Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Saturday, October 20, 2018

AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 112 na 113 )

juu
MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA- 0657072588
ILIPOISHIA   

“Alikusaliti kivipi?”           
“Alinichukulia mwanaume wa maisha yangu, alinichukulia mwanaume niliye mpenda. Isitoshe akamuaa mwanaume huyo mbele ya macho yangu”
“Mwanaume huyo ni nani?”
“Ni raisi aliye pita”
“Ina maana K2 alimuua kaka yake?”
“Ndio”
Moyo wangu ukajikuta ukipatwa na ubaridi mkali sana, japo nipo kwenye mateso ila maneno ya Yudia yamezidi kunifanya kumchukia K2 na kuapia nikipata nafasi nyingine nitahakikisha kwamba nitakikata kichwa chake kwa mikono yangu mimi mwenyewe.
   
ENDELEA           
“Ila nilisikia kwamba raisi aliye pita aliugua akashindwa kuiongoza nchi?”
 
“Ndio aliugua kutokana K2 alimuwekea sumu iliyo kuwa ikimua taratibu taratibu na nilikuja kushuhudia akimalizia kwa kumziba uso wake kwa mto”
“Daaa, ninakuomba basi uweze kuniachia, au muachie mke wangu aondoke”
“Dany, mke wako  kwa sasa amesha ingia kwenye mtandao wa kigaidi, akitoka uraiani huyo hata wananchi wa kawaida wanaweza kumua. Na kitu kingine kumbuka kwamba mimi na wewe ni maadui bado japo tunazungumza ila sikuamini, wala mimi najua huwezi kuniamini”
“Hilo la kuaminiana ninaamini kwamba halito kuja kutokea siku hata moja”
Yudia akachomo bastola yake baada ya mzee mmoja akuingia akiwa amebeba laptop aina ya Mac.
“Unahitaji kufanya nini?”
“Halikuhusu, tulia kama ulivyo”
Mzee huyu akamkabidhi Cajoli laptop hiyo, taratibu Yudia akamsogelea Cajoli huku akiwa amemnyooshea bastola ya kichwa.
 
“Unaweza kuhamisha pesa hiyo kwa namba ya benki ambayo nitakupatia”
“Yudia unafika mbali, haufuhamu kwamba hiyo pesa mimi nimeitafuta kwa tabu gani?”
“Dany kelele hili ni kati yangu mimi na Cajoli na kama anahitaji wewe uishi basi akubaliane kwa kile ambacho ninamuhitaji yeye kufanya”
“Tafadhali Yudia ninakuomba hiyo pesa usiichukue, nimepata tabu, nimehangaika miaka yangu yote ili niweze kupata nguvu ya kulipiza kisasi”
Nilizungumza huku machozi yakinilenga lenga usoni mwangu.
“Dany kuzungumza kwa muda mfupi sio kwamba sisi ni marafiki unanisikia. Muda wowote na wakati wowote endapo utajaribu kurudia kufanya ujinga wako wakuzungumza mambo yako ya kijinga, nitahakikisha kwamba mke wako ninamfumua ubongo wake ujue kwamba sina huruma”
“Dany pesa tutatafuta”
 
Cajoli alizungumza huku akijipangusa machozi usoni mwake. Taratibu Cajoli akaanza kuminya minya batani za laptop hiyo, baada ya dakika tano akamgeuzia mzee huyo laptop, taratibu mzee huyo akatingisha kichwa chake huku akimtazama Yudia usoni. Gafla Cajol pasipo kuwa na huruma akamtandika Cajoli risasi ya kichwa, taratibu nikamshuhudia Yudia akianguka chini huku damu nyingi zikimtoka kichwani mwake. Macho yangu yakanitoka, mwili mzima ukaanza kutetemeka kwa hasira kali, Yudia akanigeukia na kunitazama kwa macho ya dharau kisha akatoka ndani ya chumba hichi huku akiwa ameongozana na watu wake. 
 
“CAJOLIIIII”       
Niliita kwa nguvu huku machozi yakinimwagika usoni mwangu, taratibu nikaanza kujisogeza na kiti changu japo ni zoezi gumu, ila nikajikaza hivyo hivyo kuhakikisha kwamba ninamfikia Cajoli mke wangu ambaye tayari emasha poteza maisha.
Gaidi mmoja akanisogele huku akinitazama usoni mwangu, akamtazama Cajoli kisha akatoka katika chumba hichi. Magaidi wote wakatoka katika chumba hichi na kunicha nikiwa na maiti ya mke wangu.
 
‘Yudia nitakuua kifo kibaya sana’   
Nilizungumza huku nikijitahidi kusogea taratibu hadi alipo mke wangu Cajoli. Nikakajiangusha chini na kiti changu, nikabaki nikimtazama kwenye sura yake huku machozi yakiendelea kunimwagika.
“Cajoli nisamehe mke wangu, haya yote yametokea kwa ajili yangu”
Milio ya risasi ikaanza kurindima ndani ya mapango haya jambo lililo nifanya sasa nianze kujaribu kujifungua mikono yangu, ila sikuweza kufanikiwa kutokana na kukazwa sana kwenye hichi kiti. Akaingia gaidi ambaye muda machache alitoka kunitazama, akaanza kukata kamba nilizo fungwa.
“Tumevamiwa na jeshi”
Jamaa alizungumza huku akinifungua kamba zangu kwa nyuma. Akanikabidhi bastola moja huku akinitazama, sikujua ni kwa nini ameamfua kunisaidia.
“Ni wakati wa kuondoka sasa tukiendelea kukaa hapa tutakamatwa na wanajeshi”
Nikamnyooshea bastola huyu jaama huku nikimtazama kwa macho makali usoni.
 
“Wewe ni nani?”   
“Jina langu ninaitwa Stive, nilikuwa mpelelezi chini ya mama yako katika kikosi hichi”
“Mama yangu?”
“Ndio mimi ndio nilikuwa nikimpatia mama yako habari zote na mipango ambayo inaendelea ndani ya kundi hili”
“Kwa nini umeamua kunisaidia?”
“Dany huu sio muda wa kuendelea kuulizana maswali muda wowote hapa tutakuja kukamatwa, na kama unavyo ona tayari siri uliyo kuwa umeifanya imesha gundulika ni muda wa kondoka sasa”
Nikamgeukia Cajoli wangu, taratibu nikapiga magoti chini, kwa nguvu nikamnyanyua na kumuweka begani mwangu kitendo kilicho mdafnya Stive kushangaa.
“Amesha kufa huyo t……..”
Nilimkatisha kwa kumnyooshea bastola ya usoni mwake.
“Huyu ni mke wangu na wala hufahamu ni uchungu gani ambao ninao.”
 
“Sawa mkuu, chukua miwani hii”
Stive akanikabidhi miwani inayo weza kumsaidia mtu kuona katika giza kali. Tukaanza kutoka huku tukikimbia, sikuhitaji kumuangalia mke wangu kwa maana anaweza kunipa simanzi kubwa kwye maisha yangu. Tukaendelea kukimbia kwenye njia ambazo Stive anaonekana kuzifahamu ivuziri.
“Huku tunaelekea wapi?”   
“Tuna mwendo mrefu na tutatokea nchini Kenya”
“Tutatumia msasaa mangapi?”
“Masaa mawili kwa mguu, ila njia hizi zinatisha sana kwa hiyo unatakiwa uwe jasiri”
“Wewe twende tu”
 
Tukaendelea kusonga mbele, huku tukiwaachia kizaa zaa Yudia na watu wake. Sehemu ambayo ilitulazimu kukimbia, inatubidi kukimbia na sehemu iliyo tulazimu kutembea basi ikatubidi kutembea kwa mwendo wa haraka sana huku mwili wa mke wangu nikiendelea kuubeba begani.
“Ilijuana vipi na mama yangu?”
“Mama yako alikuwa ni mwalimu wangu, na hata kuingia kwenye kundi hili la Al-Shabab yeye ndio alihitaji mimi kuingia ili kuweza kufanikisha mipango yake”
“Alikuwa ni mwalimu wa nini?”
“Sayansi na teknolojia, na hicho ndio kitu ambacho kilinifanya niweze kuishia kwenye kundi hili kwa muda wa miaka sita sasa”
“Na mauji dhidi ya mama pamja na ndugu zangu ulilifahamu hilo?”
 
“Nililifahamu baada ya tukio kutokea, tena hii ni baada ya kuanza kupita wiki pasipo mama kuzungumza na mimi, ilinibidi kuanza kufanya uchunguzi wa chini chini hadi nikafanikiwa kuona maiti zao”
Tulizungumza huku tukizidi kusonga mbele, kwa mwendo wa kutembea kwa haraka sana. Tukafika kwenye moja ya majabali yaliyo chungoka vizuri kama viti.
“Ninaomba tupumzike hapa”   
“Hii sehemu sio salama tuzidi kusonga mbele”
Ikanibidi kumbadilisha Cajoli na kumlaza kwenye bega jengine kwa maana hili ninaona linaweza kuvunjika.
“Je baba yangu unamfahamu?”
“Ndio ninamfahamu”
“Vipi kuhusu yeye?”
“Yeye ndio mtu wa kwanza kuuwawa na K2, baada ya hapo ndio ikafwatia familia nzima. Ila kuna kitu kimoja muhimu tukifika nchini Kenya nitakukabidhi, niliambia nikupe wewe na baba yako”
“Kitu gani?”
“Utakifahamu palee tutakapo fanikiwa kufika nchini Kenya”
“Ilikuwaje baba yangu akakukabidhi wewe kitu hicho”
“Ukweli ni kwamba……..”
Stive akaka kimya kwa muda huku tukiendelea kusonga mbele.
 
“Zungumza huo ukweli?”
“Dany ni muda wa kuhakikisha kwamba tunatoka salama kwenye haya mapango, ninakuomba hayo mazungumzo tukayafanyie Kenya”
Tukaendelea kusonga mbele, ikafikia hatua Stive akanisaidia kumbeba Cajoli begani mwake na safari hii ndefu kwa miguu ikazidi kusonga mbele. Tukafanikiwa kutoka nje ya mapango haya salama salimini, sehemu tuliyo tokea ni kwenye msitu mkubwa sana na wenye hewa ya baridi kubwa sana.
“Tuelekee huku”   
Stive aliendele kuzungumza na mimi sikuwa na budi zaidi ya kuendelea kusonga mbele. Tukafika kwenye kijumba kimoja kilicho tengenezwa kwa mbao.
“Karibu nyumbani?”   
“Huyu!!?”
 
“Ndio hapa ndio kwenye maficho yangu”
Stive alizungumza huku akifungua mlango wa chumba hichi. Tartaibu tukaingia ndani huku nikiangaza macho yangu huku na kule. Kajumba haka kana seble moja pamoja na chumba kimoja, tukaingia ndani ya chumba chii, nikaona ngazi zinazo elekea ndani ya chumba hichi. Stive akaendelea kuongoza na kuelekea chini. Aminya swichi ya ukutani na kuziruhusu taa zote zililomo ndani ya chumba hichi kuwaka kwa pamoja. Akaandaa kitanda kidogo, kisha nikamlaza mke wangu Cajoli ambaye ni mda mrefu alisha paukua kutokana na kupoteza maisha. Taratibu Stive akanisogelea na kunishika begani kwa mkono wake wa kulia.
 
“Unatakiwa kuwa jasiri, mkakamavu. Kufariki kwa shemeji iwe ni moja ya changamoto kubwa kwenye maisha yako, kwa maana huyu ni shemeji wa pili kufariki”
Stive alizungumza maneno yaliyo nifanya nianze kumwagikwa na machozi huku nikimtazama Cajoli alivyo lala kwenye hichi kitandani.
 
“Kuna listi kubwa ya watu ambao aliniachia mzee, watu hawa tunatakiwa kuwaondoa kwenye uso wa dunia”
“Hiyo orodha ipo wapi?”
“Ninayo”
Stive akafungua kabati lililopo humu chumbani na kutoa kidabu kidogo cha kuhifadhia kumbukumbu, katika kukitazama vizuri nikaweza kugundua kwamba kitabu hichi nilisha wahi kumuona nacho baba.
“Hichi kitabu mzee alinikabidi na kunipa maelezo kwamba nikupatie wewe, kina maeleo yote ya jinsi ya kuwapata watu hao ambao tunatakiwa kuwaa”
“Inakuwaje kwamba baba anahitaji niwaue watu wake ikiwa mimi pia nina watu wangu ambao ninatakiwa kuweza kuwashuhulikia?”
 
“Kusema kweli siwezi kufahamu, yeye alinipa maelezo hayo wiki chache kabla ya yeye kufariki”
Nikafunua kitabu hichi na kupitisha pitisha macho yangu kwa haraka katika kurasa chache kisha nikakiingiza mfukoni.
“Kwa sasa kichwa changu akipo vizuri, ninahitaki kufanya mazishi ya mke wangu”
“Sawa”
“Ila si unatambua Yudia ni wapi alipo au maficho yake makubwa yanakuwa wapi?”
“Ndio ninafahamu ni wapi maficho yake yalipo kwa maana yeye kwa muda mwingi anapenda kunishirikisha katika mambo yake mengi nikiwa kama mshauri wake”
“Ningeomba kwa sasa unisaidie kumtafuta Yudia, kwa maana ninahitaji kumua kama alivyo mua mke wangu”
“Swala la kumzika shemeji ndio basi tena?”
“Nitamzika baada ya kumliza mauji yangu. Hadi sasa nina maiti mbili za kuzika, moja ipo hospitali ya Bombo mkoani Tanga”
 
“Mmmm, bisi inabidi umchome sindano shemeji ya kuukausha mwili wake”
“Nitaipata wapi kwa muda huu hiyo sindano”
“Mimi ninayo”
Stive akafungua kabati jengine, akatoa kichupa kidogo cha dawa kisha akachukua bomba la sindano. Akaliandaa vizuri kwa kuifunga sindando kisha akavuta dawa ya kutosha.
“Hii dawa inakaa wiki moja kabla ya mwili kuanza kuoza”
“Wiki moja nina imani nitakuwa nimesha maliza kazi yangu”
Stive akanikabidhi sindano iliyo jaa damu, taratibu nikaichoma kwenye mkono wa Cajoli na kuisukuma dawa yote ndani.
“Dani unajua muda ule nilihitaji kuzungumza kitu gani?”
“Zungumza”
“Mimi ni kaka yako wa damu moja”
Maneno ya Stive yakanifanya nimgeukie na kumtazama kwa mshangao sana kwa maana katika kipindi cha kuishi na wazazi wangu wala sikuwahi kusikia kwamba nina kaka zaidi ya kujijua kwamba mimi kwenye familia yangu ndio mtoto wa kwanza.

AISIIIII……….U KILL ME 113 
         
“Hahaa acha kunitania Stive”       
“Trust me Dany, mimi ni kaka yako”
Nitaamini vipi kama wewe ni kaka yangu kwa maana sikuwahi kukusikia ukiongelewa na mtu yoyote kwenye familia yangu”
Stive hakuzungumza chochote, akafungua droo na kutoa laptop, akaiwashana kuiweka mezani akafungua faili moja wapo la video ambayo inamuonyesha baba akiwa akaa kwenye kiti cha ofisini kwake.
 
“Dany ni kwa muda mrefu hii siri mimi na mama yako tuliamua kuificha ili mradi wewe usiweze kufahamu wala mdogo wako Diana asiweze kuligundua hili kw amaana lingeinua chuki katika familia yangu jambo ambalo nilikuwa sihitaji kulisikia wala kuliona linatokea”
Nikasimama vizuri huku nikiwa nimeikunja mikono yangu kifuani mwangu, nikiendelea kutazama video hii.
“Dany nina kaka yako ambaye amekupita miaka miwili. Anaitwa Stive ni miongoni mwa wanamgambo wa kundi la Al-Shabab, mimi na mama yako tuliamua kumpeleka hapo akawe ni mpitisha habari wa kundi hilo kwa maana tuna ndoto kubwa ambazo mimi na mama yako hatutoweza kuzitimiza, hii ni kutokana na kuzungukwa na maadui wengi sana.”
 
“Video hii nitamuachia kaka yako Stive, kwa kupitia hii video utamuamini kwa maana yeye anakufahamu wewe ila wewe akafuhamu, Stive atakuwa kiongozi wa kukufanikisha kutimiza ndoto ya mama yako kuwa raisi”
Nikaminya batani ya kuisimamisha video hii na kumgeukia Stive na kuanza kumtazama kuanzia juu hadi chini, nikarudia kufanya hivyo kwa mara kadhaa kuhakikisha kwamba ninapata japo kitu ambacho kitanifanya nimuamini kwamba ni ndugu yangu japo kwa kufanana.
“Haijaisha bado”   
“Sina haja ya kuendelea kuimaliza”
“Ila Dany unatakiwa kutimiza ndoto ya kuwa raisi”
“Hiyo ndoto sio ya kwangu sawa, aliye kuwa naye amesha kufa na wala sikuwahi kuja kufikiria kwamba ipo siku nitakuja kuwa raisi”
 
“Dany unatakiwa kulifanya hilo”
Stive alizungumza kwa msisitizo huku akinitazama usoni mwangu, taratibu nikamsogelea hadi sehemu alipo simama huku nikiwa nimejawa na hasira kubwa sana moyoni mwangu.
“Hunijui sikujui, siamini kitu alicho kizungumza baba yangu kama unahitaji nisaidie kumtafuta Yudia ila kama huitaji basi nitamtafuta mimi peke yangu. Tumeelewana”
Kwa sauti niliyo izungumza na iliyo jaa msisitizo mkubwa ikamfanya Stive kutingisha kichwa kiwoga.
“Naomba sururu na chepe”   
“Eheee?”
“Umenisikia”
Stive akarudi nyuma hatua kadhaa akatoa chepe na sururu vilivyokuwa nyuma ya moja ya kabati katika hichi chumba, akanikabidhi, nikamtazama Cajoli wangu, machozi yakanimwagika pasipo kuzungumza kitu chochote nikatoka nje ya nyumba hii, nikatafuta sehemu iliyo kaa vizuri na kuanza kuchimba kaburi peke yangu. Jasho lilivyo zidi kunitiririka, ikanilazimu kuvua shati langu na kuendelea kuchimba kaburi hili huku nikiwa na hasira kubwa sana moyoni mwangu.
 
“Yudi ulipo fika ni mbali sana”   
Nilizungumza huku nikiendelea kuchimba kaburi hili, nilipo hakikisha kwamba nimechimba kimo ambacho ninaweza kumlaza mke wangu, nikatoka ndani ya kaburi hili, nikarudi ndani na kumkuta Stive akiwa anaminya minya batani za Laptop yake. Nikamnyanyua Cajoli na kumuweka begani, taratibu Stive na yeye akasimama na kuanza kunifwata kwa nyuma.
Tukafika sehemu ya kaburi taratibu nikamshusha Cajoli na kumlaza chini huku machozi yakinimwagika usoni mwangu na kilio changu chote ninakililia ndani kwa ndani. Taratibu nikausogeza mdomo wangu kwenye kinywa cha Cajoli, nikampiga busu zito lililo dumu kwa dakika tano.
‘Nisamehe mke wangu, sikukusudia mwisho wako uwe hivi. Ninatambua haya yote yametokea kwa ajili yangu, pumzika kwa amani Cajoli wangu’
 
Nilizungumza kimoyo moyo huku nikimtazama Cajoli, taratibu nikashuka kwenye shimo na kumuomba Stive anipatie mwili wa mke wangu, japo ninamzika kwa aibu kubwa na nikinyume na sheria za kidini yangu, ila sina jinsi zaidi ya kufanya hivi. Stive akanipatia mwili wa Cajoli, taratibu nikaupokea na kuulaza chini taratibu. Nikaitazama cheni iliyopo shingoni mwa Cajoli nikaikata na kutoka nje ya kaburi. Nikachuku chepe na kuanza kufukia kaburi kwa hasira kubwa sana. Stive akarudi ndani, baada ya muda akarudi akiwa na chepe. Tukasaidia kufukia kaburi hadi tukafanikiwa tumemaliza.
“Nitahitaji hii sehemu niijengee”
“Kwa leo itashindikana kwa maana hapa sina vifaa vya kujengea”
“Poa”
Nikaondoka katika eneo la kaburi huku nikiwa ninaburuza chepe langu, nikaingia ndani.
“Dany unatakiwa kuoga sasa”   
“Nitaoga, umefanikiwa kumpata Yudia?”
“Ndio nimefanikiwa kupata location aliyopo kupitia satelait”
“Yupo bado Tanzan?”
“Hapana kwa sasa ninamini kwamba anaelekea nchini Somalia”
 
“Itabidi twende leo”
“Dany unatakiwa kupumzika kidogo”
“Nipummzike, mke wangu amekufa kwa ajili yake, kama ni pesa alichukua, inakuwaje amuue mke wangu eheeee”
Nilizungumza kwa kufoka huku nikimtazama Stive usoni mwake.
“Dany kazi kama hizi haziogozwi kwa hasira, ni akili hapa ndio inahitajika kutumiwa sawa, ukikurupuka utaingia tena mikononi mwao”
“Huo ni ujinga na upumbavu unao uzungumza. Kwanza wewe ni nani hadi unizuie kuhusiana na mipango yangu”
“Mimi ni kaka yako na ni mshauri wako na unahitajika kufwata amri nitakayo kuambia”
“Samahani sijakusikia vizuri”
“MIMI NI KAKA YAKO NA UTAFWATA AMRI NITAKAYO KUAMBIA”
Stive alizungumza kwa sauti nzito huku akinisogelea kwa ukaribu sana. Kwa hasira nikamsukuma akapepesuka kidogo, akajaribu kunishika mkono wangu wa kulia, ila nikawahi kuutoa kwenye kiganja chake na kurusha ngumi kwa mkono wa kulio iliyo mpata kichwani mwake na kumfanya awewesuke tena, nikarusha ngumi nyingine mfululizo ila zote Stive akazikwepa.
 
“Dany sihitaji kupambana na wewe na wala sihitaji kukuumiza”
Sikumjibu chochote Stive zaidi ya kuendelea kupambana naye, ila kadri nilivyo jaribu kupambana naye Stive alinikwepa sana na wala hakuhitaji kuipiga ngumi yoyote mwilini mwangu.
“Dany tulia sihitaji kukuumiza tafadhali”   
Stive alizungumza huku akijaribu kunishika, mikono yangu, nikamtandika kichwa cha pua na kumfanya aishike pua yake. Gafla nikastukia akinipiga teke moja la shingo, lililo nifanya nianguke chini na giza kali likatawala kwenye macho yangu.
                                                                                                       ***
“Cajoli”   
Nilikurupuka usingizini huku nikihema sana, jasho jingi linanimwagika mwilini mwangu. Nikamtazama Stive aliye simama pembeni yangu. Ukimya ukatawala kati kati yetu huku kwa mara kadhaa tukiwa tunatazamana pasipo kuzungumza chochote.
“Nikuletee chai”   
“Kwani ni saa ngapi muda huu?”
“Ni saa kumi na mbili alfajiri”
”Imekuwaje hadi nimelala muda wote huo”
“Hilo sio jambo la kulizungumzia kwa wakati huu. Nimepanga safari ya sisi kuelekea Somalia kuhakikisha tunatoa hukuma kwa wale wote ambao wamesababisha maumivu ya mioyo yetu”
“Umepata ni sehemu gani alipo Yudia?”
“Ndio sehemi hiyo sio ngeni kwako, kwa maana ulisha fika”
“Una maana ni kambi ya Al-Shabab?”
 
“Ndio ni kwenye kambi hiyo na hapo ndipo Yudia alipo”
“Sawa kazi nzuri Stive”
“Ingia bafuni humo, oga njoo unywe chai.”
Stive alizungumza huku akinitupia taulo, akatoka chumbani na kuniacha peke yangu, nikaingia bafuni nikavua suruali niliyo lala nayo na kuanza kuoga. Kila ninapo jaribu kuyafumba macho yangu ninahisi kuiona sura ya Cajoli, jambo lililo nifanya nianze kujisikia vibaya moyoni mwangu.
Nikatoka bafani huku nikiwa nimejifunga taulo, nikaeleka katika chumba kilichopo chini ya aridhi na kukuta ngo za polisi wa nchini Kenya.
 
“Chuku nguo zako hizo utavaa, tutatumia usafiri wa gari  la polisi kuhakikisha kwamba tunapitoka ndani ya nchi ya Kenya pasipo wewe kustukiwa na mtu yoyote”
“Somali je?”
“Huko napo nitakueleza ni nini cha kufanya cha muhimu ni kuhakikisha kwamba tunatoka ndani ya Kenya salama salami”
Sikuwa na maswali lolote zaidi ya kuchukua nguo hizi na kuzivaa. Nikavaa buti za polisi pamoja na kofia. Kisha Stive naye akavaa nguo zake, tukajiandaa vya kutosha na kila mtu kwenye shati lake ana tumia jina tofauti huku mimi nikitumia jina la sajenti Ulolo David nay eye akitumia jina la Koplo Celvin Orig.
“Kuna gari lipo nyuma ya nyumba, ni gari la polisi, hakikisha kiswahili tunacho kitumia kitafanana kabisa na Kiswahili cha Kenya”
 
“Hicho Kiswahili cha Nyanya ndio bibi?”
“Hicho hicho. Kumbuka kwamba hii kazi tunayo iendeea hatuendi kusalimia mtu, ila tunakwenda kumua mtu, sasa wewe ule ugonjwa wako wa kuonyeshwa kum** na mwanamke na ukajisahau sinto hitaji kuusikia”
“Sawa”
“Chai kwanza ndio tuondoke”
Tuikaka mezani na kupata kifungua kinywa, tuakamaliza kwa mapamoja, kila kitu cha maandalizi ya kazi Stive alisha kiandaa na kukiweka kwenye begi. Tukatoka ndani ya yumba, moja kwa moja tukaelekea hadi lilipo kaburi la Cajoli, taratibu nikachuchumaa.
 
“Baby ninakwenda kufinya hii kazi, ninakuomba uniombee huko nilipo, siku si nyingi nitakuja huko ulipo”
Macho yakanilenga lenga, kusema kweli kifo cha Cajoli kinaniuma kupita maelezo kwa maana ninajiona kama mimi ndio chanzo kikubwa sana na laiti ingekuwa si mimi kukubali kumuhusisha kwenye matatizo yangu wala leo asinge kuwa ndani ya hili kaburi. Honi ya gari ikanistua na kunitoa kwenye dimbwi kubwa la mawazo, kwa ishara Stive akaniita ili tuondoke katika hili eneo. Nikanayanyuka taratibu huku nikiwa na mawazo mengi sana, nikaingia kwenye gari na taratibu tukaondoka katika eneo hili.
“Hivi ni vitambulisho vyote ni feki ila ni original”
Ni feki na ni original ndio lugha gani?”
“Kwani majina yaliyopo kwenye mashati yetu ni majina yetu ya kuzaliwa?”
“Poa umeshinda”
“Una muda gani na mkeo?”
“Wiki sasa”
 
“Hahaah one week ndio inakufanya ulie namna hiyo kwa ajili ya huyo mwanamke?”
“Stive katika hilo ninakuomba usiningiilie”
“Hilo ndio tatizo lako mdogo wangu, mama wewe si alikuagiza kichwa cha K2, hadi leo kipo wapi?”
Stive alizungumza huku akiongeza mwendo kasi wa gari.
“Dany sasa hivi moyo wako ninahitaji usipende, ninahitaji moyo wako uwe ni mgumu, yupo wapi mkeo, yupo wapi mwanao. Ukiwa unafanya kazi hii unatakiwa swala la kujenga familia uliweke kando kwa maana kupitia familia yako adui zako wanaweza kukuyumbisha kama alivyo fanya Mariam”
Jina la Mariam nilipo lisikia masikioni mwangu, taratibu nikajikuta na yeye nikimuweka kwenye mabano na kuzidi kuapia kwamba nikifika nchini Somalia ni lazima nitamuangamiza Mariam na mama yake.

==>>ITAENDELEA KESHO
chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )