Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Wednesday, October 17, 2018

Jibu la Gigy Money Kuhusu Kujiunga lebo ya WCB

juu
Msanii  wa Bongo Fleva, Gift Starnford maarufu Gigy Money, amesema hajawahi kufikiria kujiunga na lebo ya WCB na kama ingemlazimu kufanya hivyo angeenda kuwa Diamond wa kike.

Gigy anasema anaamini kila msanii ana nafasi ndani ya kazi zake na hajawahi kufikiria kujiunga na kundi hilo kwa kuwa uwezo wake ni wa kipekee.

“Si kwamba WCB kusingetimiza ndoto zangu, nina malengo ya mbali sana na kama ungenilazimisha nijiunge pale basi labda ningeenda kuwa Diamond wa kike, yaani nifanye zile kazi anazofanya yeye na kitakachotutofautisha na jinsia pekee,” amesema Gigy Money.

Ameongeza kuwa kitendo cha kuwa karibu na Diamond kimezidi kumpa uthubutu na kuona ana deni kubwa mbele ya mashabiki zake huku akidai amekuwa akipata msaada mkubwa wa jinsi ya kuongeza ufanisi wake kutoka kwa staa huyo.
chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )