Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Wednesday, October 3, 2018

Jeshi la Polisi Dar Laingiza Bilioni 2.74 Kwa Makosa ya Barabarani

Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa amesema Makosa mbalimbali ambayo yanafanywa na wanaoendesha vyombo vya moto barabarani yamesababisha Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kupata zaidi ya Sh.Bilioni 2.74.

Mambosasa aliyasema hayo jana ambapo alifafanua  kuwa jeshi hilo linaendelea na operesheni ya kuwasaka madereva wa magari na watumiaji wa vyombo vya moto ambao hawazingatii sheria ya usalama barabarani.

Alisema  katika operesheni hiyo wamefanikiwa kukamata magari madogo,maroli, pikipiki na daladala ambapo wahusika wametozwa faini ambapo zaidi ya Sh.Bilioni 2.74 zimepatikana.

Kamanda Mambosasa amewawataka watu ambao wametozwa faini za barabani kulipa kwa wakati kwani kuna tabia ya kulimbikiza deni na wataendelea kuwasaka wadaiwa wote na iwapo watashindwa gari litachukuliwa na kuwekwa Polisi.
chn
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )