Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Monday, October 1, 2018

Baraza la Wazee CHADEMA Lasema Lina Ushahidi wa Wabunge na Madiwani Wao Kununuliwa na CCM

juu
Baraza la Wazee wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) limesema hatua ya baadhi ya viongozi na wanachama wa vyama vya siasa kuhamia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kunatokana na shinikizo kutoka katika chama hicho tawala.

Wakizungumza na waandishi wa habari wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wazee Kimataifa, Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa Chadema, Hashim Juma Issa, na katibu wake  Roderick Lutembeka  wamesema baadhi ya viongozi huzushiwa kesi kwa lengo la kuwatishia ili wahamie chama tawala.

Katibu wa baraza hilo  Roderick Lutembeka amesema Chadema inaposema wabunge na madiwani wao wanaoamia CCM wananunuliwa inao ushahidi.

"Suala la ushahidi wa wabunge na madiwani kununuliwa tunao na tuliwahi kutoa ushahidi wa mkuu mmoja wa wilaya akizungumza na kupanga mipango yote. Ushahidi huo tuliupeleka Takukuru lakini ukafunikwa funikwa," amesema Lutembeka na kuongeza;

"Kuna mtu kahamia juzi tu hapa, kafika huko kaanza kufanya mambo ya ajabu, kuna kijana mmoja alichukua mkopo alikuwa rafiki wa huyo mtu, alikuwa akimlazimisha ahamie huko ushahidi wa ushawishi huo tunao"


Katika hatua nyingine, baraza hilo limetoa maazimio ya sera mpya ya Chadema na kudai linaunga mkono sera hiyo ambayo pia imewagusa wazee.

"Leo ni siku ya wazee tunaona tuitumie siku hii pia kutoa maazimio yetu juu ya sera mpya ya Chadema tunaona sera imeelezea namna itakavyotatua changamoto za wazee" amesema Lutembeka.

Lutembeka amesema miongoni mwa maazimio ya wazee ni kuunga mkono sera hiyo katika kutatua changamoto za wazee ikiwamo huduma za afya kwa wazee.
chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )