Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Saturday, October 27, 2018

Mwanafunzi Anusurika Kifo Baada ya Choo cha Shule Kutitia.......Tazama Picha

juu
Mwanafunzi  wa darasa kwanza katika Shule ya Msingi Seliani, wilayani Arumeru mkoani Arusha, Emanuel Zakaria (7), amenusurika kufa baada ya kutumbukia ndani ya choo cha 
shimo.


Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Ramadhani Ng’azi, alithibitisha
kutokea kwa tukio hilo jana wakati mwanafunzi huyo alipokwenda 
kujisaidia wakati wa mapumziko.

“Tunaangalia chanzo cha kuvunjika kwa shimo hilo ni nini na
ukizingatia sasa hivi ni kipindi cha mvua kubwa zinazoendelea 
kunyesha, tutaangalia pia kama ujenzi haukuwa madhubuti au ni
kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha bado tunafanya uchunguzi wa
tukio hilo,” alisema.

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Jerry Muro, alisema tukio hilo lilitokea
 majira ya saa 3: 45 asubuhi muda mfupi kabla ya muda wa mapumziko.


Alisema mwanafunzi huyo, mkazi wa Kijiji cha Olevolosi, baada ya kuopolewa, alipelekwa kwenda kupata matibabu katika Hospitali ya Selian na kwamba hali yake 
inaendelea vizuri.

Muro alisema lilitokana na kutitia kwa ardhi 
kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali ya mkoani
 Arusha.


Mkuu huyo wa wilaya aliwapongeza wananchi wa eneo hilo kwa utayari na kutoa kwa moyohali ambayo ilisaidia kunusuru maisha ya mwanafunzi huyo.


“Niwapongeze wananchi kwa utayari wa moyo wenu wa kujitolea, serikali 
inataka watu wenye moyo wa kujitolea kama walivyofanya leo (jana)
 kuokoa maisha ya mwanafunzi huyu,” alisema.

Hata hivyo, alisema Serikali ipo tayari kuungana na wananchi katika
ujenzi wa choo cha kisasa hadi kitakapokamilika.


“Nimeshatoa maelekezo kwa Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Arusha, waanze mchakato wa ujenzi wa choo kipya, Jumatatu, nitakuwa
 shuleni hapo kushirikiana nao ili kuhakikisha ujenzi huo
 unakamilika kwa wakati,” alisema.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Olevolosi, Samweli Mollel, alisema baada ya
kutokea kwa tukio hilo, waliwaita wanafunzi wote madarasani ili
 kuwafanyia uhakiki kwa majina kuangalia watoto kama wapo wote.
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )