukaa kwenye kiti alicho kikalia. Nikaongozana na meja Gerad hadi kwenye chumba maalumu cha kujiandaa.
“Dokta Lameck kutana na Agent Leonard Thomas, ni kiongozi wa hii oparesheni”
“Nashukuru  kukufahamu dokta Lameck”   
“Hata mimi pia ninashukuru kukufahamu”
“Hapa kuna silaha za kila aina na unaweza kuchagua ni silaha gani ambayo unaweza kuichukua”
“Sawa musijali katika hilo”
 
Nikachukua bastola mbili pamoja na magazine kumi zenye ujazo mzuri wa risasi. Nikavaa jaketi la kuzuia risasi, nikakabidhiwa kifaa maalumu cha mawasiliano.
“Timu yetu ina watu wanne, ameongezeka dokta Lameck David, location ya bomu lipo maeneo ya Kariakoo, katika gorofa la Machinga. Ila hadi sasa hatujafahamu maadui hawa wapo sehemu gani na wanampango gani”
“Ngoja kwanza agent Leonard, mumejuaje kwamba bomu lipo maeneo ya gorofa la Machinga ikiwa hamfahamu kwamba magaidi hao wapo sehemu gani?”
Swali langu likawafanya ma agent hawa wa NSS kutazamana.
“Kutokana na taarifa ambayo tulipatiwa na wapelelezi wetu walihisi kwamba bumu hilo lipo katika gorofa hilo”
“Agent Leonard sahamani sana kama nitakuwa ninawaingialia kwenye kazi hii yenu. Ila kitu ambacho munakifanya hapa ni utoto, hamuweze kuapata habari zisizo na uhakika na kusema kwamba tunaweza kwenda eno hilo na kukuta bomu.”
 
Nilizungumza huku nikimtazama kila mtu usoni mwake.
“Hili ni bomu, na hili sio andazi wala muhogo ambao tunaweza kusema kwamba tunaweza kwenda kuukuta sehemu umetulia. Tazama leo magaidi wameweza kuvamia hadi ikulu, inaonyesha kuna mtu au watu ndani ya serikali ambao wameweza kusababisha swala la uvamizi wa Ikulu. Kwanza ni aibu na pili, zile video ambazo zimetumwa kwa raisi ni feki”
“Feki, una maana gani dokta Lameck?”
“Al-Shabab sio  kundi ambalo linanguvu sana ya kuweza kuvuka nchi kama Kenya, na kuja kuipiga ikulu yetu kirahisi namna ile, inaonyesha kwamba NSS haina imeishiwa uwezo wa utendaji wake wa kazi”
 
“Dokta Lameck wewe ni daktari na sisi ni wapelelezi wa serikali kwa kila tunacho kifanya tuna uhakika nacho, kwa hiyo kama unahitaji kuongozana nasi tuongozane, kama utahitaji kubaki unaweza kubaki kwa manaa hii sio siasa ni swala la ulinzi wa taifa”
Agnet mmoja alizungumza huku akinikazia macho, nikawatazama kisha kwa haraka nikachomoa bastola yangu na kumnyooshea agent huyu na kuwafanya wezake wote nao kuninyooshea bastola zao.
“Ninaujuzi mkubwa zaidi yako katika hili swala, sifanyi kazi ya kufwata upelelezi usio kamili, sijitoi sadaka kwa nchi, bali najitoa sadaka kwa ajili ya mke wangu. Nilisha mpoteza wa kwanza ila huyu sihitaji ujinga huo kuweza kujitokeza tena”
“Dokta Lameck weka bastola yako chini”
Agent Leonard alizungumza huku bastoka yake akiwa ameninyooshea mimi kichwani mwangu. Nikamtazama kwa jicho la pembeni kisha taratibu nikaushusha mkono wangu wenye bastola na kuirudisha sehemu nilipo itoa.
“Samahani kwa hili, ninaomba kuuliza, je kuna mtu amekamatwa katika uvamizi wa ikulu?”
“Ndio yupo mmoja”
“Ningeomba kuonana naye kisha nyie muendelee na utaratibu wenu ambao mumejiwekea”
“Agent Chris msindikize dokta Lameck katika chumba cha mahojiano”
“Sawa mku”
 
Nikaondoka na agent mwengine ambaye hajapangwa katika zoezi hili la kwenda kuvamia eneo la gorofa la Machinga linalo sadikika kwamba kuna bumo  la nyuklia ambalo limetegwa katika eneo hilo.
“Agent Beatricem hutu ni dokta Lameck anahitaji kumuona muhusika aliye shikwa katika tukio la kuivamia ikulu”
“Karibu dokta Lameck”
“Asante agent Beatrice”
“Ila kabla ya kuingia katika chumba cha mtuhumiwa, ningeomba kuuliza kwamba una professional yoyote ya kudili na swala la kigaidi?”
“Ndio”
“Na je umepewa mamlaka hayo na nani?”
“Mpigie raisi wako umuambie kwamba nipo katika chumba cha mahojiano”
Agnet Beatrice akanitazama usoni kwa kunikazia macho na mimi nikamkazia macho taratibu akatingisha kichwa akiashiria kuniamini kwa kile anacho kifanya.
“Twende huku”       
“Shukrani”
 
Tukaingia kwenye moja ya chumba chenye Tv zipatazo nne zinazo muonyesha mtuhumiwa aliyopo chumba cha pili katika chumba cha mahojiano akiwa amefungwa pingu na kukalishwa katika kiti cha chuma.
“Ameweza kuzungumza lolote juu ya ugaidi ambao umefanyika ikulu?”
“Hadi sasa hivi hakua alicho kizungumza japo tumempa mateso ya kutosha na hata kumchoma sindano ya maumivu ila hajazungumza chochote”
“Mumweze kufahamu ni wapi alipo tokea?”
“Ndio, jina lake ni Hassan Abdalah, ametokea nchini Somalia ana umri wa miaka ishirini na tisa”
“Ana familia yake?”
“Ndio”
Nikamtazama jamaa huyu kwenye tv iliyopo katika chumba hichi, nikaitazama saa ya ukutani inaonyesha ni saa kumi kamili alasiri
 
“Nipe dakika kumi”   
“Sawa dokta”
Nikaingia katika chumba alipo gaidi Hassan Abdalah. Alipo niona kidogo akastuka, inaonekana ni mtu ambaye ananifahamu kidogo labda kwa kuelekezwa au kwa kuonana.
“Ninaitwa dokta Lameck ninahitaji kukuuliza maswali machache ukinipa ushirikiano basi utakuwa salama”
Nilizungumza huku nikiwa nimesimama mbele ya meza yake.
“Ni wapi lilipo bomu la nyuklia pamoja mke wangu Cajoli”
Hassan Abdalah hakuzungumza kitu chochote zaidi ya kunikodolea macho ya dharau.
“Ninazungumza kwa upole tu, ila ninakuuliza ni wapi alipo mke wangu pamoja na bomu la nyuklia ambalo mumepanga kulilipua”
“Haahaaa umechelewa”
Hassani alizungumza kwa kujiamini sana hukua akinikodolea macho yake. Kwa haraka nikachomoa bastola yangu, nikaisogeza meza pembeni kisha nikamtandika risasi moja ya paja la mguu wa kulia, na kumfanya Hassan Abdalah kupiga ukelele wa maumivu makali.
 
“NI WAPI LILIPO BOMU LA NYUKLIA NA MKE WANGU CAJOLI”
Niliuliza kwa kufoka huku nikiwagandamiza mdomo wa bastola yangu kwenye jeraha lake la nguu. Mlango wa chumba hichi ukafunguliwa akaingia agent Baetrice pamoja na vijana wake wawili.
“Dokta Lameck huo sio uhojiji  mzuri wa maswali”
“Kaa pembeni hili swala halikuusu”
“Mimi ndio msimamizi wa hii kesi”
Agent Beatrice alizungumza kwa hasira huku akinikazia macho, nikamtazama kwa hasira, nikamsogele vijana wake wakachomoa bastola zao na kuninyooshea, sikuliogopa hilo zaidi ya kumsogelea karibu zaidi hadi nikaribia usoni mwake.
“Kuna mamilioni ya watu, muda wowote na siku yoyote wanakwenda kupotezama maisha kwa ajili ya hawa wajinga wachache, mke wangu ametekwa kwa ajili ya hawa wajinga wachache. Kuna walinzi wa raisi, pamoja na wafanyakazi wa ikulu kwa ajili ya hawa watu wachache leo hii unanimbia kwamba huu sio utaratibu wa kuhoji maswali. Unaakili kichwani mwako AGENT BEATRICE?”
 
Nilizungumza huku nikiwa nimeyang’ata meno yangu na kumfanya agent Beatrice kunitazama usoni mwangu kwa maana hasira niliyo kuwa nayo na haya niliyo yazungumza yana ukweli ndani yake.
“Waambie vijana wako  kushusha bastola zao na mutoke nje, kabla hili swala halijawabadilikia nyinyi”
Agent Beatrice taratibu akawaamuru vijana wake kushusha bastola zao chini. Wakatoka ndani ya chumba hichi taratibu kisha wakaufunga mlango. Nikamgeukia Hassan Abdalah huku nikiwa na bastola yangu mkononi.
 
“Ni wapi alipo Cajoli na bomu  la nyuklia lipo  wapi?”
“Si….sijuiii mimi, niliagizwa tu kufanya shambulizi ikulu”
“Uliagizwa na nani?”
“Mkuu wetu Yudia”
“YUDIAAA…….!!?”
“Ndio mkuu, ni Yudia”
“Yudia anafanya kazi na Al-Shabab?”
“Ndi…ioo mkuu, alikuja kutoa ada ya sisi kutekeleza hilo jambo”
“Yeye yupo wapi?”
“Sifahamu mkuu sisi ni vibaraka tu tunafwatisha amri”
“Bomu la nyuklia lipo wapi na Cajoli yupo wapi?”
“Sifahamu, ila nilisikia kwamba bomu la nyuklia litalipuliwa katika eneo la…la Posta”
“Na sio Machina Kariakoo”
“Ndio”
 
Na litalipuliwa saa ngapi?”
“Saa kumi na moja kamili alifajiri”
“Mungu wangu, lipo posta katika eneo gani?”
“Lipo eneo la gorofa refu katika magorofa yote ya posta”
Nikamtazama Hassan Abdlah jinsi anavyo zungumza kwa kumwagikwa na machozi mengi usoni mwake. Kwa haraka nikaufungua mlango na kukuta Beatrice akiwa amesimama na watu wake
“Haraka anda timu itakayo kwenda post, kuangalia ni gorofa gani lililo tegwa bomu”
“Sawa dokta”
Nikarufi katika chumba alipo Hassan Abdlah, nikamkazia macho kwa haraka nikamfwata hadi sehemu alipo kaa, nikamnyanyua na kumuangusha chini kwa nguvu.
“Ni wapi alipo Cajoli mke wangu la sivyo risasi zote hizi zitaishia kichwani mwako”
“Ca…..ca….caj…oli ni master plan”
“Master Plan una maana gani?”
“Cajoli mke wako ndio aliye panga haya yote”
Masikio yangu nikahisi yananiwasha kwa hichi nilicho kisikia kwa maana Cajoli ninaye mfahamu mimi sioamini kama ni mwanamke mwengine msaliti kwenye maisha yangu.

==>>ITAENDELEA KESHO
chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )