Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Saturday, October 27, 2018

AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 126 na 127 )

juu
MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA- 0657072588
ILIPOISHIA   
Mlango wa nyuma ya gari letu ukafunguliwa, wanaume wawili walio funika nyuso zao na kuacha macho yao tu huku mikononi mwao wakiwa na bunduki, wakaanza kuwatoa wezangu mmoja baada ya mwingine ndani ya gari hili na mimi nikawa wa mwisho kutolewa. Cha kusangaza Hawa na wezake wote wao wamesimama ila mimi ndio nimelazwa chini huku mitutu ya bundiki ya wanaume hawa wakiwa wamenielekezea mimi.
“Halooo Dany”   
Sikuamini macho yangu nilipo muona baba Hawa akisimama pembeni yangu, huku mkononi mwake akiwa ameshika bastola tayari kwa kuniua.
   
ENDELEA   
Taratibu nikamtazama Hawa machoni mwake, taratibu Hawa akatazama pembeni akimaanisha kwamba haitaji kutazama mauaji yangu. Gafla tukamshuhudia mwanaume mmoja wa baba Hawa akianguka chini jambo lililo wafanya watu kuanza kumzunguka baba hawa huku bunduki zao wakiwa wamezishika vizuri. Baba Hawa na watu wake wakaanza kukimbilia kwenye gari walilo kuja nalo huku wakiwa wameniacha chini nimelala. Nikaona gari gari mbili nyeusi za FBI zikija eneo hili kwa kasi huku wakiendelea kuwashambulia watu wa baba Hawa ambao nao wapo wengi kiasi.
 
Nikachukua bunduki ya mmoja wa watu wa baba Hawa aliye pigwa risasi, nikaanza kubingiria nayo hadi pembezoni mwa barabara, kwa haraka nikanyanyuka na kupiga goti moja chini huku mguu wangu mwengine nikiwa nimeukunja kwa nyuma. Nikafumba jicho langu la upande wa kushoto huku nikimtazama baba Hawa jisi anavyo ingia kwenye gari lake. Hawa akageuka kwa nyuma, akakiona kitendo changu cha kuhitaji kumua baba yake, kwa haraka akasimama mbele yake jambo lilio nifanua nishindwe kabisa kumshambulia baba yake.
“Shiti”       
Nilizungumza kwa hasira huku nikitazama gari la baba Hawa likiondoka kwa kasi huku magari mengini yakiwafwata kwa nyuma. 
 
“Weka silaha yako chini”   
Nilisikia sauti ya ukali ikitokea nyuma yangu, kwa haraka nikaitupa bunduki niliyo ishika pembeni kisha nikalala chini, askari mmoja akanifwata akanifunga mbingu kwa nyuma na kuninyanyua juu.
“Nahitaji kuzungumza na raisi”   
“Una haki ya kukaa kimya siwezi kufanya hivyo pasipo kupata ruhusa yoyote”
“Sawa nalitambua hilo ila ninahitaji kuzungumza na raisi wa nchi yako”
Nilimuambia askari huyu kwa msisitizo, hakulijali hilo zaidi ya kuniingiza ndani ya gari lake. Askari wa vitengo tofauti tofauti wakaanza kufika katika eneo hili la tukio. Askari huyu akanifungulia mlango, akanifungua pingu za mikono yangu.
“Kuna simu yako kutoka kwa muheshimiwa raisi”
 
“Shukrani”
Nilizungumza huku nikiichukua simu hii anayo nipa askari huyu.
“Ndio muheshimiwa raisi”
“Ohooo asate Mungu upoa salama Dany”
“Nashukuru muheshimiwa raisi kwa hilo, ila hii kazi muheshimiwa raisi nahitaji kuiendeleza kabla watu hawa hawajatoka ndani ya Marekani”
“Dany unatakiwa kupumzika kwa sasa, ajali uliyo ipata ni mbaya”
“Nalitambua hilo muheshimiwa raisi, ila sijaumia. Ninakuomba uweze kuniruhusu kuungana na vikosi vya wanausalama wako wanao watafuta magaidi hawa”
 
“Dany”
“Tafadhali muheshimiwa raisi, sihitaji kukuangusha. Ninawajua hawa magaidi nimefanya nao kazi zaidi ya miaka miwili na ninatambua udhaifu wao”
Raisi akaka kimya kwa sekunde kadhaa huku nikisubiria jibu lake.
“Nimekuruhusu, hakikisha kwamba unawaangusha hao magaidi wote”
“Nashukuru muheshimiwa raisi, ila ninakuomba muheshimiwa raisi ufanye uchunguzi katika kamati yako ya ulinzi kuna msaliti kwa maana watu tuliokuwa tunajua hii oparesheni ni watu wachache sana, sasa kuna mtu atakuwa amevujisha mpango mzima, ndio maana magaidi hawa wameweza kutuvamia kabla hatujafika katika sehemu husika”
 
“Nitalichukualia uangalizi na hilo”
“Asante muheshimiwa raisi”
“Mpatie simu hiyo askari”
Nikairudisha simu kwaaskari huyu, akazungumza na raisi baada ya sekunde kadha akaka simu na kiunitazama usoni.
“Unahitaji nini?”   
“Ninataji mavazi, silaha pamoja na kuweza kujua hawa magaidi hadi kwa sasa wamelekea wapi?”
“Sawa”
Nikaongozaa na askari huyu hadi kwenye moja ya gari kubwa la FBI, nikakabidhiwa nguo ninazo zihitaji ambazo ni mavazi meusi, nikakabidhiwa jaketi la kuzuia risasi pamoja na bastola na magazine nne.
 
“Mumeweza kufahamu ni wapi magaidi hawa wapo?”
“Tumeweza kuwapoteza”
“Kuwapoteza kivipi?”
“Tuliwafwatilia, tukakwakuta magari yao yakiwa yametelekezwa chini ya daraja moja na wao hawapo?””
“Mumeweza kuwafwatilia?”
“Ndio vikosi vinazidi kuwafwatilia”
“Ninaweza kufika katika eneo hilo la tukio?”
“Ndio ila kuna umbali mkubwa kutoka hapa nilipo, inabidi kutumia helicopter kuweza kufika hilo eneo”
“Naomba tufanye hivyo”
Askari huyu akawasiliana na makao makuu yao, na kuomba masaada wa helicopter.
“Itachukua muda gani kufika hapa tulipo?”
“Dakika tano”
“Sawa”
 
Ndani ya dakika tano kama alivyo zungumza  askari huyu, helicopter ya FBI ikatua pembezoni mwa barabara. Mimi na askari huyu moja kwa moja tukakimbilia kwenye helicopter hii na kuingia ndani. Safari ya kueleka katika eneo yalipo telekezwa magari ya magaidi hawa ikaanza. Tukatumia dakika kumi tukiwa hewani, tukafika katika eneo la tukio ambapo napo tukakuta askari wengine wakiwa wamelizunguka eneo hilo likiendelea kufanyiwa uchunuguzi.
“Habari meja Thomsande”
“Salama, meja Barak, huyu anaitwa Dany ni agent anaye fanya kazi chini ya ofisi ya raisi”
“Habari yako agent Dany?”
“Salama tu meja Thomsande”
“Salama tu”
 
“Mumeweza kugundua ni sehemu hani ambayo magaidi wameweza kuelekea?”
“Hadi sasa hivi tumeweza kufanya uchuguzi wote ila hatujaweza kufahamu ni sehemu gani magaidi wamelekea, na hata kamera za hapa hazijachukua tukio lolote na inavyo onekana zimeweza kufutwa matukio yote”
“Je mumeweza kuwafwatilia kwa kutumia satelaiti?”
“Tumejaribu kufanya vyote ila vimeshindikana”
“Je kuna njia za chini?”
“Katika hili eneo hakuna njia za chini ya ardhi kabisa”
Nikalisogelea gari moja ambalo ndio alikuwa amepanda baba Hawa, nikaanza kulikagua kwenye siti za nyuma, katikati ya siti moja na nyingine nikakutana na kipande cha karatasi kidogo sana mbacho si rahisi kwa mtu kuweza kukiona. Nikakifungua na kukuta maandishi yaliyo andikwa kwa damu ya binadamu.
“Somalia”
Niliyasoma huku nikirudi kwa askari niliye kuja naye.
“Umepata nini?”
 
“Wanaelekea Somalia”
“Umejuaje?”
“Kuna hichi kikaratasi kilicho andikwa na damu, kwenye hii gari alipanda baba Hawa pamoja na mwanaye na hii hati ya ya kuandika inafanana kabisa na Hawa.
“Hawa?”   
“Mwanamke ambaye ni mpenzi wake na yeye yupo kinyume na baba yake”
“Basi niwasiliane na wakuu wa viwanja vyote vya ndege, treni pamona na bandari zote ziweze kufungwa ili ulizni uzidi kuimarishwa. “
“Sawa ninaomba kuwasiliana na raisi”
“Sawa”
Raisi akapigiwa simu, nikakabidhiwa simu na kuzungumza naye.
“Dany umepata kitu gani?”
“Wanaelekea Somalia, kwa sasa ningeomba kuweza kupata ndege itakayo nipelekea Somalia moja kwa moja, ili niweze kuwawahi”
“Wewe unahisi watakuwa kweli wanakwenda Somalia?”
“Nina amani hivyo muheshimiwa raisi kwa maana sidhani kama wanaweza kwenda nchi yoyote Duniani, ikiwa wanajua wanataftwa karibia Daunia nzima”
 
“Dany kwa hili inabidi tujirishishe mapema sana kuamini kwamba watakuwa wametoka nje ya nchi hii. Kwani watu wangu wanaendelea kujitahidi kuhakikisha kwamba wanaimarisha ulinzi wa kuweza kuwatafuta”
“Muheshimiwa raisi, kumbuka muda hautusubiri, na laiti kama wangekuwa wapo ndani ya hii nchi tungeweza kupata muongozo kuanzia hapa tulipo. Ila kumbuka muheshimiwa raisi kwamba hawa watu wanapata ushirikiano na watu waliomo ndani ya serikali yako ndio maana mpango mzima umekwenda tofauti na vile tulivyo kuwa tunafikiria.”
Nilizungumza kwa msisitizo ili kummshawishi raisi Donald Bush kuweza kuamini kwa kile ninacho mueleza.
“Muheshimiwa raisi, nimeianza hii kazi ninakuomba unipe nafasi ya kuifanya hadi iishe tafahali”
“Rudi ikulu”
“Muheshimiwa raisi”
“Dany nimekuambia ninakuhitaji hapa ikulu”
“Sawa muheshimiwa raisi”
 
Sikuwa na jinsi ya kufanya zaidi ya kukata simu, wakanifwata askari wawili wengine wakaniomba tueleke kwenye helicopter kwa safari ya kwenda ikulu. Moyoni mwangu nikajisikia vibaya sana kwa kuona raisi anawaachia magaidi hawa kutoka nje ya nchi yake kirahisi namna hii. Nikaingia kwenye helicopter niliyo kuja nayo na safari ya kuelekea ikulu ikaanza. Tukatumi nusu saa hadi kufika ikulu, nikakabidhi bastola yangu pamoja na magazine kwa walinzi wa ikulu kisha nikapelekwa moja kwa moja hadi ofisi ya raisi niliye mkuta akiwa na mwanaume mmoja mweusi.
“Samahani Dany kwa kuweza kukurudisha katika opareheni yako uliyo kuwa umeianza”
“Hakuna tabu katika hilo”
“Kutana na balozi wa Tanzan bwana Jackson Bongole”
“Habari yako muheshimiw a balozi”
 
“Salama Dany, ni muda mrefu sijakuona”
“Nikumbushe uliniona wapi?”
“Nilikuona katika ziara moja ya raisi aliye toka madarakani, ukiwa mmoja wa walinzi wake”
“Nashukuru katika hilo”
“Dany balozi wako amekuja kuomba kusitishwa kwa wewe kutumiwa na Marekani katika kuendesha oparesheni za kuwasaka magaidi, pasipo nchi ya Tanzan kuweza kutambua”
Raisi alizungumza kwa utaratibu huku akinitazama usoni mwangu, nikamtazama balozi Jackson Bongole kwa macho makali sana yaliyo jaa hasira’
“Dany mimi nimepokea amri kutoka nchini Tzania kutoka kwa raisi na sasa unahitajika kurudi nchini Tannia haraka iwezekanavyo”
 
“Ngoja muheshimiwa raisi pasipo kushusha heshima yako mbele ya raisi, ila hicho kitu unacho kizungumza hakiwezekanai kabisa kwenye maisha yangu. Hivi unatambua ni jambo gani linalo endelea duniani kwa sasa?”
“Mimi nimefwata amri ya raisi wangu, na tambua kwamba Tanzania na Marekani tuna ushirikiano mzuri sana ambao unaweza kuvunjia muda wowote kwa ajili yako”
Nikaka kimya huku nikimtazama balozi, nikamtazama raisi Donald Bush, kisha nikayarudisha macho yangu kwa Balozi Jackson Bongole.
“Muheshimiwa balozi, ninakuomba unisaidie kitu kimoja kama huto jali, ninakuomba niweze kuimaliza hii kazi kisha ndio nitarudi Tanzania”
“Dany ingekuwa ni amri yangu ningeweza kukuruhusu urudi Tanzania, ila sio amri yangu. Mimi mwenyewe ninafwata amri na nimepewa masaa kumi na mbili niwe nimekurudisha nchini Tanzania”
 
“Natambua muheshimwa balozi kwamba unafwata amri, ila tambua huyo ambaye amekupa amri hiyo yeye mwenyewe ni adui yangu namba moja”
“Kivipi?”
“Raisi K2 yeye kwanza ndio amehusika na mauaji ya raisi aliye pita kwa uroho wa madaraka. Raisi K2 yeye ndio anahusika na upotevu wa watoto wa kike unao zidi kuendelea nchini Tanzan, na nchi za jirani. Watoto hao anawakuza na kuwafanya wauaji ambao wanafanya kazi za hatari ambazo kwa wanausalama wa kawaida hawawezi kupambana nao, na hicho kizazi chake amekiandaa kwa miaka mingi sana”
 
“Hayo yote wewe umeyajulia wapi?”
“Kabla ya kujua nimeyajulia wapi, yeye ndio aliye waua wazazi wangu, familia yangu nzima damu yake ipo kwa K2, leo hii unanihitaji kurudi Tanzan ambapo karibi watu wote nchi nzima anajua kwamba mimi ni gaidi, ikiwa gaidi mkubwa ni huyo anaye waongoza. Tafadhali muheshimiwa balozi, hili ninalo lizungumza ni kati yako wewe na mimi, tafadhali ninakuomba uniruhusu kuimaliza hii kazi niliyo inaza”
Mueshimiwa balozi Jackson Bongole akakaka kimya huku akionekana kutafakari jibu la kuweza kunipatia.
“Dany”
“Ndio muheshimiwa Balozi”
“Ukiachilia mbali  tu kwamba kazi yangu ninaweza kuipoteza, ila familia yangu pia ninaweza kuipoteza”
“Kivipi?”
“Muheshimiwa raisi K2 ameniambia kwamba nisipo hakikisha wewe unafika nchini Tanzani basi familia yangu ataingamiza”
“Familia yako ipo wapi muheshimiwa Balozi?”
“Ipo nchini Tanzania, hapa nipo na mtoto wangu wa kiume anaye soma chuo”
 
“Samahani muheshimiwa balozi, una ushahidi wa sauti?”
Raisi aliuliza huku akimtazama balozi usoni mwake.
“Ndio ninao muheshimiwa raisi”
Muheshimiwa balozi Jackson Bongole akatoa simu yake ya mkononi na kutuwekea mazungumzo aliyo kuwa anazungumza na raisi K2.
“Hili swala nitalisimamia mimi kama raisi wa Marekani, nitahakikisha nchi yangu inamshihulikia raisi wako nimemvumilia nimeshindwa. Kabla hajaiteketeza familia yako basi nchi yangu itaanza na familia yake. Dany nakuruhusu kuendelea na oparesheni yako hakikisha kwamba hata raisi K2 unamuweka mikononi mwako na ikiwezekana na yeye unamuanguamiza nitakulinda kwa hali yoyote na hakuna serikali itakayo weza kukukamata sawa”
“Sawa muheshimiwa raisi”
Nilijibu huku nikitabsamu, kwa maana K2 sasa ameingia kwenye sehemu ambazo ni lazima mwisho wake utafika na tena utafika kama ilivyokuwa kwa gaidi wa dunia Osama Bin Laden.

AISIIIII……….U KILL ME 127

“Ndege ya kukupelekea Somalia imesha andaliwa, Dany hakikisha kwamba huniangushi katika hili”
“Mungu anitangulie na nitahakikisha kwamba kila jambo linakwenda bizuri”
“Sawa Dany”
Raisi akanyanyua mkonga wa simu iliyopo mezani mwake
“Njooni mumchukue”
Hazikupita hata dakika mbili, wakaingia wanajeshi wawili walio valia mavazi ya jeshi, wakampigia raisi saluti.
“Mshindikizeni Dany hati katika kiwanja cha ndege cha jeshi”
“Sawa muheshimiwa raisi”
 
Nikamsogelea balozi wa Tanzania bwana Jackson Bongole, nikampa mkono huku nikimtazama machoni mwake.
“Ni wakati wa wewe kuwa jasiri na usiwe nyonge katika hili”
“Sawa kijana, kazi njema”
“Asante”
Nikatoka na wanajeshi hawa, tukatoka nje na kuingia katika gari aina ya HAMMER ambalo hutumiwa na wanajeshi hawa. Safari ya kuelekea katika kambi yao ikaanza huku ndani ya gari hili nikiwaza maneno ya Kk2 jinsi alivyokuwa akimmshinikiza balozi Jackson Bongole kuhakikisha kwamba ananipelekea nchini Tanzaa ambapo moja kwa moja ninatambua kwamba nitakapo fika huko ni lazima tu ataniua.
“Tutachukua muda gani hadi kufika kambini?”
 
“Zimebadki dakika kumi”
“Sawa”
Tukafanikiwa kufika katika kambi ya jeshi, nikakambiziwa kwa mkuu wa anga ambaye moja kwa moja akanipelekea hadi katika kiwanja cha ndege ambacho nimekuta kuna ndege nyingi za kivita zikiwa zimejipanga vizuri.
“Kila kitu unacho kihitaji katika kazi yako kipo ndani ya ndege hii, rubani atakupeleka hadi nchini Somali”
“Sawa”
“Ramani nzima pia ipo humo ndani, chukua hichi kifaa, hakikisha kwamba pale unapokuwa umeshikwa kwenye kazi hii, unakitumia kukiminya hii batani basi sisi huku tutakuwa tumeelewa ni kitu gani kinacho endelea na tutahakikisha kwamba tunakufika katika muda mdogo sana kwa maana ndege zetu hizi zinakwenda kwa mwendo wa kasi sana”
“Shukrani”
Nilijibu huku nikitazama kivaa kidogo lilicho kaa kama rimoti ndogo za magari huku kikiwa na batani moja yenye rangi nyekundu.
 
“Nakutakia kazi njema”
“Asante”
Nikaingia katika ndege hii ndogo ya kijeshi ila inaonekana ina uwezo mkubwa sana katika swala la kwenda kasi. Nikaka kwenye siti, rubani akaniomba nijifunge mkanda pamoja na kuvaa earphone ilizopo pembeni ya siti yangu. Nikafanya hivyo kwa haraka sana, taartibu nikaanza kusikia injini za ndege hii zikianza kunguruma, ndege ikaanza kuondoka katika uwanja huu kwa mwendo wa taratibu, kadri muda ulivyo zidi kwenda ndivyo ilivyo zidi kushika kasi na baada ya nusu saa ikaanza kunyanyuka kuelekea juu. Ndani ya dakika moja na sekunde kadhaa ndege ikaka sawa hewani, kwa kupitia earphone nilizo zivaa masikioni mwangu, rubani akaniambia kwamba ninaweza kufungua mkanda na kutazama vifaa vilivyopo kwenye mabegi ndani ya hii ndeg. 
 
    Nikaanza kuchagua bastola ambazo kuseme kweli ni silaha ambayo kwa upande wangu ni rahisi sana kuweza kuitumia na ninapo mlenga mtu huwa ninahakikisha kwamba ninamuangusha. Nikachukua na bunduki mbili kubwa moja ikiwa ni ‘HK M27 IAR’ na nyingine ‘FN SCAR MK 17 ambayo kila mmoja ina uwezo mkubwa sana katika mashumbulizi hususani ya mbali na maadui wangu. Nikachukua mabomu sita ya kurusha kwa mkono. Nikachukua ramani ya inayo onyesha inchi ya Somalia, nikaanza kuiptia taratibu, nikaona ni sehemu gani ambayo kambi ya Al-Shabab ipo, nikachukua peni na kuizungushia dura.
“Dany una simu yak kutoka ikulu”
Rubani alizungumza, nikatazama pembeni ya siti yangu nikaona simu, nikaichukau na kuiwekea sikioni.
“Dany”
“Ndio muheshimiwa raisi”
“Ndani ya hiyo ndege kuna kofia za kijeshi, ningeomba uvae moja, ina kamera ambayo itaonyesha kila unapo kwenda na sisi huku ikulu tutakuwa tunafwatlia hatua baada ya hatua kila unapo pita”
 
“Sawa muheshimiwa raisi”
Nikachukua kofia moja ya rangi nyeusi mama mavazi yangu, nikaitazama vizuri na kuona kamra ndogo iliyopo mbele katika hii kamera, nikaivaa vizuri na kuikaza mikanda yake.
“Hapo tunakupata, pia kuna kinasa sauti naomba ukivae utakuwa unazungumza na mimi moja kwa moja”
“Sawa muheshimiwa raisi”
Nikafungua kijiboksi kidogo sana mithili ya viboksi vinavyo wekea pete za ndoa, nikatoa kifaa cha mwasiliano na kukichomeka katika sikio langu la kushoto.
“Muheshimiwa raisi unaisikia?”
“Ndio ninakusikia Dany”
“Hata mimi ninakusikia”
“Tuambie hadi sasa kwenye hiyo ramani umeweza kugundua kitu gani?”
“Katika hii ramani, sehemu hii ndipo kwene kambi ya Al-Shabab”
Nimuonyesha muheshimiwa raisi, nina imani kwamba anaona kila kitu kutokana na kofia ngumu niliyo ivaa na yenye kamera.
 
“Ndio”
“Haya ndio maeneo yao makuu na si rahisi sana kwa mtu kuweza kufahamu kwamba kuna kambi”
“Ila ni jangwani?”
“Yaa ni jangwani sana na si rahisi kwa mtu kuweza kuiona sehemu”
“Ukifika basi utatusaidia, tumesha andaa wanajeshi mia moja wa Marekani kutokea katika kambi yetu ya jeshi iliyopo hapo Somalia”
“Sawa muheshimiwa raisi, ila ningewaomba waweze kutulia hadi pale nitakapo hakikisha kwamba nimewapa amri ya kuweza kuingia katika kambi, kazi yangu kubwa ni kumkamata mkuu wa Al-Shabab, la sivyo tukicheza vibaya atatutoka mikononi mwetu muheshimiwa raisi”
 
“Sawa, wewe ndio chief kamanda wa hiyo oparesheni”
“Nashukuru muheshimiwa raisi”
Safari ikazidi kwenda mbele huku mara kwa mara nikiandaa silaha zangu, kuhakikisha kwamba hakuna silaha ambayo inaweza kuniletea shida yoyote pale nitakapo kuwa kazini.
“Tuna dakika kumi kufika katika anga la Somalia, unatakiwa uvae parachute”
Rubani alizungumza, nikajikuta nikianza kuingiwa na wasiwasi mkubwa sana kwani kwenye maisha yangu sijawahi kuvaa parachute na wala katika mafunzo niliyo yapata katika chuo cha NSS, wala sikuwahi kuambiwa kwamba kuna swala zima la kuvaa parachute. 
 
Sikuwa na jinsi ya kufanya zaidi ya kuchukua begi la parachute, nikalivaa na kufunga mikanda yake, nikasoma maelezo yake jinsi ya kufanya ninapohitaji kulifungua. Ikanilazimu kichwa changu kuelewa haraka sana kwa kila jambo nililo lisoma kwenye hili parechati.
“Begi langu la silaha vipi?”
“Hilo nalo utalishusha kabla yaw ewe kuruka”
“Nitalipatia wapi?”
“Likifika tu chini begi, kwenye PDA yako hiyo hapo pembeni utaweza kuona ni wapi limeangukia na utalichukua”
“Kama ni mbali”
“Sidhani kama ni mbali”
Nikatazama kivaa changu kidogo(PDA) kilicho kaa muundo wa simu, hichi kinatumika kwa ajili ya kuweza kutazama ramani kwa njia ya mtandao, na hata kutumia picha kadhaa kwa njia ya mtandao.
“Dany una dakika tau kuwa tayari”
“Sawa”
 
“Kuha miwani ya kuzuia upepo hujaivaa, vaa kabla hujaruka”
“Ipo wapi?”
Tazama kwenye begi la kushoto kwako”
Nikatazama begi la kushoto kwangu, nikalifungua kwa haraka na kutoa miwani kubwa, nikaivaa na kuikaza mikanda yake nyuma ya kichwa changu.
“Una dakika moja na nusu kaa tayari mlangoni, hakikisha unatanguliza begi”
“Sawa”
“Kwa sasa Somalia ni saa nane usiku”
“Nimekuelewa”
“Una sekunde thelathini kaa tayari”
Mlango wa ndege taratibu ukaanza kufunguka, kusema kweli jinsi upepo mwingi unavyo ingia ndani ya hii ndege ukanifanya nianze kuchanganyikiwa”
“Tupa begi Dany”
Sikuwa na hata jaja ya kulisikua begi kwani upepe unao ingia wenyewe ukalivuta begi na kulitoa.
“Ruka”
 
Nikaachia sehemu nilizo kuwa nimeshikilia na kujitosa angani. Nikaanza kuzungushwa zungushwa hewani, huku kwa mara kadhaa nikijikuta nikipiga mayowe, ambayo natambu kabisa yanasikika hadi ikulu.
“Dany Dany”
Niliisikia sauti ya muheshimiwa raisi akiniita.
“Ndio, naanguka”
“Tulia, bana pumzi, hakikisha viongo vyako unavikaza, bana miguu yako pamoja na mikono”
Nikafanya kama alivyo niangiza muheshimiwa raisi, taratibu nikajikuta nikianza kuhimili kasi ninayo kwenda nayo chini. Nikajikuta miguu yangu sasa ikiwa ndio inaelekea chini tofauti na nilivyo toka kwenye ndege kwani kicha ndio kilikuwa kimetangulia kwenda chini.
 
“Unaweza kufungua parachute, minya batani katika bega lako la kushoto”
Niliendelea kuyasikilia maelekezo ya raisi, ambaye ameamua kuisimamia hii opareheni yeye mwenyewe japo kuna watu ambao wanapaswa kuisimamia hii oparesheni. Nikaiminya batani iliyopo kwenye mikanda ya hili parachute, fuko kubwa likajitokea kwa juu yangu, sasa hapa nikaanza kupata muhimili mzuri. Nikashika vijikakamba viwili vilivyopo pembeni yangu na kuanza kuliongoza parachute hili, nikaanza kuvuta pumzi taratibu huku nikizidi kwenda chini. 
 
Nikaanza kuikwepa miti ailiyopo katika eneo hili hadi nikafanikiwa kutua chini huku nikikimbia ili kuhimili fuko hili kubwa linalo jikunja lisinifunike. Nilipo hakikisha kwamba nimesimama, nikavua begi la parachuti hili na kuanza kulikusanya kwa haraka, kisha nikalificha kwenye moja moja ya kichaka hata kama ikitokea kwamba nimeshuka katika eneo la maadui basi wasiweze kujua ni kitu gani kinacho endelea. Nikatoa PDA, yangu nikaminya batani ya pembeni, nikaona alama nyekundu inayo onyesha ni wapi bebi langu lilipo, cha kumshukuru Mungu si mbali na eneo hili nilipo.
 
    Nikachomoa bastola yangu na kuanza kutembea kwa umakini katika msitu huhu uku nikifwata maelekezo ya PDA yangu niliyo ishika mkononi mwangu.Nikakaribia eneo ambalo ndipo begi langu limeangukia, nikaona taa za tochi zilizo nifanya nijibanze kwenye moja ya mti.
Mwanga wa mbalamwezi ukanifanya niweze kuwaona watu hawa vizuri, ni wanajeshi walio valia mavazi mavazi ya serikali ya Somalia. Mmoja wao amefungua begi langu na kutoa magazine ya bastola zangu.
“Muheshimiwa raisi kuna wanajeshi wa serikali wanaonekana kulikagua begi langu, na endapo watatoa taarifa kwa wezao inaweza kuwa tataizo kwangu”
 
“Unaweza kujisalimisha mikononi mwao?”
“Nini!!?”
“Nitazungumza na raisi wao na wanaweza kukuachia ndani ya muda mfupi tu na utaendelea na oparesheni yako”
“Hakuna wa kumuamini muheshimiwa raisi katika hili, hawa ndio wanao ogoza kula rushwa kutoka katika kundi la Al-Shabab ndio maana wanashindwa kukabiliana na hili swala”
Nilizungumza huku nikifunga kiwambo cha kuzuia sauti kwenye bastola yangu, nikajisogeza kwenye mti mwingine taratibu pasipo wao kuweza kuniona. Kitendo cha mwanajeshi mmoja kunyanyua simu yake ya upepo na kuhitaji kuwasiliana na wezake ikawa ni kosa kubwa kwangu kwani sikuwa na jinsi ya kufanya zaidi ya kumuua mwajeshi huyu kwa kumpiga risasi ya kichwa jambo lililo mfanya mwenzake kubaki akiwa ameduwaa asijue hata cha kufanya kwani mkononi mwake hana hata silaha ya kujitetea.

==>>ITAENDELEA KESHO
chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )