Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Sunday, October 21, 2018

AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 114 na 115 )

juu
MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA- 0657072588
ILIPOISHIA

“Wiki sasa”           
“Hahaah one week ndio inakufanya ulie namna hiyo kwa ajili ya huyo mwanamke?”
“Stive katika hilo ninakuomba usiningiilie”
“Hilo ndio tatizo lako mdogo wangu, mama wewe si alikuagiza kichwa cha K2, hadi leo kipo wapi?”
Stive alizungumza huku akiongeza mwendo kasi wa gari.
“Dany sasa hivi moyo wako ninahitaji usipende, ninahitaji moyo wako uwe ni mgumu, yupo wapi mkeo, yupo wapi mwanao. Ukiwa unafanya kazi hii unatakiwa swala la kujenga familia uliweke kando kwa maana kupitia familia yako adui zako wanaweza kukuyumbisha kama alivyo fanya Maria”
Jina la Mariam nilipo lisikia masikioni mwangu, taratibu nikajikuta na yeye nikimuweka kwenye mabano na kuzidi kuapia kwamba nikifika nchini Somalia ni lazima nitamuangamiza Mariam na mama yake.
       
ENDELEA   
“Umejuaje kwamba nilikuwa na mahusiano na Mariam?”
“Mariam mimi nimemfahamu baada ya kuiua familia yetu, nilimfwatilia sana na hapo ndipo nikagundua alifanya kazi hiyo kwa kushinikizwa”
“Alishinikizwa na nani?”
 
“K2 eti ndio raisi wa nchi, hivi watu walikosa kuchagua mtu wa kueleweka hadi wakamuweka yeye madarakani?”
Nikakaa kimya huku nikifikiria furaha niliyo kuwa nayo kipindi nipo kijana mdogo sana. Mama yangu alituea vizuri sana na mdogo wangu Diana. Hapakuwa na mtu aliye itambua huzuni katika maisha yetu.
“Listi aliyo iacha baba ni lazima tuweze kuitekeleza, la sivyo tutateseka sisi na vizazi vyetu. Mimi siwahamu ndugu wengine, ninakujua wewe peke yako tu na tukisema sisi tuangamie basi utambue kwamba tukakufa kifo cha aibu sana”
Stive alizungumza na wala mazungumzo yake sikuyafwatilia kabisa, kwani kichwani mwangu ninacho kiwaza ni kitu kilicho pita miaka mingi nyuma.
“Ahaaa ndio maana siipendi Nairobi”   
Stive alizungumza huku akipunguza mwendo kasi wa gari, ikanibudi kutazama mbele, nikaona kizuizi cha askari wakikagua magari yote yanayo pita katika barabara hii inayo katiza hapa.
 
“Watakuwa wanatafuta nini?”   
“Sifahamu ila kausha na ukumbuke kile nilicho kuambia, kiswahili hapa kiwe cha Kikenya, sasa wewe zungumza kiswahili fasaha hapa uone watacho kufanya”
“Poa”
Taratibu Stive akasimamisha gari pembeni ya barabara na akafungua vioo vya gari, kwa kupitia kioo cha pembeni tukamuona askari wa kiume akitufwata huku ameshika bunduki yake. Alipo niona akapiga saluti na mimi nikapiga saluti ya kiskaji tu kwa maana nimepita cheo.
“Jambo afande”   
“Jambo ona elekea mujini?”
“Ndio, nini endelea mbona road block kubwa?”
Nilizungumza kiswahili hichi hadi Stive akanitazama kwa jicho la kuiba.
 
“Gaidi toka Tanzania, ingia Kenya, wametoroka baada ya vurumai huko mapango ya Amboni, sasa zidi imarisha ulinzi mana Tanzania lipuliwa bomu la nyuklia”
“Ahaa hakikisha gari zote muna fanya chake up ya uhakika, hakuna jambazi katiza katika City yetu”
“Sawa afande”
“Kazi njema”
Taratibu nikafunga kioo cha upande wangu na tukaondoka eneo hili huku Stive akiwa amejawa na tabasamu pana usoni mwake.
“Kwa kiswahili hicho lazima tutoboe bila kistukiwa”
“Yaaa, kwenye uigizaji nipo vizuri”
“Hahaa hongere sana”
“Shukrani aiseee kwa maana mmm”
Safari ikazidi kusonga mbele huku nikimuadisia Stive maisha ya mateso niliyo wahi kupitia katika maisha yangu, sikuwa ni binadamu mwenye furaha kabisi kwa maana kila kukicha kwangu kuna matukio mapya.
“Katika mazungumzo yako yote, chanzo kikubwa cha matatizo yako ni mapenzi”
 
“Usinilaumu  sana kuhusiana na mapenzi kwa maana kila mtu kwenye maisha yake anapenda”
“Ndio kupenda kupo, ila si kuwa mdhaifu kama wewe unavyo fanya. Tazama kuachana na K2 si ndio kumekufanya wewe kuteseka kwa maana, kama unavyo zungumza umesema amekupandikizia kesi za ajabu ukaonekana gaidi, so kama ungekuwa sio kupenda penda kwako, leo hii mama, Diana wote wangekuwepo”
“Stive maisha hayo yamesha pita, usije juu kisa kupenda kwangu au kupendwa kwangu, kwani wewe kwenye maisha yako hukuwahi kupenda wewe”
Nilizungumza kwa kufoka, ikambidi Stive kufunga breki za gafla na gari likasimama kwenye barabara hii iliyopo katikati yam situ. Stive akashuka kwenye gari huku akiwa amekasirika sana, na mimi nikashuka huku nikiangalia jinsi jua linavyo zama taratibu ili kuruhusu giza kuchukua nafasi yake.
 
“Kwa stahili hii Dany utanifelisha katika mipango yangu ninayo taka kwenda kuipanga Somali”
“So unahisi kwamba mimi ninafanya kazi chini yako, au unahisi kwamba mimi nitakuwa mjakazi wako. Sina kaka kwenye maisha yangu haya na wala sihitaji kuwa na kaka kwa maana sikuwahi kusikia habari yako kwenye familia yako”
“Unasemaje Dany?”
Stive alizungumza huku akinisogelea, nikamkazia macho nikakumbuka jana alivyo nipiga taratibu nikaanza kukunja ngumi na endapo atajaribu kuleta ujinga wowote nitamvuruga kama sio mimi.
“Umenisikia, kunisaidia kutoka katika yale mapango usihisi kwamba ndio unaweza kuniongoza akili yangu. Na swala lakuwa ndugu mimi na wewe sahau, huna hata chembe chem…….”
 
Nikastukia ngumi nzito ikitua kwenye mbavu zangu, nikajikunja kwa maumivu makali ninayo yapata. Stive akajaribu kunipiga kigoti ila nikafanikiwa kukiona na kukikwepa kwa kuruka pembeni. Nikasimama wima huku nikimtazama Stive, akanisogelea kwa ajili ya kunipiga, ila katika vitu ambavyo amevikosea kwenye maisha yake ni kujaribu kupambana na mimi. Kitendo cha kunisogelea, nikajirusha hewani na kumrudisha kwa teke zito lililo tua kifuani mwake, sikumpa nafasi ya kujipanga, nikamsogelea na kuanza kumtandika makonde mazito ya uso, kila alipo jaribu kurudisha mapigo yayo, niliweza kumdhiniti kwa kuhakikisha kwamba haingizi ngumi yoyote kwenye mwili wangu.
    Uzuri wa hii barabara haina magari yanayo pita mara kwa mara kwa hiyo, kipigo hichi ninacho mpatia Stive hakina shahidi yoyote ambaye anaweza kwenda kuita waamuzi.
“Stive umekosea sana kujihisi wewe ni mbabe, huniwezi hata kwa ndumba”
 
Nilizungumza huku nikiwa nimemkaba kabali moja ya shingo, iliyo mfanya Stive kuweweseka sana akijaribu kutitoa kwa mikono yake.
“Nieleze ukweli wewe ni ndugu yangu, au ninafunja shingo yao hii”
“Ndio, ndio mimi ni ndugu yako”
“Una uhakika?”
“Ndio Dany”
“Hakuna mpango wowote ambao umeupanga na wajina wezako wa kuniaminisha ili nirudi Somalia mukaniue”
“Hakuna Dany, na…na…aa apia kwa mu….ng…..”
Nilipo muona Stive anaweza kukata roho, nikamuachia kwa kumsukuma chini, akaanza kukohoa huku akijaribu kuvuta pumzi kwa haraka kwa maana kabali niliyo mkaba imempotezea hewa nyingi sana.
“Endapo utajaribu kuenenda kinyume na mimi nitakuvunja shingo sawa?”
“Sawa”
 
Stive aliendelea kunijibu huku badi akiwa ameinama chini akitafuta pumzi. Nikaingia kwenye gari upande wa dereva, nikampigia honim taratibu akaingia kwenye gari huku akiwa ameshika koo lake.
“Nielekeze hapa tunaelekea wapi?”       
“Tunanyoosha moja kwa moja”
“Poa”
Tukaondoka eneo hili na kazi ya Stive ikawa ni kunielekeza njia za kupita hadi tukafanikiwa kufika mpakani. Eneo hili linanikumbusha siku nilipo kuwa ninatoroka kutoka nchini Somalia na watu wa baba hawa ndipo walipo nizuia na kupita mateso mengi.
“Vipi unasubiriwa wewe kufungua kioo”
Stive alizungumza baada ya kuniona nikiwa nimeshikwa na bumbuazi kubwa sana kwa maana macho yangu na akili yangu bado inafikiria tukio ambalo lilinipta katika sehemu hii. Nikashusha kioo na kumtazama afande huyu aliyopo pembeni yangu. Akanipigia saluti kama wanavyo fanya wezake.
 
“Habari yako afande”
“Salama, ninaelekea kwenye oparesheni hapo Somalia”
“Na weza ona kitambulisho chako mkuu”
“Mumeanza lini kuuliza vitambulisho vya mabosi wenu”
Nilizungumza kwa kufoka huku  nikimtazama afande huyu usoni mwake anaye onekana ndio kwanza ni mgeni kazini.
“Samahani afande ndio utaratibu wa hapa”
Taratibu nikatoa kitambulisho changu mfukoni na kumpatia, akakitazama kisha akanirudishia.
“Ninaenda huku, nikirudi nikute barua yako ya maelezo juu ya hili ulilo lifanya”
Nikamkoromea kijana wa watu na kumfanya azidi kunitolea macho, taratibu nikaondoa gari nikafunguliwa geti na kuendelea na safari yangu.
“Tusielekee Mogadishu moja kwa moja”   
“Kwa nini?”
“Ni rahisi kustukiwa, kuna club moja hapo tutafikia kisha tutaanza kupata taarifa zote zinazo endelea katika nchi hii”
“Hiyo Club una iamini vipi?”
 
“Mimi nina wenyeji wangu wengi hapo kwahiyo ni rahisi kwa sisi kukaa pasipo bugza ya mtu yoyote”
“Poa”
Stive akanielekeza sehemu yenye club hiyo na hadi inatimu saa tano usikuwa tukawa tumefika katika club hii niliyo kuta gari nyingi nje, ikionyesha kwamba ndani kuna watu wengi sana.
“Ngoja nishuke kwanza nikaandae mazingira”
“Tunakwenda wote”
“Dany acha ubishi basi, watu hawa wakikuona wewe na hayo mavazi wanaweza kuhisi kwamba nimekuleta hapa kuwapeleleza”
“Kwani hii Club ni ya watu wa aina gani?”
“Dany una maswali mengi hadi muda mwingine unakera. Natambua kwamba huniamini, ila jaribu hata kujenga imani yao kidogo kwangu”
 
Stive alizungumza huku akinitazama usoni mwangu. Nikaka kimya kwa sekunde kadhaa huku nikiendelea kuyasoma mazingiya ya hili eneo.
“Sasa na hili gari la polisi?”   
“Hakuna tabu, kikubwa ninakuomba unisubirie”
“Poa una dakika tano, zikizidi zaidi ya hizo ninaingia ndani mwenyewe”
“Poa”
Stive akashusha kwenye gari akaanza kutembea kuelekea ndani huku akitazama kila eneo la hii Club. Baada ya Stive kuingia ndani ya hii Club, nikachukua begi lenye silaha lililopo nyuma ya gari, nikalifungua, nikatoa bastola moja, nikaitazama kama ipo vizuri, nikaikuta ipo safi, nikaichomeka kwenye buti la upande wa kulia nililo vaa. Nikaitoa laptop ya Stive nikaiangalia vizuri na kuirudisha ndani ya begi kisha begi nikaliweka sehemu nilipo litoa.
 
Baada ya dakika nne, nikamuona Stive akirudi akiwa ameongozana namsichana mmoja mrefu na aliye valia nguo nyeusi, kwa mtazama wa huyu msichana inaonyesha kwamba si msichana wa masihara kabisa.
“Oya Dany twende ndani”
Stive alizungumza huku akichungulia kwenye kioo cha upande wake alio shuka.
“Hili begi je?”   
“Nalichukua”
Tukatazamana na msicha huyu kwa sekunde kadhaa kisha akanikonyeza na kulipokea begi alilo kabidhiwa na Stive. Nikashuka kwenye gari na kulifunga, tukaanza kuelekea ndani, tukafungua mlango na kukutana na mabaunsa wanne wakiwa wamesimama, wakanizuia.
 
“Nipo pamoja naye huyo”
Stive alizungumza na ikawafanya mabaunsa hao kuniachia huku wakinitazama kwa macho makali na ya kunichunguza. Kwenye club hii sikutegemea kuweza kukuta mziki wa wasanii wa kitanzani ukipigwa na watu wanaucheza kwa shangwe sana. Kitu kingine kilicho nishangaza ni uchafu unao fanyika humu ndani.
“Dany unashngaa nini ndio mambo yako”
“Acha ujinga hao ni mashoga?”
“Yaaa leo hakikisha kwamba unatoa ngezi zako zote tukitoka hapa tunafanya kazi tu na si mapenzi sawa dogo”
Stive alizungumza huku tukimtazama jimama moja lililopo juu ya meza kubwa katika hii Club, linacheza uchi kabisa huku likitingisha makalio yake makubwa sana jambo lililo nifanya nijikute nikimeza mate kwa kulitamani.
                                                                           
AISIIIII……….U KILL ME 115
 
“Twendeni”   
Binti aliye beba begi letu alizungumza huku akitutazama, na kutufanya sote kuyatoa macho yetu kwa jimama hilo na kuendelea kumfwata. Kuzimu ambayo siku zote tunaisikia kwenye vitabu vya dini ipo humu ndani yaani kitu kinacho kosekana humu ni moto wa kuwaunguza watu waliomo humu ndani. Tukaingia kwenye moja ya chumba na kukuta mabinti wa kisomali zaidi ya kumi wakiwa wamevalia bikini na sidiria huku wengine wakiwa hawana sidiria kabisa. Kila msicha ninaye mtazama mkono mwake ameshika bastola, huku wengine wakiwa wameshika bunduki aina ya SMG. Tukasimama kwenye meza kubwa huku kwenye kiti kilichopo nyuma ya hii meza kukiwa na jimama kubwa jeusi lililo jichora mwili mzima hadi usoni mwake.
“Stive huyo ndio mdogo wako”       
Jimama hilo lilizungumza kwa sauti nzito huku likinitazama usoni mwangu
 
“Yaaa huyu anaitwa Dany”   
“Mbona anaonekana legevu legevu?”
“Yupo vizuri”
“Ahaa wapi simuamini, hei hembu mpime huyo”
Jimama huyu lilimpa ishara msichana mmoja na watu wote wakasogea pembeni hadi Stive. Msichana mmoja mrefu mwenye kisu mkononi mwake akanisogelea huku akinitazama kwa macho makali sana. Akanitisha kidogo, katika kuyumba kwangu nikastukia akinichana na kisu chake mkononi mwake, watu wote wakashangilia ndani ya chumba hichi.
“Dany usimuonee huruma atakuua huyo”
Stive alizungumza huku akinitazama usoni, nikamtazama msichana huyu kuanzia chini hadi juu. Afya yake aliyo nayo wala haistahili kupambana na mimi na kwa maana amedhohofika hata chupi aliyo ivaa emeibana kisawa wasa kwa mikanda yake.
 
Msichana huyu akajaribu kurusha mateke huku akitoa milio ya ajabu kama waigizaji wakichina wakipigana.
‘Nitakiua hiki masikini wee’
Nilizungumza huku nikiendelea kukikwepa kisichana hichi ambacho kusema kweli hakijiwezi, katika kurusha rusha kwake mateke na ngumi nikamdaka mkono alio shika kisu, nikamtandika makofi si chini ya sita kisha nikasukumia kwa wezake walio kuwa wamesimama pembeni yangu na kuwafanya wote kuanguka kwa pamoja.
“Stive huwa sihitaji majaribio kwenye maisha yangu na kama tumekuja hapa kujaribiana ni bora mimi niondoke”
Nilizungumza huku nikimtazama Stive kwa hasira usoni mwake, taratibu Stive akanisogelea akanishika bega la upande wa kuli huku akiwa katika hali ya huzuni.
 
“Mdogo wangu, hawa watu wanaweza kutusaidia katika kazi ambayo sisi tunaweza kwenda kuifanya. Ninahitaji tuwafanyie ambushi Al-Shabab, kwa sisi wawili ni ngumu sana kwa sisi kuweza kufanikiwa katika hilo”
“Unawaamini vipi hawa watu, ikiwa hakuna hata mmoja ambaye mimi ninamfahamu”
“Niamini mimi Dany, kila jambo litakwenda poa, kuwa mpole katika hili”
“Mdogo wako anaonekana ni mtu wa hasira sana?”
“Yaa kila kitu nitakimaliza mimi wala usijali katika hilo”
“Dogo, sisi kundi letu kaka yako ametuletea kazi, uzuri ni kwamba tuna uhasama mkubwa sana na hao wanaojiita Al-Shabab, na kama utakubali msaada wetu basi tunaweza kukusaidia ila kama huto hitaji msaada wetu unaweza kuondoka”
 
Jimama hilo lilizungumza huku likinitazama usoni mwangu, nikamshika mkono Stive na kumvuta pembeni kwa ajili ya kuzungumza naye.
“Stive isije tukawa tunajiingiza kwenye mitego sisi wenyewe, kwa maana moyo wangu kwa sasa hivi haumuamini mtu yoyote”
“Hilo haliwezekani, huyu bi maza ni rafiki yangu kwa miaka tisa sasa, ananijua na ninamjua vizuri tangu alipokuwa Al-Shabab”
“Kujuana na mtu sio ishu, hivi mimi kama Mariam nilihisi kwamba ipo siku atakuja kunifanyia unyama mkubwa kwenye familia yangu?”
“Hayo ya Mariam hembu achana nayo kwa muda huu, tuangalie ni kitu gani tunaweza kukipanga na huyu mama akatupa vijana wake, kwa maana mimi ninaifahamu kambi hiyo  basi inaweza kuwa rahisi kwetu kuivamia kwa urahisi mkubwa sana”
 
Nikaka kimya kwa muda huku nikimtazam Stive usoni mwake, nikamtazama pia jimama hili lililo kaa kwenye meza yake likiendelea kuvuta sigara kubwa kwa fujo.
“Dany hii ndio nafasi ya pekee kuweza kutimiza kilie ambacho kipo mbele yangu.”
“Poa”
“Ila Dany kesho itabidi mimi nikuache hapa, mimi nielekee kwenye kambi ya Al-Shabab kwenda kufanya upelezi wangu kisha tujue ni wapi tutakapo anzia”
“Uniache hapa?”
“Kuwa na amani, utahudumiwa kwa kila kitu wewe kuwa na amani”
Nikashusha pumzi taratibu, nikarudia kuwatazama watu waliomo humu ndani ya hichi chumba kwa haraka haraka, sijaona msichana ambaye anaweza kuniletea madhara hata kwa kupambana na mimi.
“Fine nimekubali, ila utakwenda kwa muda maalumu sio kwenda na uzamie huko?”
“Itabidi nitumie siku mzima kuwa huko kwa maana bila kufanya hivyo inaweza kustukiwa”
“Poa”
 
Tukarudi mbele ya meza ya jimama huyu,
“Zero, dogo amekubaliana na kila kitu”
“Ahaa dogo karibu kwenye ulimwengo wa Ziro”
“Asante”
Nilijibu kwa unyonge huku nikimtazama mama huyu usoni mwake, likanyanyuka kwenye kiti chake hapa ndipo nilipo weza kuona umbo lake lililo jazia minyama nyama mingi. Akatusogeleka na kunipatia mkono wake wa kulia, nikautazama kwa sekunde kadhaa kisha na mimi nikampatia mkono wangu. Akanivutia karibu yake, akanitazama kwa sekunde kadhaa kisha likanipiga busu la mdomo na kunifanya nirudi nyuma kidogo huku nikiwa nimekunja sura yangu.
“Dogo busu tu unanuna”   
Nikataka kuzungumza kitu ila Stive akaniwahi kuniziba mdomo kwa maana anatambua kitu kitakacho toka kinywani mwangu kinaweza kuchafua hali ya hewa kwa kila mmoja ndani ya chumba hichi.
 
“Ningeomba mutupatie chumba cha kulala”
“Hakuna tabu wee K wapeleke wageni chumba namba ishirni”
“Sawa bosi”
Binti tuliye ingia nanye humu ndani akatuongoza kuelekea katika chumba hicho, akatufungulia na kutupa funguo huku akitukaribisha ndani. Chumba hichi hakina ubora kabisa wa mtu kuweza kulala kwa amani. Kwanza kina harufu ya uvundo, pili kitanda chake mashuka ni machakavu kupita maelezo.
“Oya nitalala kwenye gari na si humu ndani”
“Kwa nini?”
“Ahaa wewe huu uvundo huusikii?”
“Kawaida, acha ubishoo Dany”
“Wewe ubishoo kwenye uvundo, hivi nikiumwa na mafua unahisi kwamba hata hiyo kazi yenyewe nitaifanya kama nilivyo hitaji?”
 
“Poa bwana”
“Unapesa ambayo ninaweza kuitumia kununua hata kinywaji?”
“Fungua kwenye hiyo zipu ya pembeni ya begi utaona kuna vibunda amavyo nimeviweka humo”
Nikafungua zipu aliyo nielekeza Stive nikakuta vibunda vitatu vya pesa za kimarekani, nikachukua kibunda kimoja kisha nikatoka nje. Nikajichanganya kwenye wingi wa watu ndani ya huu ukumbi, nikasimama kwenye kaunta ya kununulia vinywaji, nikaagizia mzinga wa whyne, nikaulipia na kuanza kuunywa taratibu. Wasichana wengi waliopo karibu yangu, macho yao yote yakawa kwangu, sikulijali hilo kwa maana kichwa changu bado kinamuza Cajoli, msichana aliye tokea kujali hisia zangu na kujitolea maisha yake kwa ajili yangu. Nikatoa nje ya Club hii na kuanza kutembea kuywe barabara hii iliyo zungukwa na jagwa kwa maana hata Club yenyewe ipo kwenye jangwa. 
 
Sikuwa na wasiwasi wowote zaidi ya kusonga mbele huku  nikiwa nimeshika chupa yangu ya whyne na kwa mara kadhaa nikawa nikigigida mafumba kadhaa ili mradi kuyatoa mawazo ya Cajoli kichwani mwangu. Katika kutembea kwangu pembezoni mwa barabara nikaona jiwe kubwa lililo chongoka. Kwa mwendo wa ulevi nikaanza kulisogelea hadi sehemu lilipo, nikalitazama vizuri na kuanza kulizunguka taratibu. Gafla nikaona gari zipatazo nne aina ya Toyota pickup, zikipita kwa kasi katika barabara hii wakielekea katika eneo la Clib huku zikiwa zimejaza watu wengi wenye silaha wachache kati yao wakiwa wameshika bendera nyeusi ambazo moja kwa moja niliweza kuzitambua kwamba zimetoka katika kundi la Al-Shabab.
 
Nikataka kujitokea kwenye jiwe hili, ila nikasita hadi gari zote zilivyo pita. Hazikupita hata dakika tano nikaanza kusikia milio ya risasi ikitokea kwenye Club, nikaichomo bastola yangu kwenye viatu vyangu na kuanza kukimbia kueleka katika eneo la Club. Pombe yote ambayo ilisha anza kunitawala kichwani mwangu taratibu ikaanza kunipotea, hadi ninafika eneo la Club, sikuhitaji kuuliza ni kitu gani kinacho endelea ikiwa ninesha ona jinsi wanamgambo hawa wa Al-Shabab jinsi wanavyo endelea kushambulia watu wasio na hatia.
 
‘Leo mutanikoma’
Nilizungumza huku nikiua kila mwanajeshi wa Al-Shabab ambaye kwa sasa wote ni maadui kwangu, sikujali mauaji yangu yanafanyika vipi, nikijisikia kumpiga mtu risasi ya kichwa basi ninampiga kichwani, nikijisikia kupiga risasi ya kifua basi nitampiga hapo. Bastola yangu ikaisha risasi, sikulijali hilo nilicho kifanya ni kuokota bundiki ya adui yoyote ambaye amefariki na nilicho kifanya ni kuendeleaza mashambulizi. Hadi zinatimia dakika kumi, wanajeshi wote wa Al-Shabab, waliopo nje nikawa nimewamaliza. 
 
Nikamuona Ziro akitoka nje akiwa ameongozana na watu wake huku Stive akiwa ni mmoja wapo. Kila mmoja alivyo niona na wingi wa maiti zilivyo sambaa nje wote wakaonekana kushangaa sana.
“Dany Dany Dany”
Stive aliniita huku akinitingisha kwa maana hadi wananifikia, nilikubwa ninamtazama adui mmoja jinsi alivyo lala chini. Nikampiga risasi zisizo na idadi adui huyo aliye lala chini kisha bunduki nikaitupa pembeni.
“Dany tulia mdogo wangu”   
Nikamtazama Stive kwa jicho kali pasipo kumsemesha kitu chochote zaidi ya kuachana naye kutafuta sehemu nikakaa. Ziro pamoja na Stive wakanifwaya eneo nililo kaa, Stive akachuchumaa huku akinitazama usoni mwangu.
“Dany yameisha”  
  
“Yameanza, sihitaji wewe uendee kwenye hiyo kambi, nitahitaji kwenda mimi mwenyewe”
“Dany”
“Ninajua ni nini cha kufanya sihitaji kufundishwa katika hili”
“Dogo, ungeacha tukakusaidia nina vijana wengi”
“Sihitaji vijana wowote, inaonyesha ni jinsi gani wewe na vijana mulivyo wanyonge, mumevamiwa, ni kitu gani cha maana ambacho mumekifanya”
“Dany usizungumze hivyo”
“Sikia Stive. Hii ni kazi yangu na hichi ni kisasi changu, mtu ninaye muhitaji katika kambi ya Al-Shabab ni mmoja tu ama wawili, nikishawapata hao, mimi na wao hatutokuwa na shida nao”
Nilizungumza huku nikisimama, nikaanza kumpitia maiti mmoja baada ya mwengine huku nikiwafungua sura zao.
“Unafanyaje?”
“Nahitaji kutafuta nguo ya kuvaa”
“Unataka kwenda huko peke yako?”
“Ndio”
 
Nikaipata maiti moja ambayo risasi yake imetua kichwani mwake. Kwa haraka nikaanza kumvua nguo zake, nikamuacha na nguo za ndani tu alizo zivaa.
“Dany ila kwenda mwenyewe inaweza kuwa ni hatari kwa upande wako?”
“Stive nina mafunzo mengi sana na si mjinga kama unavyo hisi, tazama hawa jamaa waliwavamia wewe na huyo rafiki yako, wote mulibaki kufunga miliango na kushambulia mukiwa ndani kuna hata adui ambaye muliweza kumua?”
Stive akaka kimya asijua nini cha kujibu. Nikavua nguo zangu na kuanza kuvaa nguo za adui huyu, nikatafuta kilemba ambacho wanajeshi wa kundi hili huwa wanajifunga na vyote huwa vinafanana. Nikajifunga kichwani mwangu na kubakisha macho yangu tu.
 
“Siendi kupeleleza ninakwenda kufanya mauaji. Wewe Ziro tazama baadhi ya wateja wako wameuawa, na siku zote umesema kwamba huwa muna uhasama na hawa jamaa, sasa leo ni nafasi ya nyinyi kulipiza kisasi, kama mutaamua kunifwata sawa kama mutaamua kukausha poa”
“Hatujajipanga na watu wangu kwa sasa wana pombe kichwani”
“Ahaa endeleeni kunywa mutakuja kufa na pombe zenu”
Nikachukua bunduki mbili zilizo jaa risasi, nikaziingiza kwenye moja ya gari la Al-Shabab, nikingia nikawasha na kuondoka katika eneo hili huku kila mmoja akiwa ananishangaa. Kutokana ninafahamu kambi ilipo halikuwa tatizo kubwa sana kwangu kukosea njia.
 
Baada ya kama saa moja na nusu nikafanikiwa kufika katika geti kubwa la kuingilia katika ngome hii ya Al-Shabab, walinzi walipo nisogelea nikaanza kuzungumza kiarubu huku nikiwapa taarifa kwamba wezetu wameuwawa na mimi nimekuja kutoa ripoti.
Mlinzi akakubali kunifungulia geti, nikaingia kwa kasi na nikalisimamisha gari kwenye eneo la maegesho. Laiti kama wangefahamu kwamba mimi sio mwenzao na nimekuja kufanya mauaji ya wakuu wao wanao waabudu kama miingu watu basi wala wasinge weza kuniruhusu kuingia humu ndani. Kwa haraka nikashuka kwenye gari huku nikiwa na bunduki moja mkononi, nikaanza kukimbilia katika nyumba wanayo kaa viongozi.
“Hei”
Niliisikia sauti nyuma yangu, ikanifanya nisimame pasipo kugeuka.
“Unakwenda wapi katika jengo la waheshimiwa usiku wote huu”
Sauti ya mtu huyu sio ngeni kabisa masikioni mwangu, ni sauti ya mwalimu wangu aliyekuwa ananipenda kipindi nikiwa ni mwanachama wa hili kundi.
 
“Wezangu wameuwawa, nimekuja kuomba watu zaidi  kuweza kunisaidia katika kulipiza kisasi”
Nilizungumza kwa sauti nyinyine tofauti kabisa na sauti ambayo mwalimu wangu huyu anaifahamu.
“Usinidanganye, geuka kabla sijakupiga risasi”
Mapigo ya moyo yakaanza kunienda mbio huku jasho likianza kunimwagika usoni mwangu, taratibu nikaanza kuwaza ni jinsi gani ninaweza kumtuliza huyu mwalimu.
“Dany nimekufahamu geuka tu”
Mwalimu kulitaja jina langu ndio akazidi kunizidisha woga na wasiwasi mwingi, taratibu nikageuka na kumkuta akiwa amesimama peke yake huku bastola yake akiwa ameielekezea chini.
“Nifwate”
Alizungumza huku akitazama kila eneo la hapa tulipo simama. Tukaongozana hadi kwenye chumba chake, tukaingia ndani na akawasha taa.
 
“Umekuja kufanya nini Dany?”
“Kwanza umenijuaje mwalimu?”
Nilizungumza huku nikivua kitambaa hichi usoni mwangu.
“Hujanijibu swali langu”
“Nimekuja kumchukua Yudia”
“Yudia, mbona una hatari sana?”
“Kwa nini?”
“Yudia analindwa sana kuliko hata Hawa, na Yudia kwa sasa ana cheo kikubwa kuliko Hawa”
“Kisa ni nini cha Hawa kushushwa cheo ikiwa yeye ni mtoto wa mkuu”
“Kisa cha yeye kushushwa cheo na kupokonywa madaraka yote ni wewe Dany”
Nikabaki nikiwa nimekodolea macho mwalimu kwa maana nina kipindi kirefu sana tangu mimi kuondoka katika hii kambi na sijafahamu ni kitu gani Hawa amekifanya na kinacho nihusu mimi hadi kupokonywa madaraka yake na kukabidhiwa Yudia.

==>>ITAENDELEA KESHO
chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )