Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, October 18, 2018

Leo Ni Siku 7 Tangu Mo Dewji Atekwe...Hii Ni Kauli Mpya ya Haji Manara

juu
Ikiwa zimetimia siku saba hii leo tangu mfanyabiashara maarufu barani Africa na mwekezaji wa klabu ya Simba, Mohammed Dewji ‘Mo’ alipotekwa na watu wasiojulikana .

Afisa Habari wa klabu ya Simba ambaye alikamatwa siku ya pili baada ya tukio kutokea na kuachiwa siku chache baadaye baada ya kuhojiwa, ameendelea kumkumbuka Mo Dewji kwa kuandika mfululizo wa kauli mbalimbali zenye kuwafariji mashabiki na wanachama wake wa Simba.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram hii leo, Manara ameandika;” Wiki moja kamili imetimia toka tukio la kutekwa kwa kiongozi wetu litokee, MO kwangu mimi binafsi ni tukio baya sana toka nimeanza kazi Simba na moyo wangu bado umesinyaa, tuendelee kumuomba Mola apatikane akiwa mzima na salama.

“Naamini Dua na Sala zetu zitasikika na Insha'Allah kwa jitihada za vyombo vyetu na matakwa yake Mwenyezi, mambo yatakaa sawa." Ameandika Haji Manara

Katika jitihada za kumpata Mo Dewji, familia yake imetoa ofa ya kiasi cha Shilingi billioni 1 kwa mtu yeyote atakayetoa taarifa za ukweli za kupatikana kwake huku Jeshi la Polisi likiwashikilia watu saba mpaka sasa kwa mahojiano zaidi, baada ya kuwaachia kwa dhamana watu 19 mapema wiki hii akiwemo Haji Manara.
chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )