Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, October 18, 2018

Mwanafunzi Kidato ch Tano Ajinyonga Jijini Mwanza

juu
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza  tunamshikilia mtu mmoja aitwaye Bilenjo Paul, miaka 46, mkazi wa Igombe, kwa kosa la kupatikana na pombe  ya moshi (gongo) kiasi cha lita arobaini (40) pamoja na dawa ya kulevya aina ya bhangi kiasi cha kilogram mbili (2) , huko maeneo ya Igombe Wilaya ya Ilemela  Jiji na Mkoa wa Mwanza, kitendo ambacho ni kinyume cha sheria.

Tukio hilo limetokea  tarehe 17.10.2018 majira ya saa 11:00hrs baada ya Polisi kufanya doria maeneo tajwa hapo juu  na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo akiwa na kiasi hicho cha pombe ya moshi/ gongo pamoja na dawa ya kulevya aina ya bhangi. Jeshi la Polisi tunaendelea na uchunguzi  pindi uchunguzi ukikamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza  tunatoa onyo kali kwa wananchi wote wanaojihusisha na shughuli hizo za uuzaji na utumiaji wa pombe haramu ya gongo na dawa za kulevya waache mara moja na endapo mtu/watu watabainika hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

Katika tukio la pili, mwanafunzi mmoja  wa shule ya secondary ya Sengerema high school aitwaye  Ayoub Yahya @ Petro , miaka 19, anayesoma kidato cha 5 mchepuo wa PCB, mwenyeji wa Kyerwa-Kagera,  amekutwa akiwa amejinyonga hadi kufa kwa kutumia kamba ya neti (chandarua) aliokua ameifunga kwenye mti uliopo pembeni ya uwanja wa mpira wa shule hiyo, iliyopo  Wilayani Sengerema Mkoa wa Mwanza.

Tukio hilo limetokea tarehe 18.10.2018 majira ya saa 06:00hrs asubuhi, hii  ni baada ya wanafunzi wenzake kupita eneo la uwanja wa shule kisha kuona mwili wa marehemu ukiwa unaning’inia juu ya mti na kutoa taarifa kwenye uongozi wa shule ambao ulifikisha taarifa hizo kituo cha polisi.

Polisi tulifanya ufuatiliaji wa haraka hadi eneo la tukio na kuukuta mwili wa marehemu mahali hapo. Chanzo cha mauaji hayo bado hakijafaamika, Polisi bado tunaendelea na uchunguzi kuhusiana na tukio hilo. Mwili wa marehemu umehifadhiwa hospitali ya DDH Sengerema kwa ajili ya uchunguzi pindi uchunguzi ukikamilika utakabidhiwa kwa ndugu wa marehemu kwaajili ya mazishi.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza linatoa wito kwa wananchi waendelee kutoa  ushirikiano kwa kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu ili waweze kukamatwa na na kufikishwa katika vyombo vya sheria.
chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )